16 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Langu ni kukuunga mkono katika kuwakaribisha wanafunzi kutoka Kaunti ya ndugu yangu, Sen. Mwangi, ambaye ni Seneta mtendakazi. Vile vile, ningependa kuwaambia vijana kwamba Maseneta wote waliopo hapa walikuwa vijana kama wao. Walienda shule, wakafanya bidii na hatimaye wamejipata hapa kwa sababu ya kuchaguliwa na wananchi. Pia nyinyi pia mnaweza kuwa Maseneta kama sisi baada ya sisi kustaafu na muendelee kujenga taifa letu. Nawatakia kila la kheri wanafunzi kutoka Kaunti ya Nyandarua. Nafurahi pia kuona kwamba ndugu yangu amefurahishwa sana kwa kuja kwenu.
view
10 Jul 2019 in Senate:
Madam Temporary Speaker, I beg to second.
view
20 Jun 2019 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Nawashukuru waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Uganda kwa sababu hao ndio majirani wetu wa karibu sana.
view
20 Jun 2019 in Senate:
Nawapa wabunge wa Uganda kongole kwa kuja hapa kujifunza. Ingawa Maseneta wengine wanasema kwamba Wabunge hawa hawaelewi Kiswahili, naamini kwamba wengi wao wanaelewa Kiswahili. Nina imani kwamba watajifunza mambo mengi sana hata lugha ya Kiswahili. Ningependa kuwashawishi kwamba Kenya ina mahali kwingi ambapo wanaweza kutembea jioni jioni. Kiongozi wa wengi wa Seneti, Sen. Murkomen, anajua sana sehemu ninazozungumzia, kwa hivyo anaweza kuwatembeza jioni.
view
20 Jun 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, nawashawishi Wabunge wa Bunge la Uganda wachukuwe nafasi hiyo ili waone Kenya inaweza offer kitu gani.
view
20 Jun 2019 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda.
view
19 Jun 2019 in Senate:
Ahsante Bw. Spika. Hilo jambo ni la kusikitisha. Ninatoa pole kwa familia ya wale waliopoteza maisha yao. Ni aibu ya kwamba kitendo kama hiki kinatendeka kila siku.
view
19 Jun 2019 in Senate:
Bw. Spika, kuna kelele ambayo sielewi.
view
19 Jun 2019 in Senate:
Bw. Spika, kuna vitengo vya ujasusi ambavyo vinaweza kuchunguza na kutuambia jinsi ya kuepuka janga kama hilo. Vitengo hivyo viko ndani ya serikali na watu hao wanalipwa mshahara. Ningependelea ya kwamba taarifa ya Sen. Farhiya ichukuliwe kwa umuhimu zaidi ili tupatiwe majibu mwafaka.
view
19 Jun 2019 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view