Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1931 to 1940 of 1944.

  • 22 Oct 2013 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii iliyoletwa na Sen. Elachi. Jambo la kwanza ambalo ningependelea kuunga mkono ni kwa sababu ni haki ya mfanyikazi kuona ya kwamba wakati wa ugatuzi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 15 Oct 2013 in Senate: Hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Spika. Je, ni haki kwa ndugu yangu, Sen. (Dr.) Machage, kutumia neno “hasara” badala ya jina Sarah? Tunajua neno “hasara” linamaanisha jambo mbaya. Je, ni jina lipi lilo sawa ni Bi Sarah au hasara? view
  • 15 Oct 2013 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, nataka kumpongeza dada yangu, Sen. Elachi, kwa kuleta Hoja hii. Kitu ambacho nataka kufafanua zaidi ni upande wa Katiba. Mimi kama mwanasheria, nahisi kuwa kuna umuhimu wa kuthibitisha sheria za Katiba. Kulingana na Kipengele cha 96, kinasema kuwa jukumu letu si kuwakilisha peke yake, bali ni kulinda na kutetea rasilmali za kaunti na serikali zake. Hiyo, kisheria, haina haja ya kufafanua zaidi. Kazi ya Seneti hapa ni kulinda na kutetea serikali za kaunti. Kwa hivyo, ni makosa kuona ya kwamba shirika linaloangalia suala la mishahara ya wafanyikazi wa Serikali halizingatii ... view
  • 15 Oct 2013 in Senate: wakati wa mama huyu kujificha kama mbuni umekwisha. Kunao umuhimu wake kukaa na kufahamu ya kwamba ikiwa yeye anapata mshahara wa mamilioni, basi kunao waheshimiwa katika bunge za kaunti ambao wanapata mshahara wa Ksh79,000 kwa mwezi; na kunao umuhimu kuona ya kwamba zile pesa wanazopata zimeongezwa. Tunajua kabisa kuwa sheria za leba za wafanyikazi zinazosema ya kwamba mfanyikazi anayelipwa vizuri huwa pia anayo bidii ya kufanya kazi. Lakini mfanyakazi ambaye humlipi vizuri hana budi kukuibia wewe mwenyewe kama tajiri. Tunaanza mfumo ambao ni wa kusikitisha kwa sababu ikiwa hawa tumewapatia jukumu kama waheshimiwa katika bunge za kaunti, na mapato yao ... view
  • 18 Sep 2013 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza, ningependa kumpongeza wakili Seneta Mutula Kilonzo Junior kwa ushindi wake katika uchaguzi mdogo. Ushindi wake ulikuwa wa kukamilika na kuthibitisha ya kwamba ni wakili na mtetezi ambaye watu wa Kaunti ya Makueni walikuwa wamejitolea kumpa nafasi ili aweze kuwahudumia. Bw. Spika, namfahamu Sen. Mutula Kilonzo Junior kama wakili mwenzangu ijapokuwa nimepita viwango kadha nikwa jaji na hatimaye kuweza kustaafu. Kama wakili, kuna nyakati amekuwa mbele yangu nikiwa jaji na nimeona kwamba amekamilika kiwakili. view
  • 18 Sep 2013 in Senate: Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kumpongeza Sen. (Prof.) Lonyangapuo kwa Hoja hii. Mtu anayeitwa KPR ni askari ambaye amepewa kifaa cha kujitetea, kulinda amani na kuweza kuona ya kwamba watu wanaishi kwa amani. Lakini tunajiuliza ni kwa sababu gani watu hawa wanaopewa vifaa kama hivi hawalipwi mishahara. Ni mpango gani Serikali iko nayo kuona ya kwamba watu hawa wamelipwa mishahara? Kutolipwa mishahara inamaanisha kwamba watu hawa wanafanya kazi bure ilhali hii si kazi ya kanisa, bali ni kazi ya kulinda amani. Amani haiwezi kupatikana kule pwani ikiwa mashamba ya watu wa pwani yamechukuliwa na ... view
  • 24 Jul 2013 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, is it in order for my colleague to refer to the Temporary Speaker as “Mr. Chairman?” view
  • 23 Jul 2013 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Nataka kuunga mkono Mswada huu wa ugawanyaji pesa. Kama tunavyoelewa, kulingana na kipengele cha 96 cha Katiba, sisi kama Seneti kazi yetu ni kulinda na kutetea rasilmali za zile kaunti tunazotoka. Ya pili ni kuhakikisha kwamba ugawanyaji wa pesa zitakazotoka katika Serikali kuu zimefika mashinani na zimefanya kazi inayohitajika kufanyika huko. Wakati ule Mswada wa pesa ulipokuja hapa, tuliona kwamba pesa zile zilikuwa hazitoshi, ndio sababu tukasema ziongezwe kutoka Ksh210 bilioni hadi Ksh258 bilioni. Lakini kwa ukosefu wa nidhamu ama kutozingatia masilahi ya serikali za kaunti, zile pesa zilipunguzwa ama zilibaki pale ... view
  • 23 Jul 2013 in Senate: Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, nataka kuunga mkono na kusema kwamba Mswada huu ni mzuri na utaweza kuleta maendeleo, hasa tukihakikisha kwamba wale magavana ambao wako katika utawala wa serikali za kaunti wasitusiwe. Tumeona hivi majuzi kwamba wanaitwa sijui “maraisi.” Ukiitwa “his Excellency,” wewe sio raisi; unaitwa “ his Excellency the Governor ;” haukuitwa “ his Excellency the President .” Lakini tukiangalia watu wengine – kwa sababu wanajaribu kuharibu majina ya hawa watu walio pale – wanaanza kutumia lugha isiyofaa. Mimi nasema ya kwamba magavana wetu wanafanya kazi nzuri, na kulingana na utawala wao mpaka sasa, naona ya kwamba wanafanya ... view
  • 11 Jul 2013 in Senate: Bi. Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasi hii. Pia mimi ningependa kujumuika na Maseneta wenzangu na Wakenya wengine kuomboleza vifo vya wanafunzi vilivyotokea kule Kisii. Hawa ni baadhi ya wanafunzi ambao wamechaguliwa na wana akili sana. Kama tunavyojua, ukisomesha mwanafunzi umesomesha taifa nzima. Maisha yao yamekatizwa kwa wakati ambao haujafika. Mimi, familia yangu na watu wote wa Kilifi County ningependa kuwapatia pole sana wazazi wa watoto hawa, familia na jamii zote za watu wa Kisii haswa nikizingatia sana Gavana ambaye ni rafiki yangu, Gavana Ongwae. Ninajua ana wakati mgumu sana wakati huu. Pia ningependa kumwambia kwamba aweke juhudi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus