Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1651 to 1660 of 2263.

  • 10 Apr 2019 in Senate: Bw. Spika wa muda, sijui kama umesikia alivyosema dadangu, Sen. (Dr.) Musuruve. Amesema ya kwamba ataendelea kuongea mambo ya walemavu mpaka mwisho wa hii Seneti. Ninauliza, ni haki yeye kutabiri mwisho fulani wa hii Seneti ama yalikuwa mazungumuzo aina gani? Anaweza kutueleza vizuri? view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda. Kwanza, naunga mkono Hotuba ya Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta aliyoitoa kwa Vyumba viwili vilivyokutana ndani ya Bunge la Kitaifa. Ninamshukuru Rais kwa kutoa Hotuba iliyogusa mambo mengi ambayo yana husika na wananchi ama ujenzi wa taifa. Kuna mengi ambayo Rais hakuguzia na ingekuwa vyema kama angeyaguzia. Jambo la kwanza na muhimu ni jukumu la Serikali kuona ya kwamba kazi kwa vijana imetekelezeka. Hii ni kwa sababu katika manyumba zetu vijana wengi wanaomaliza shule hawana kazi. Hakuna njia za aina yeyote ambazo Serikali imeanzisha ya kuona kwamba vijana hawa wamepata kazi. Bw. Spika wa Muda, hakuna ... view
  • 10 Apr 2019 in Senate: kazi, nyingi zao hazina wenye taluma yakuzitumia. Kwa hivyo, hawapati faida. Mashini hizi zimelala na serikali za kaunti zinalipa madeni lakini hazifanyi kazi. Rais katika Hotuba yake angeleta jinsi ya kutatua jambo hili lakini hakuleta. Hii imekuwa ni hasara tupu kwa serikali za kaunti. Sisi kama Maseneta tunazingatia umuhimu wa kuona ya kwamba serikali za kaunti zinafaidika na pesa ambazo tunapigania hapa. Ikiwa serikali za kaunti zitapata hizo pesa, ni makosa sana kwa Serikali Kuu kuzifuata ilhali mashini hazifanyi kazi na hazina faida yeyote katika hospitali za kaunti. Bw. Spika wa Muda, ningependa kuguzia hali mbovu iliyoko katika hopitali zetu. ... view
  • 10 Apr 2019 in Senate: ni muhimu ili tuvuke ile daraja na WaKenya waweze kupendana. Hili ni jambo muhimu katika nchi hii. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Tunakumbuka ya kwamba mwaka wa 2017, hatimaye tu baada ya kupiga kura, kama Wakenya tulilumbana sana. Tulileta shida kubwa sana kwa sababu hatukukubali na tuliamini ya kwamba kura zetu katika National Super Alliance (NASA) ziliibiwa. Hatukukubali kabisa kwamba Serikali iliyoko katika mamlaka ilikuwa Serikali kamilifu iliyochaguliwa na Wakenya. Matokeo au mavuno yake ilikuwa fujo katika barabara na biashara na hali ya uchumi katika Kenya ikaenda chini. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Kitu cha muhimu nataka kusisitiza ni kwamba Rais asirudi nyuma; asijaribu kurudi nyuma katika mambo haya ya kutengeza daraja ambayo Wakenya wataendelea kupendana. Pia, tunataka kumshukuru haswa Baba Raila Amolo Odinga, ambaye alijitolea mhanga, ijapokuwa alikuwa ameshinda lakini wakatangaza kwamba alishindwa. Mambo mengine yalitokea lakini, yali isha baadaye, yako nyuma yetu. Tuna angalia mbele, hatutaangalia nyuma. Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Sasa yale yanayojiri ni kwamba lazima Wakenya hivi sasa washikane mikono pamoja na waweze kwenda mbele. Inafaa tupendane na kuona ya kwamba dhana hii ya view
  • 10 Apr 2019 in Senate: imefaulu. Asante sana, Bw. Spika wa Muda. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 20 Mar 2019 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 20 Mar 2019 in Senate: Mr. Speaker, Sir, is the distinguished Senator for Machakos County, Sen. (Dr.) Kabaka, whom I respect so much in order to start canvassing this matter before it is even ventilated by the Joint Committee of Parliament? If he wants to air those views, my suggestion is that he table them before the Joint Committee of Parliament and not on the Floor of this House. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus