11 Jul 2013 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, asante sana kwa kunipa nafasi hii. Pia mimi ningependa kujumuika na Maseneta wenzangu na Wakenya wengine kuomboleza vifo vya wanafunzi vilivyotokea kule Kisii. Hawa ni baadhi ya wanafunzi ambao wamechaguliwa na wana akili sana. Kama tunavyojua, ukisomesha mwanafunzi umesomesha taifa nzima. Maisha yao yamekatizwa kwa wakati ambao haujafika. Mimi, familia yangu na watu wote wa Kilifi County ningependa kuwapatia pole sana wazazi wa watoto hawa, familia na jamii zote za watu wa Kisii haswa nikizingatia sana Gavana ambaye ni rafiki yangu, Gavana Ongwae. Ninajua ana wakati mgumu sana wakati huu. Pia ningependa kumwambia kwamba aweke juhudi ...
view
3 Jul 2013 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi nichangia Hoja hii. Pia ningetaka kuchukua nafasi hii kumshukuru Sen. Obure kwa kuleta Hoja hii inayowahusu wafanyakazi. Kama sote tunavyojua, mfanyakazi ni mtu muhimu sana katika uendelezaji wa uchumi wa nchi yetu. Lakini ni jambo la kusikitisha tukiona kwamba baada ya mfanyakazi kustaafu anapatikana barabarani, ofisini na nyumbani za marafiki akiomba omba ili apate namna ya kuweza kujikimu kimaisha. Ningetaka kuhimiza mapato ambayo yanapewa na mahakama yalipwe mara moja kwa sababu ni haki ya mfanyikazi. Mfanyakazi aliyefanya kazi au kwa bahati mbaya amepoteza kazi yake, ni sharti alipwe ikiwa mahakama imeamua ...
view
3 Jul 2013 in Senate:
On a point of information, Madam Temporary Speaker. His Excellency the President referred to children joining class one and not those that are one year old.
view
24 Apr 2013 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuwashukuru watu wa Kilifi Kaunti kwa kunichagua kama Seneta wao wa kwanza. La pili, pia vile vile ningependa kukupongeza kwa kuchaguliwa kama Spika wa Seneti. Pia, ningependa kuwapongeza Maseneta wenzangu kwa kuchaguliwa kuwa Maseneta. Katika Hotuba ya Rais, alizungumzia kuhusu kutofautiana kwa maoni na kuheshimiana. Ningependa kuongea juu ya mambo ya utalii. Ile Kaunti ambayo ninawakilisha hapa Seneti ina hoteli nyingi kuanzia Mtwapa mpaka Tana River. Hoteli hizo hutembelewa na watalii wanaotoka katika sehemu nyingi sana za nchi za ng’ambo. Watalii wanaokuja katika nchi yetu, baadhi ya wale wanaotembelea mbuga za ...
view