23 Jul 2019 in Senate:
Bw. Naibu Spika, amesema kwamba nimetumia neno ‘wachungaji’ ambalo hata ndani ya Bibilia linamaanisha mtu anayetafuta kondoo aliyepotea na kumleta nyumbani. Nimesema kwamba hawa ndugu zangu wanaishi katika sehemu ambapo wanafuga mifugo kama vile ndugu yangu Sen. (Dr.) Ali anafuga ngamia, hawa wanafuga ng'ombe ambao wanatupatia maziwa na bidhaa zingine. Ndio maana nilisema nimeketi katikati ya dadangu na kakangu ambao ni Maseneta wa nguvu kutoka maeneo ya Kajiado na Narok. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Bw. Naibu Spika, hawa hawakupata nafasi hii kwa urahisi. Walifanya bidii wakiwa watoto kama nyinyi katika sehemu za ufugaji. Kwa hivyo, nyinyi mnaweza kuwa kama wao.
view
18 Jul 2019 in Senate:
Asante sana, Bi Spika wa Muda. Najiunga na Hoja hii ambayo imeungwa mkono na wenzangu wote. Bubu ni mtu asiye na uwezo wa kuzungumza. Wakati unatesa bubu, itafika wakati bubu ataanza kububuja maneno ili aanze kuongea, unafaa kukimbia mbali sana. Tulikuwa tumenyamaza kwa muda mrefu sana, lakini sasa tunawaambia ndugu zetu kwamba hatunyamazi tena. Maseneta 52 walioandamana leo ni walinzi wa serikali za kaunti. Tulienda kortini leo kudai haki ya serikali za kaunti. Nia yetu ni kuona kwamba serikali za kaunti zimepata fedha zao na wanaweza kutekeleza wajibu wao kwa wananchi. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono kwa dhati Hoja ...
view
17 Jul 2019 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
17 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, sisi sote hatufahamu lugha ya Kiswahili kwa ufasaha. Wewe ni mtu amabaye umekua ukiona maneno hayo yakitendeka hapa na umekua na roho ya kuweza kuwasikiliza. Mimi ningeomba, Sen. Were ni dada yangu, ana upungufu kidogo wa kuweza kujieleza kwa lugha hii. Kwa hivyo, mpatie nafasi aweze kujieleza katika lugha anayoifahamu sana.
view
17 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ningependa kuunga mkono taarifa hii. Tunaona ya kwamba watoto wakiwa wamekubaliwa kuingia shule za upili, hasa shule ambazo ni za hadhi ya juu, siku ya kwanza, wiki ya kwanza, mwezi wa kwanza au muhula wa kwanza, wanateswa na wenzao wa vidatu vingine. Wanaweza kuwafanya wenzao kuwa kama watumwa. Wakati mzazi anapopeleka mtoto wake shule, nia yake ni kwamba mtoto huyo aweze kujifunza na kupata masomo ambayo yatamfaidi siku zake za usoni. Lakini hii dhuluma inayoendelea katika shule zetu hakubaliki kamwe. Juzi tulisoma kwenye gazeti, jua ya Nairobi School ambapo wanafunzi wa kidatu cha kwanza walifanyiwa dhuluma kubwa ...
view
17 Jul 2019 in Senate:
Ahsante sana, Bw. Spika. Nampa kongole ndugu yangu, Sen. Orengo, kwa huo ufafanuzi. Katika hoja yangu ya nidhamu, nilikuwa nataka kusema mambo hayo hayo. Ninatoka katika eneo moja na Sen. (Dr.) Zani na ninamheshimu sana. Yeye ni msomi. Katika wale madaktari wanaotoka kule kwetu, yeye yuko katika ulingo wa hali ya juu sana---
view
17 Jul 2019 in Senate:
Leo amenoa kwa sababu amekuita “mzungumzishi”. Katika Bunge la Tanzania, Bwana Spika anaitwa Bwana Spika. Hajapewa jina lingine na Mheshimiwa Mbunge huwa anaitwa Mheshimiwa Mbunge wa eneo fulani. Hakuna jina kama “mzungumzishi” ama cheo cha “mzungumzishi”. Je, ni haki dadangu kuendelea kutumia jina “mzungumzishi”? Tunaomba aliondoe jina hilo jina atumie jina Bwana Spika.
view
17 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, asante. Kuna tafakari mbili hapa za Google. Google ile ya Sen. Malalah inasema wewe ni chatter Ile Google nyingine inasema ya kwamba wewe ni “mzungumzishi”. Hata hivyo, tunasema ya kwamba Google hizi zote mbili hazifai kwa sababu sio Kamusi ya Kiswahili. Google moja imetoa kwa maktaba na nyingine ya Sen. Malalah ninafikiria pengine ame-Google pande hiyo--- Maktaba imetoka upande za Pwani; hii ya Sen. Malalah ambapo Spika anaitwa chatter hatujui ni ya upande gani. Katika maoni yangu, hiyo amri uliyotoa kwanza---
view
17 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, mimi ninaongea hapa katika Bunge na ningependa unitegee masikio kwa sababu ukishatoa amri iwe ni sawa au si sawa, ni lazima amri yako itimie ndani ya Bunge hili. Hatusemi kwamba yale Seneta dada yangu alivyokuwa anasema au Sen. Malalah wana makosa. Lakini tunasema kwamba kwa sababu umetoa amri, hiyo amri yako itimie halafu kama kuna marekebisho ya aina yoyote, yaletwe kesho; sio leo baada ya Bw. Spika kutoa amri ya Bunge hili.
view