19 Mar 2019 in Senate:
Bw Naibu Spika, nashukuru kwa muda ulionipa. Ndugu yangu Sen. Cheruiyot ni mdogo wangu, na ninampenda. Yeye ni Seneta wa Kericho, na pia anaangalia masilahi yetu hapa ndani ya Bunge kama kamishna.
view
19 Mar 2019 in Senate:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir.
view
19 Mar 2019 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kulenga na kuangalia juu ni maneno mawili tofauti. Sio haki kwa Seneta wa Kaunti ya Mombasa, ambaye ni ndugu yangu mdogo, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Mar 2019 in Senate:
kutumia neno ambalo sio sahihi. Sio haki kwake kusema maneno haya ni sawa mbele ya wanafunzi kutoka Kaunti ya Makueni, ambao Seneta wao yuko hapa, na amesifiwa kwa kuvaa vizuri. Haya maneno mawili ni tofauti kabaisa. Mfano hawa watoto wa Kaunti ya Makueni watakaouiga ni wa Sen. Mutula Kilonzo Jnr., Seneta wa Makueni.
view
19 Mar 2019 in Senate:
Shukrani Bi. Spika wa Muda. Ni jambo la aibu sana kwa nchi yetu ya Kenya na Serikali ya Kenya, kwamba, leo Mkenya anaweza kufa kwa sababu ya baa la njaa. Taifa la Israeli linaweza kuenda mahali popote katika ulimwengu kuona ya kwamba, yule mwnanchi wa Israeli ambaye anapata shida ya aina yeyote, mojawapo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Mar 2019 in Senate:
ikiwa ni chakula - na wao wanaishi katika jangwa huko Israeli - hakuna anayepoteza maisha. Ilhali sisi udongo wetu ni udongo ambao unaweza kuleta chakula na tukapata chakula kingi na hatuoni ni kwa sababu gani, ndani ya nchi yetu ya Kenya, kwamba Mkenya anaweza kupoteza maisha yake kule Turkana. Bi Naibu Spika wa Muda, hatuulizi ya kwamba sisi kama wakenya, hatubahatishi, ama hatuwezi kusema ya kwamba tuna bahati ya kuishi Kenya ama tunaomba tuishi Kenya, ili tufe. Hao hao mabwanyenye ambao wanafanya mambo ya ufisadi, ndio hao hao, hivi sasa wenye mabloki ya mafuta uko; sijui yanaitwa Ngamia block, wamerurumana ...
view
19 Mar 2019 in Senate:
Sawa nimekubali kukosolewa hapo.
view
19 Mar 2019 in Senate:
Bi Spika wa Muda, ni sawa makamu wa Rais ikiwa anafanya jambo kama hilo, ninampa kongole kwa kufanya hivyo, lakini hiyo imekuja muda baada ya watu wameshapata hasara ya maisha na wengine wamekufa. Angechukua hiyo hatua The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Mar 2019 in Senate:
hapo awali kuweza kutekeleza wajibu wa kuona ya kwamba maisha ya Mkenya hayatapotea. Vile vile, ninataka kusema ya kwamba, huu ukorofi wa mambo ya Galana Kulalu; tuliua Galana Kulalu ambapo sisi tuliweza kuweka pesa nyingi ndani yake kuona ya kwamba kila Mkenya---.
view
19 Mar 2019 in Senate:
Asante ndugu yangu Sen. Malalah kwa kuwa wakili wangu. Umenisaidia sana. Wafisadi walioshiliki katika mradi wa Galana-Kulanu ndio wamefanya Kilifi Kaunti iwe na njaa. Hao ndio wamepeleka ufisadi katika Kaunti za Turkana na Baringo na hatimaye watu wamepoteza maisha. Kwa hivyo, mimi namuunga mkono ndugu yangu, Sen. Wetangula, kwa kuleta taarifa kama hii Bungeni. Namshukuru sana.
view