Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1541 to 1550 of 2266.

  • 12 Nov 2019 in Senate: Ahsante sana, Bwana Spika. Ninataka kujiunga na ndugu yangu, Seneta wa kaunti wa Wajir, Sen. (Dr.) Ali, kuzungumzia madeni ambayo yanadaiwa serikali za kaunti. Siongei kuhusu serikali ya kaunti fulani bali ninaongea kuhusu serikali zote za kaunti. Hizi kaunti hulipa watu wengine na hawalipi wengine ilhali wote wamefanya kandarasi ndani ya serikali za kaunti na hilo ni jambo la kusikitisha. Utapata ya kwamba, wale wanaofaidika katika hizi kaunti ni wale mabwenyenye. Wanabiashara wadogo katika kaunti ambao wanajaribu kujikimu kimaisha na biashara zao ndio wanapata taabu. Kwa hivyo, hii taarifa ni muhimu sana kwa taifa letu la Kenya kwa sababu linazungumzia ... view
  • 12 Nov 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: tatu kabla ya kuwalipa. Baadaye, unapata ya kwamba, pesa walizopata kwenye benki inashinda deni walilokopa. Watu wengi wamekuwa na ugonjwa wa moyo, wengine wamejitia vitanzi na wengine wamekufa. Si haki mtu kutokulipwa baada ya kufanya kazi. Taarifa hii ni muhimu sana katika nchi yetu. Magavana wanafaa kulipa watu ambao wamefanya kandarasi. Wale chief officers ambao wanazembea kazi zao kwa kuwalipa marafiki wao wanafaa kuchunguzwa na ikipatikana eti wanafanya hivyo, basi hatua ichukuliwe. Ninaunga mkono kauli hii ambayo imeletwa na ndugu yangu ambaye ni jabali katika lile Bunge la Kiafrika, kule Johannesburg, na vile vile katika Bunge la Seneti. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Asante, Bw. Spika. Pia, ningependa kumpa kongole ndugu yetu, Sen. Cherargei, kwa kuleta Taarifa hii. Ni vyema kuwa na ndege zitakazoweza kuchukua watu sehemu kidogo; ambapo malipo yake pia yatakuwa ya kadri. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Lakini, Bw. Naibu Spika, ikijiri kwamba tunataka ndege za usafiri, na hali iwe nadra, itakuwa jambo la kusikitisha kuona ya kwamba wakati tukitafuta ndege ambazo pengine zitakuwa zinasafirisha watu kwa bei nafuu, lakini zinahatarisha Maisha yao. Hivyo basi, ingekuwa bora ndege hizo zipigwe marufuku kuliko kuhatarisha Maisha ya watu, hata kama ni ya watu wawili au watatu wakiwa ndani ya ndege hizo. Bw. Naibu Spika, tunaona hatari kubwa katika uwanja wetu wa ndege wa Wilson. Naunga mkono aliyoyasema Sen. Cherargei, kwamba hata hali ya ulinzi sio njema. Nikiwa mmoja wa wale wanaosafiri na ndege hizo mara kwa mara, nimeona kwamba ... view
  • 12 Nov 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: basi kuingia ndani ya Uwanja wa Ndege wa Wilson ni kama tu kuingia ndani ya mlango wa hospitali. Kwa hiyo, uangalifu wa Uwanja wa Ndege pia unahitajika katika kitengo hiki; na pia kamati yetu ya uchukuzi inafaa iangalie jambo hili kwa kina. La mwisho, Bw. Naibu Spika, ni kwamba kama vile ilivyosemwa hapo awali, uwanja huu upo katika hali ya kusikitisha hata kama unatumiwa na vifaa hivyo vya kusafiri, kama ndege. Wakati ukija na ndege hiyo ndogo, utaona vile utakavyodunda, urudi hewani kwanza, halafu ndio uregee tena uendelee mpaka ndege isimame. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Ndio; ndege inadunda kama mpira. Haiwezi kutambaa kisawasawa hadi isimame. Nikiwa mmoja wa wasafiri, kila siku moja au mbili zinazopita, hujiandaa kwenda nyumbani kwa kutumia ndege hizo katika uwanja wetu wa Wilson. Bw. Naibu Spika, kama nilivyosema, hivyo ndiyo ndege hizo zinavosafiri. Ndio sababu jambo hili ni la kusikitisha, kuweza kutambua ni ndege gani. Lakini kwa hivi sasa, ambavyo wananchi wanajua kwamba ni Silverstone, basi ni lazima kampuni hiyo wajikakamue. Kama wanahitaji ndege zao kuendelea kutumia uwanja huo, basi walete ndege ambazo hazitahatarisha Maisha ya watu. Kwa hivyo, naoimba Kamati yetu ya Uchukuzi ichunguze zaidi uhamasishaji wa watu wanaosafiri kwenda ... view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono kuongeza muda kwa hii Kamati inayochunguza vifaa vilivyopelekwa katika Kaunti vya kusaidia wananchi kiafya katika kaunti tofauti katika taifa la Kenya. Ni ukweli kabisa kwamba kazi iliyopewa kamati hii nikiwa mmoja wao ni ngumu sana. Taifa nzima la Kenya limepewa vifaa kama hivi katika kaunti zote 47 vitumiwe kusaidia hospitali. Hata hivyo, uzito ni kwamba katika uchunguzi kupatikana kwa watu hawa kuja kutueleza na sisi kuenda kule kuangalia vile vifaa inachukua muda. view
  • 12 Nov 2019 in Senate: Kwa hivyo, ningependa kusema kwamba shughuli kama hii inatakikana iangaliwe kwa kina ili kuleta ripoti. Vifaa vingine ambavyo vinadhuru wananchi kiafya vimepelekwa katika sehemu fulani ambapo hakuna madaktari maalum. Tunauliza ni kwa sababu gani watu ambao sio wataalamu wanaruhusiwa kutumia vifaa kama vile vya upigaji picha na hawawezi kujua wataweka miale ya aina gani ambayo itaingia katika mwili wa binadamu? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus