19 Feb 2019 in Senate:
kwamba pesa za wafanyikazi zimewekwa mahali ambapo kila wafanyikazi wanapofanya kazi na ikifika wakati wa kustaafu, wanaona pesa zao ziko katika hali madhubuti na wanaweza kuzifikia, kuzitoa na kuzitumia. Jambo la kuaibisha zaidi ni kwamba, kumekuwa na majabali wawili wakipigana kuhusikana na mambo haya ya pesa za wafanyikazi za kustaafu. Na sijui ilikuwaje wakati huu ikaonekana kwamba Mswada huu ni lazima uanzie katika Bunge la Kitaifa. Jambo hili ni makosa makubwa. Niliweza kulisema jambo hili na kuliweka wazi katika Kamati yetu. Ninashukuru ndugu yangu Mwenyekiti yuko hapa. Nilipinga sana na nikasema si haki kwa Mswada huu kuanzia katika Bunge la ...
view
19 Feb 2019 in Senate:
Lakini kama tunavyoelewa, wakati ule kulikuwa bado hakuna handshake . Kwa hivo ilikuwa ‘wengi wape’. Na ikapita ikaendelea. Leo tunajadili Mswada huu ukiwa ulipitishwa na Bunge la Kitaifa kisha kuletwa hapa. Sisi ni kama ambao tumeambiwa ‘jadilieni yale yaliyoko sasa.’ Wafanyikazi katika kaunti zetu ni binadamu kama sisi. Wanaweza kucheleweshwa malipo yao ya kustaafu ama ya uzeeni. Utakuja kuona ya kwamba, wakati wa kustaafa, utashangaa kama mtu huyu alifanya kazi hapo awali ama hakufanya kazi kabisa, kwa sababu atakuwa amecharara na hali yake ya maisha ya baadaye yanakuwa mabaya sana. Watoto wake pengine hawataendelea na masomo kwa sababu ya ukosefu ...
view
19 Feb 2019 in Senate:
Hoja ya Nidhamu, Bi. Spika wa Muda.
view
19 Feb 2019 in Senate:
. Asante Bi. Spika wa Muda. Nina Hoja ya nidhamu. Je itakuwa sawa kwa Mwenyekiti kuweza kufafanua kwa kutumia lugha inayoeleweka anaposema kwamba haina haja ya Sen. Halake kuuliza ni kwa nini huu Mswada ulianza katika Bunge la Kitaifa na kuja Bunge la Seneti na tukaukubali? Hilo ni swala ambalo ni sharti bwana Mwenyekiti alijibu sasa hivi au katika mchango kwa huu Mswada. Je ni haki kwetu kujadiliana Mswada huu ambao hatukuuanza? Tunataka kujua ni kwa sababu gani.
view
19 Feb 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Kuna jambo moja tu ambalo nilikuwa nataka kujua: Ikiwa kuna Mswada ambao tunaujadili kutoka katika Bunge la Kitaifa; na vile vile Kamati yetu ya Seneti imetengeneza Mswada kama huo, nataka kumwuuliza ndugu yangu, Mwenyekiti, ambaye anasema kwamba ni sharti ule Mswada wake utakuja kujadiliwa, kwamba, Kiongozi wa walio Wengi ndani ya Bunge la Seneti hatoweza kukubali kabisa ikiwa yeye ndiye aliyeleta Mswada huu hapa.
view
19 Feb 2019 in Senate:
Hivi leo, Mwenyekiti wangu anatuambia kwamba atakuwa na uwezo wa kuleta Mswada huo huo; maneno ni hayo hayo, sheria ni hiyo hiyo, na kila kitu ni hicho hicho. Hatutamkubalia Kiongozi wa Wengi wa Seneti, Sen. Murkomen, hapa ndani ya Bunge hili la Seneti. Huo ndio ukweli wa mambo.
view
19 Feb 2019 in Senate:
Kwa hivyo, tusifichane kilugha hapa; tuambiane wazi wazi iwapo Mswada alio nao ataendelea nao, ama atauwacha. Halafu tuangalie tutashika lipi na tuache lipi kuliko kuleta mkanganyiko. Hivi sasa, kuna Mswada unaozungumziwa katika Bunge la Kitaifa, na pia kuna mwingine unaozungumziwa hapa katika Bunge la Seneti, na hiyo sio sawa. Iwapo tutafanya hivyo, lazima tuzingatie kwamba ndovu wakipigana, nyasi ndizo huumia. Hapa tunaendelea kupigana sijui ni Bunge la Kitaifa, na Bunge la Seneti; tunagombana kwa sababu ya pesa za wafanyakazi. Wanaoumia hapa ni wafanyikazi. Hatukuletwa hapa kuonea wafanyakazi; tuliletwa hapa kuwasaidia wafanyikazi na sheria. Hii sio haki! The electronic version of ...
view
19 Feb 2019 in Senate:
Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, lazima Mwenyekiti afafanue kinaga ubaga.
view
14 Feb 2019 in Senate:
Madam Temporary Chairperson, I beg to second.
view
14 Feb 2019 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view