12 Mar 2019 in Senate:
Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba yule anayelinda mwenzake ndiye sasa anayetakikana kulindwa. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu Bunge la Kaunti linatakikana kuangalia matumizi, makadirio na kazi inavyoendelea katika serikali zetu za kaunti.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba sasa wale county executives wana mamlaka zaidi ya bunge lililoko katika serikali za mashinani. Tunawaambia kwamba tabia kama hizo hazifai kulingana na maadili yaliyomo ndani ya Katiba. Katiba yetu inatuambia kwamba bunge litakuwa na uwezo wa kuangalia kazi inayoendelea ndani ya serikali za kaunti.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Bw. Naibu Spika, ikiwa kuna kitendo kama hicho kinachoendelea vile ambavyo Sen. Faki amesema ingekuwa vizuri kikome kwa sababu wao kama executives hawana mamlaka ya kuweza kuwafuta kazi wale waliochaguliwa na wananchi katika serikali za kaunti. Kwa hivyo, lazima kuwe na uwiano mwema ndani ya serikali za Mashinani na wasifanye vitendo vya kupinga Katiba ya Kenya na uwezo wa zile bunge za mashinani.
view
12 Mar 2019 in Senate:
Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Spika, kutendanisha ni kama kumaanisha kwamba wakili, Sen. Wetangula hakielewi Kiswahili sawa sawa, ama alikuwa anamaanisha jambo gani?
view
19 Feb 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika Wa Muda, kwa nafasi hii nami nitoe maoni yangu. Kwanza, ninakubalina na ndugu zangu wote, Maseneta walionitangulia kuongea, akiwemo Sen. Mutula Kilonzo Jnr., Sen. Ochillo-Ayacko – ambaye sijui kama ametoka ama yuko kule nyuma – na vilevile, Sen. Cheruiyot.
view
19 Feb 2019 in Senate:
Kwanza mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati hii ya kuangalia hasa zaidi mambo ya wafanyikazi wa kaunti katika Bunge lililopita. Ukizingatia zaidi, utaona kwamba ni jambo la aibu hivi sasa tunapoongea. Ni aibu kubwa sana kwa Bunge la Seneti kujadili Mswada huu ambao haukuanzia hapa katika Bunge la Seneti. Ni kwa sababu haiwezekani kuwa tutakuwa na mambo yakiendelea katika serikali za mashinani hasa ikizingatia sana pesa za wafanyikazi ambao wamestaafu. Hicho ni kitu ambacho lazima kianzie hapa.
view
19 Feb 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, mimi mwenyewe nikiwa Mwenyekiti, nilianzisha Mswada huu hapa na tukaenda nao mpaka mwisho. Wakati ukatupata na kukawa na vikwazo vile ambavyo ndugu zangu wamesema, ya kwamba kunazo interests tofauti ama kunao watu wenye nafsi zao tofauti, na tulifika pale karibu na Mto Jordan halafu tukaona mamba wengi sana. Ikabidi sasa haiwezi kuvukika.
view
19 Feb 2019 in Senate:
Hayo yote ni kwa sababu kulikuwa na watafunaji ambao wako na nafsi zao za kibinafsi.
view
19 Feb 2019 in Senate:
Kitu muhimu katika Mswada huu ni sisi sote kama Wakenya na Maseneta ndani ya Bunge la Seneti, kuzingatia ya kwamba sisi tukilumbana au kushindana, watakaoumia ni wafanyikazi ndani ya serikali za mashinani katika kaunti. Lengo la Mswada huu ni kuona kwamba tumeweka pesa zao sawa sawa na kuwa kuna mikakati bora ya kuona The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view