Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1561 to 1570 of 2266.

  • 23 Oct 2019 in Senate: mtoto kipofu au kiwete humpeleka huko. Shule hiyo inasaidia kila Mkenya kwa sababu wanafunzi wa shule hiyo hutoka kila eneo la Kenya. Ni aibu kuwa, pesa za kuwasaidia wanafunzi vipofu au wenye ulemavu fulani haziwafikii. Hayo ni mateso na huenda watoto hao wakafa. Ninavyoongea sasa, Thika School for the Blind haina pesa za chakula. Hiyo inamaanisha kuwa wanafunzi hao wanateseka. Sen. Mwaura ameleta Kauli ya maana sana na ninaiunga mkono. view
  • 25 Sep 2019 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza, kuna tabia inayoitwa utovu wa nidhamu, kwa sababu ya hawa mabepari wa ufisadi, haswa tamaa ya pesa iliyoingia zaidi katika huyu mwekezaji ama mwenye jengo hili. Hili ni jambo la kusikitisha kuliona likitendeka nchini Kenya, kwa sababu yeye alithamini pesa kuliko maisha ya watoto wetu tunaompelekea ili waweze kujifundisha kusoma, kupita mitihani na kuendelea. Hivi sasa, imekuwa tunampelekea watoto ili waweze kufa ndani ya madarasa. Hili ni jambo la kukemea zaidi. Bw. Spika, vile vile, ni muhimu Serikali ichukue hatua dhidi ya mwenye kumiliki shule hiyo; wale watu waliojenga, walioidhinisha ujenzi wa shule kama hiyo na ... view
  • 25 Sep 2019 in Senate: Kwa hivyo, tunasema kwamba watoto wetu ni muhimu katika nyumba zetu na katika maendeleo ya Taifa letu la Kenya. Kwa hivyo, ikiwa watoto wetu wataaachiliwa kiholela, itakuwa ni jambo la kusikitisha iwapo shule kama hizi zitaendelea kujengwa kila mahali katika nchi yetu. Hii inahatarisha maisha ya watoto wetu. Kwa hivyo, nikiunga mkono, inafaa hatua ichukuliwe ya kupitisha mjengo ambao utaruhusiwa, ili watoto wetu waweze kuketi ndani ya madarasa tukijuwa kwamba wako salama salmin na wanaweze kusoma ili wawe viongozi wa siku za usoni. Asante. view
  • 24 Sep 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Kwanza, ningependa kujiunga na wenzangu waliongea hapo awali na kusema kwamba Mswada huu ni muhimu sana katika maisha yetu ya kaunti na taifa nzima. Katika Bunge la Kumi na Moja tulikuwa na Mswada huu ambao tuliufanyia marekebisho yaliyokuwa yanahitajika. Hata hivyo, kwa sababu ya wakati, hatukuweza kuukamilisha na uwe sheria. Tukizingatia zaidi, tunaona kwamba Mswada huu unaleta sura ambayo watu wa mashinani wataweza kuhusihwa kutambua watu ambao walifanya mambo ya kutambulika katika vitongoji vyao. Hii ndio sababu inaitwa County Hall of Fame. Ni ukumbi wa watu waliobobea ambao historia yao inatambulika na wale wanaoishi katika kaunti ... view
  • 24 Sep 2019 in Senate: Uzuri wa Mswada huu ni kwamba haujampa mtu mamlaka ya kuweka mtu katika view
  • 24 Sep 2019 in Senate: . Ukumbi huu wa watu waliobobea utakua mjadala wa kila mtu katika kaunti. Hakuna hata mtu mmoja atayekuwa na uwezo wa kumfuta jina la mtu fulani ambaye kamati mzima imemkubali. Itakuwa ni kamati na itakapopitisha, ndivyo vile viongozi wa kaunti ile watafuata. Bw. Naibu Spika, nasisitiza ya kwamba wanaofahamu historia ya Mijikenda ni watu wachache sana. Watu kama sisi tulikuwa na wazee wetu ambao walitueleza vile kulikuwa, lakini hawakuandika historia yetu. Hawakuchukua hiyo habari kutoka kwa mababu zao. Baba yangu angekuwa ameipata historia hiyo kutoka kwa babu yangu. Leo hii ingekuwa akitafakari na kusema: “Mjukuu wangu, kulikuwa hivi au vile.” ... view
  • 18 Sep 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Pia mimi nilikuwa katika hiyo harakati ambayo wakili ama kiongozi, Sen. Sen. Orengo, aliposema kwamba ingekuwa bora kusuluhisha jambo hili kuhusu wale ambao majina yao yameandikwa hapa, kwa heshima ya hili Bunge. Nimekuwa katika Bunge kuanzia mwaka wa 2013. Kwa hivyo ingekuwa heshima kubwa ikiwa hao ambao wako katika hii list, badala ya sisi kupoteza wakati mkubwa, wajiondoe wenyewe ili sisi tupate nafasi. Hata sasa hivi, tunaweza kuchaguana hapa ndani; wote wanatosha. view
  • 18 Sep 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, Katiba yetu inatuambia kwamba tutakapokuwa tunachaguguana, lazima tuangalie kila sehemu ya nchi hii, ili kuona kwamba watu wote wanapewa nafasi ya kufanya kazi kama hiyo. Lakini tukiangalia majina haya, hata kama Sen. Wetangula amesema kwamba walienda pamoja na Professor na wakaweza kuwashawishi wale wakubali, ingawa wengine walikataa na wengine walikubali. Lakini ikiwa swala kama hili linafanya jina lako linaanza kuharibika saa hii, na uko hapa ndani, basi afadhali ujiondoe. La mwisho, Bw. Naibu Spika, ikiwa wanachama wa Kamati hii hawataki kujiondoa, basi nafikiria nafasi iliyoko sasa ni kuchukua hatua ya sisi wenyewe kuwaondoa. view
  • 18 Sep 2019 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. view
  • 10 Sep 2019 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I did not hear. I was not paying attention, but I am sorry about it. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus