13 Mar 2019 in Senate:
Ahsante, Bw. Spika. Sen. (Dr.) Ali ni ndugu yangu na rafiki yangu. Tusiweze kuwa na sintofahamu kwa sababu hivyo ndivyo anavyo ongea akiwa kule anakotoka. Sio hasira ama kutukana mtu. Hiyo amesema ni sawasawa kabisa.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bw. Spika. Hili ni Bunge ambalo tunaweka stakabadhi ya yote yanayosemwa hapa. Itakuwa hatari kubwa kwa mmoja wetu hapa kusema kwamba kuna mmoja wa magavana---.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Bw. Spika, yuko chama fulani ambacho amekitaja hapa; cha Jubilee, ambaye ameshindwa kutekeleza vile anavyotakikana kupeleka madawa katika hospitali. Hiyo hoja ni muhimu sana na itakuwa matusi kwa Wakenya ikiwa hatuwezi kuambiwa ni gavana yupi.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Ni nani huyo? Hilo ndilo swali tunalotaka kuuliza. Ni nani huyo? Atoboe hapa hapa.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Aseme hapa ili tupate kujua kinaga ubaga.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika kwa kunipa nafasi hii. Pia, nataka kuunga mkono taarifa ambayo imetolewa na Sen. Mutula Kilonzo Jnr.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Kwanza, natoa rambirambi kwa familia za watu wote ambao waliathiriwa na ajali hiyo ya ndege. Kuna Wakenya na watu wengine kutoka mataifa mbalimbali ambao walipoteza wapendwa wao katika ajali hiyo ya ndege.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Kadiri ya vile tunavyoelewa ni kwamba ndege za Boeing zimeweza kupigwa marufuku kutua katika viwanja vya maeneo ya Uropa. Hii ni kumaanisha ya kwamba kule wameona kuna sintofahamu kidogo katika ndege hizo. Bw. Spika, kwa hivyo ingekuwa muhimu sisi kama Wakenya ambao tulipata madhara makubwa--- Nafikiria katika ndege hii waliopoteza watu wengi zaidi ulimwenguni ilikuwa ni Wakenya. Hii ni kwasababu walikuwa wanatarajia kufika nyumbani salama salimini kuungana na wapendwa wao. Kwa sababu hiyo, ingekuwa muhimu sana kama nchi yetu pia ingechukua hatua hiyo kama ilivyochukuliwa na nchi za Ulaya ya kwamba ndege yenye muundo huo wa Boeing 737 Max 8 ...
view
13 Mar 2019 in Senate:
na wamerekebisha pale ambapo panafanya ndege hizi wakati zimepaa kupoteza mwelekeo, kuanguka na kuleta maafa haya. Mwisho ni kwamba kwa ababu tumepoteza Wakenya wengi, familia nyingi hivi sasa wanaomboleza. Kuna familia moja ambayo imepoteza watu watano katika ajali hiyo wakiwemo dada wawili na watoto wao wa kike watatu. Familia hizo sasa zitazika watu watano ambao ni wengi sana. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha. Ningependa sana ikiwa taifa letu la Kenya litatambua---
view
12 Mar 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kuniruhusu niongeze sauti yangu kuhusu taarifa ya ndugu yangu, Sen. Faki.
view