30 Jul 2019 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bw. Spika.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, wakati huu tunapoomboleza vifo vya viongozi wetu, singependa kumuingilia dada yangu, lakini umeyasikia matamshi yake hapo awali, kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Raila, hakufanya chochote kwa miaka 20 aliyowakilisha Kibira na kwamba huyu marehemu tunayeomboleza alifanya mengi kwa muda mfupi? Je ni sawa kwa yeye kusema maneno kama hayo? Standing Orders zetu hapa haziruhusu mheshimiwa kumkashifu mtu ambaye hayuko ndani ya Bunge hili.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu ambao unataka kufanya mageuzi katika sheria zetu zilizoko za ugonjwa wa saratani na vile tunaweza kujikinga ili tusipatikane na athari zake. Tangu tuingie hapa mwaka 2017, tumempoteza Seneta mmoja, ndugu yetu, Seneta wa Migori aliyeshikwa na ugonjwa wa saratani ya koo na kupoteza maisha yake. Ikiwa itawezekana, ni muhimu kusisitiza zaidi kwamba Serikali iweze kuchukua hatua na iweze kuweka kipaombele na uangaliwe sana kama janga la kitaifa. Watu wanaofariki kutokana na athari za ugonjwa wa saratani ni wengi sana. Si wa Bomet, Elgeyo Marakwet ama sehemu za Rift Valley tu, bali Wakenya ...
view
30 Jul 2019 in Senate:
pesa nyingi zilitumika. Vile vile ndugu yetu, Ken Okoth, alitumia pesa nyingi sana kujitibu. Lakini mwishowe haikuwezekana. Ni lazima liwe jukumu letu sote, kama Wakenya, kuangamiza ugonjwa huu wa saratani kwa kupitisha sheria hii ambayo italeta mageuzi mazuri, kwamba kila Mkenya aweze kufikia hospitali ili atibiwe ugonjwa huu wa saratani. Bw. Naibu Spika, mwisho naomba uniruhusu nitoe rambirambi zangu kwa familia na jamii ya Mbunge wa Kibra, ambaye alikua rafiki yangu. Urafiki wetu ulikuja baada ya kugeuziana kofia; kwa kuwa yangu ilikua inamtosha yeye, na yake ilikua inanitosha mimi. Tulikua katika zile harakati za siasa, lakini Mwenyezi Mungu ana sababu ...
view
25 Jul 2019 in Senate:
Asante Bw. Spika. Tangu nchi hii ipate uhuru mpaka sasa, hatuja wahi kuwa na aibu kubwa kama hili jambo la wakenya kula nyama iliyo dungwa dawa. Maduka ambayo yana patikana na hatia ya kuuza nyama mbovu ni lazima yafungwe mara moja. Veterinary inspectors wana takikana wafanye kazi yao vizuri. Tunajua ya kwamba kuna ufisadi mwingi unao endelea na hatutaki kusema ya kwamba hao ni wafisadi kwa sababu hakuna hatua ya kisheria ambayo ime chukuliwa lakini tuna sema ya kwamba huu upotevu ni wa kusikitisha. Daktari ambao wana chunguza nyama wasiwe wazembe katika kazi.
view
25 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, katika sheria zetu, mtu hana hatia mpaka apatikane na hatia. Hawa madaktari ambao wana chunguza hao wanyama ndio wako na hatia. Ni lazima hao madaktari wazingatie ya kwamba wakenya wana tumia chakula hiyo na wanaweza poteza maisha yao wakikula chakula mbaya.
view
24 Jul 2019 in Senate:
Shukrani sana, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Mimi ningependa kuunga mkono taarifa hii inayohusika na mbuga za wanyama wa porini. Mimi natoka katika maeneo ya wakulima. Wakulima wa Mkongani, Magharini na Ganze wanaathirika wakati ndovu, twiga na wanyama wengine wanapovamia mashamba na kuharibu mimea yao. Bw. Spika, hii ni taarifa muhimu sana kwa watu wanaoishi karibu na mbuga za wanyama. Hivi sasa kuna hatari ya wawindaji haramu kumaliza wanyama wetu. Idadi ya ndovu na twiga imepungua sana. Haya yote yanaletwa na tamaa ya wawindaji haramu ambao wanawaua wanyama wetu. Naunga mkono taarifa hii ili shirika la KWS lipewe nguvu zaidi ...
view
24 Jul 2019 in Senate:
Leo nilienda Lewa Marathon wanapofanyia itikadi ya kukimbia. Tulimpata simba mmoja ambaye hana mke. Hiyo yote imeletwa na uwindaji bandia. Tuliuliza na tukaambiwa ya kwamba simba huyo ni wakiume na anahangaika kutafuta mwenzake watakayeishi naye pamoja.
view
24 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, hili ni jambo la kusikitisha sana. Tunaangamiza sehemu moja ya tatu katika wanyama wetu. Kwa hivyo, ninasisitiza ya kwamba Shirika la KWS lichukue msimamo hususan wakumaliza wawindaji bandia. Ikiwa mtu hafanyi kazi kwa msitu au mbuga za wanyama, hana haki ya kwenda kule. Anaweza kwenda kama mtalii au apewa kibali cha kuingia kuangalia wanyama wetu na kufurahi kama wataliii halafu aondoke atuachie wanyama wetu vile walivyo. Lazima Serikali itilie mkazo jambo hili na kuwasaidia watu wanaofanya kazi katika Shirika la KWS.
view
24 Jul 2019 in Senate:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir.
view