12 Nov 2019 in Senate:
Kazi iliyoko mbele yetu ni ngumu na inahitaji muda. Ninafikiria muda uliokubaliwa katika Kamati kwamba wanaomba muda wa siku 45 ni kadiri. Si muda ulioongezwa zaidi ama kidogo. Natumaini kwamba katika muda huu wa siku 45, tunaweza kuafikiana na kufika mwisho wa safari yetu. Pia, tunaweza kuleta ripoti muhimu na iliyokamilika ya utumiaji wa vifaa hivi hospitalini.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu wa Spika. Naunga mkono.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuunga mkono na kuafiki Hoja ambayo imependekezwa na ndugu yetu, Sen. Olekina. Katika kizingumkuti hiki kwamba naibu wa gavana atakuwa hana mamlaka ama katika harakati ya kwamba atachukua ofisi nusu awache nusu, tunaona ya kwamba jambo hili limeleta hali ya sintofahamu. Kwa hivyo, Hoja hii ni muhumi ili iweze kufananua kamili ya kwamba kazi ya Gavana itaanza hapa na kuishia hapa na kazi ya naibu gavana itaanzia hapa na kuishia hapa. Hii ni kwa sababu wakati wa uchaguzi, hao wawili watasimama pamoja. Sheria inatumia neno “shall” kumaanisha kwamba ni lazima itekelezwe ...
view
5 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Singependelea kabisa kuingilia kati dada yangu katika heshima---
view
5 Nov 2019 in Senate:
Nimesema yeye ni dadangu---
view
5 Nov 2019 in Senate:
Asante. Sen. Kabaka ni wakili, lakini kwa sababu ni mara yake ya kwanza kuwa hapa, ni sawa kumkosoa kidogo.
view
5 Nov 2019 in Senate:
Bw. Naibu Spika, dada yetu, Sen. Omanga, amesema “mtondo na mtondogoo.” Hiyo ni lugha ambayo hatuwezi kuifafanua kisawasawa. Sijui kama ni sawa angelisema “kesho, kesho kutwa, kisha afike mtondogoo. Asante, Bw. Naibu Spika.
view
23 Oct 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili pia mimi niongeze kuunga mkono hii Kauli ya ndugu yangu mdogo, Sen. Loitiptip, Seneta wa Lamu. Bw. Spika, jambo la kusikitisha ni kwamba, kwa miaka mingi, tumeona watu wa Lamu wakiwa kana kwamba sio Wakenya. Jambo la kwanza ni kwamba, hata ardhi ya watu wa Lamu pia imekuwa sasa sio yao. Watu wa Lamu wenyewe wanajulikana kwamba wanao Uamu wao. Lakini hivi sasa, ukifika huko, ni jambo la kusikitisha kuona The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained ...
view
23 Oct 2019 in Senate:
kwamba ardhi yao imekua kama mbuga ya wanyama. Kila mtu ni mgawo; kila mtu ni kinyang’anyiro. Hivi sasa, watu wa Lamu hawana mahali popote pa kuishi. Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba, vipande vikubwa sana vya ile ardhi ya Lamu vimechukuliwa na mabepari. Na hao ambao sio wengine, lakini ni Waafrika weusi, na ni Wakenya matajiri ndani ya Serikali ya Kenya. Pia, kumekuwa na ugawanyaji wa mashamba. Hivi sasa, tunaona kwamba baada ya kuporwa yale mashamba, sasa kumeingia jambo la kutengenezwa kwa bandari ya Lamu. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha pia kwamba, sisi kama watu wa eneo la pwani, ...
view
23 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, Bunge la Seneti lazima lijitokeze wazi wazi na kuhakikisha kuwa walemavu katika taifa letu la Kenya hawateseki. Shule kama vile Thika School for the Blind ilianzishwa hata kabla nchi hii kupata Uhuru. Shule hiyo inasaidia watoto wengi vipofu hapa Kenya. Mzazi yeyote aliye na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view