24 Jul 2019 in Senate:
Yes, Madam Temporary Speaker. I am referring to the Party Leader of the Forum for the Restoration of Democracy–Kenya (FORD-Kenya) and our former Senate Minority Leader in the Senate, who is a very senior citizen. He is also one of the most distinguished and celebrated lawyers in this country; Sen. Wetangula, the Senator for Bungoma County.
view
24 Jul 2019 in Senate:
I am obliged, Madam Temporary Speaker.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Ningependa kutoa maneno yangu kuhusiana na hii taarifa ambayo imeletwa hapa na Sen. Faki. Waswahili wanasema kwamba, ukishangaa ya Musa, nenda feri kule Likoni ndio utaona maajabu. Bw. Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha katika historia ya nchi kuona Wizara nzima ambayo ina wasomi, wanaweza kufikiria kujenga makao makuu ya uvuvi, mahali kama Nairobi, South C, ilhali kuna kaunti tano za eneo la pwani ambazo ziko katika ufuo wa bahari na uvuvi wetu unaendelea huko.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Mhe. Cherargei, hawezi kuelewa misemo au methali yote ya watu wa Pwani. Kwa hivyo, mambo ya bahari ambayo kivukisho chake ni feri, pengine hicho Kiswahili kimempita na hakuelewa nilichomaanisha. Hata hivyo, ninamshukuru sana kwa kuongea Kiswahili sanifu.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, tunaona maajabu hivi sasa tunayahamisha makao makuu ya uvuvi kutoka pwani ambapo kuna bahari. Hakuna nchi yoyote katika ulimwengu ambayo imetenda kitendo kama hicho isipokuwa Kenya. Jambo la kusikitisha ni kwamba utaona watu ambao wamepewa nyadhifa kama hizo ndio wanafanya ufisadi wa hali ya juu zaidi. Ukitaka kunyanyasa watu wa Pwani, basi wewe chukua uvuvi uulete hapa Nairobi ambapo hakuna bahari wala Ziwa Victoria. Ndugu yangu Sen. Sakaja hawezi kuelewa kwa sababu anatoka Kaunti ya Nairobi Mjini. Lakini anajua ya kwamba hapa Kaunti ya Nairobi Mjini hakuna bahari wala ziwa kubwa kama Ziwa Victoria.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, tunapofikiria kujenga makao makuu ya uvuvi katika nchi hii, ni heri kufikiria maeneo ya pwani ambapo kuna bahari. Lakini utapaka kwamba mahali ambapo panatakiwa kutengenezwa huu mjengo, tayari kuna ofisi kuu ya fisheries. Kinachohitajika kuongezwa ni majengo zaidi ili watu wafaidike na shughuli za uvuvi.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika Wa Muda, nataka utafakari jambo hili. Wavuvi wanapata shida sana kusafiri kutoka Kaunti za Mombasa, Taita-Taveta, Kwale, Lamu na Tana River; kuja Kaunti ya Nairobi Mjini ambapo ndio makao makuu ya uvuvi. Vile vile watu wa Kaunti ya Kisumu kutoka upande za Nyanza wanalazimika kusafiri mpaka Nairobi Mjini kwa sababu ya uvuvi. Hiyo si haki. Ni haki ya watu wanaoishi katika zile kaunti tano za pwani wapewe nafasi yao ya kuwa na makao makuu ya uvuvi.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Hapo awali, ulitueleza kwamba kuna watoto kutoka Kajiado County ambao mpaka sasa wako pale juu. Nina kuunga mkono kwa kuwakaribisha kwa dhati. Ninawapa kongole walimu na watoto ambao wako katika madarasa ya chini kwa kuja katika Bunge la Seneti ili wasikie, watafakari na waoene Maseneta pamoja na Spika na vile tunafanya mambo yetu. Wao ni viongozi wa siku za usoni. Ninawapa changamoto ya kwamba hakuna lisilowezekana katika ndoto zao. Kama wanataka kuwa Maseneta siku moja, hiyo ndoto inawezekana. Kwa hivyo, wafanye bidii. Nimeketi katikati ya Maseneta wanaotoka katika kaunti za uchungaji. Shule hii ni moja wa ...
view