Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1661 to 1670 of 2263.

  • 20 Mar 2019 in Senate: Asante, Spika kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, daktari aliyefariki anatoka katika eneo la Pwani. Nikiwa mhusika, ningependa kutoa rambi rambi kwa familia iliyompoteza huyu daktari. view
  • 20 Mar 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 20 Mar 2019 in Senate: Bw. Spika, chama cha madaktari walikuwa wamekataa mkataba huu na kusema kwamba hawaukubali kabisa, lakini Serikali ikaonelea ni lazima iendelee nao. Hatimaye ikafaulu na ikaona ya kwamba lazima wale madaktari waje. Walikuja na wakakaribishwa kitajiri, kama vile wenzangu wamesema. Mtu akikataa na umlazimishe, basi Waswahili husema: “Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.” Hii ndio faida tunayoipata hivi sasa, kuona ya kwamba sisi kama wakenya tulikuwa wapumbavu, tukaingia katika mkataba ambao haufai na hatimaye, tumempoteza daktari mmoja. Wizara ya Afya inayoongozwa na Cecily Kariuki ndio iliwafanya wale madaktari waende kule. Je, Waziri huyu amesema nini mpaka leo kuhusu kifo cha ... view
  • 20 Mar 2019 in Senate: Mimi na ndugu yangu, Sen. Wambua, hatuwezi kulala kwenye chumba kimoja; hairihusiwi kiafrika. Itakuwaje madaktari, ambao ni watu waliohitimu na wameenda kufanya masomo ya juu, wanaishi katika hali ambayo si ya binadamu? Si kiafrika kwa wanaume watatu kulala kwenye room moja. Kama watu wa Cuba hufanya hivyo, hapa kwetu Kenya haiwezekani mimi na ndugu yangu, Sen. (Eng.) Hargura, kulala kwenye room moja. Kwa hiyo, tunasema, heshima, lazima ilegeshwe na heshima. Ikiwa mkataba huu hauna heshima, sioni faida Serikali ya Kenya iendelee kuwa na mkataba huu baina ya sisi na wenyeji wa Cuba. Wale madaktari walio kule Cuba, kabla hatujapoteza mtu ... view
  • 19 Mar 2019 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 19 Mar 2019 in Senate: Bw. Spika, kwanza nataka kumshukuru ndugu yangu, Seneta Khaniri, kwa Statement aliyoleta. Katika maeneo ninayotoka ya Kilifi na pwani kwa ujumla, kuna watu wa tabaka mbalimbali. Kwa hivyo, cheti cha kuzaliwa ni cha umuhimu sana. Jambo la kwanza ambalo ningependa kusema ni kwamba Serikali inafaa kuondoa ada ya vyeti vya kuzaliwa. Kupata cheti cha kuzaliwa inafaa kuwa ni haki ya kila Mkenya. Wakati mtu anapozaliwa, hakuna haja ya kuandika barua ya kuomba cheti cha kuzaliwa. view
  • 19 Mar 2019 in Senate: Utoaji wa vyeti vya kuzaliwa umekuwa chombo cha kutafuta pesa miongoni mwa wafanyakazi wa afisi zinazotoa huduma hiyo. Mara nyingi, utapata mtu anaitishwa “kitu kidogo” ili fomu yake ipitishwe. Hii ni tabia inayoendelezwa na maafisa wanaofanya kazi katika ofisi za kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa sababu ufisadi umekithiri na hiyo imekuwa biashara kubwa. Hali hiyo inaathiri jamaa zetu ambao, kama nilivyosema hapo awali, ni ndugu zetu wa dini ya Kiislamu. Wengi wa wale ninaowakilisha ni Waislamu. Hii ni kumaanisha kwamba si rahisi mtoto wa Kiislamu kupata cheti cha kuzaliwa ikilinganishwa na mtoto wa Kikristo. The electronic version of the Senate ... view
  • 19 Mar 2019 in Senate: Ni aibu kumtaka mtoto ambaye wazazi wake ni Wakenya alete cheti cha kuzaliwa cha babu yake. Kwa nini mtu atake cheti cha kuzaliwa cha nyanya yangu? Ni sawa ukitaka nikuletee cheti cha kuzaliwa cha mamangu na babangu, lakini sio vizuri kuanza kuulizwa aliyemzaa babu yako ni nani na anatoka wapi. Sisi sote sio wenyeji wa nchi ya Kenya. Historia inatuonyesha kwamba watu wengi walikuja wakakutana hapa, na sote sasa ni watu tunaoishi katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, ni makosa kwa serikali yetu kufanya biashara kwa kutumia cheti cha kuzaliwa. Ukienda kutafuta cheti, utaambiwa ulipe Kshs100 au Kshs200 na usipokuwa ... view
  • 19 Mar 2019 in Senate: Ndugu yangu anasema ya kwamba kunaitwa kichochoroni, lakini sio kichochoroni; ni kule mashambani. Itakuwa matusi kama mimi nitapewa cheti, na mtu mwingine ambaye amezaliwa huko hawezi kupewa kwa sababu ya dini yake. Itakuwa makosa kwa sababu Katiba yetu inasema ya kwamba usimbague mtu kwa sababu ya dini, rangi au mahali anapozaliwa. Ikiwa mtu huyo anatetewa na Katiba, sioni sababu ya wafanyikazi katika ofisi zile kuleta shida. Tulipokuwa na shambulizi katika DusitD2, Wakenya waliwatetea wale ambao walikuwa pale. Hatukubaguana kwa msingi wa ukristo ama uislamu; na hatukusema ya kwamba, “Huyu hana dini ama ni Muhindi.” Wakenya walijitokeza na kuhakikisha ya kwamba ... view
  • 19 Mar 2019 in Senate: Ahsante sana, Bw Naibu Spika. Naona huyo ambaye yuko na wewe anakunung’unizia. Kama hajui Kiswahili ama anakielewa lakini hawezi kutafakari vile inavyotakikana, asije hapo akakuambia ya kwamba, “Wakati wake huyu umekwisha.” view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus