Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 321 to 330 of 2266.

  • 3 Oct 2023 in Senate: Bw. Spika, katika malalamishi haya, ninazingatia ya kwamba hawa wamekuwa wakizaana. Nambari yao imeongezeka. Hili shamba lililoko hapa Pumwani ni haki yao kupewa. Hivi sasa tunaona hiyo shamba imeanza kugeuzwa. Wale matajiri wamefika hapo sasa. Mipangilio imefanywa na imepelekwa katika hii Serikali ya Kaunti ya Jiji la Nairobi. Wametolewa katika ile ardhi yao waliokuwa wakiishi pale na wanafurushwa watu wengine wanapewa. Sisi tunasema ya kwamba malalamishi haya yalioletwa ni ya muhimu sana. Ile Kamati ambayo itahusika na kuangalia hii ardhilhali iangalie kwa uangalifu sana kuona kwamba wale watu wa Pumwani wamepewa haki yao kama Wakenya wanaoishi katika nchi hii na ... view
  • 3 Oct 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, Kamati hii inayochunguza maafa yaliyotokea na miili kupatikana inayopita 95 na Zaidi; hivi sasa idadi ni zaidi ya 500. Tukizingatia kwamba watu walipoteza maisha yao, ingekuwa vyema tupate ripoti nzuri. Ripoti hii inaweza patikana kulingana na muda ambao wanakamati wanahitaji, ikiwa wameomba muda uongezwe, ili waweze kukamilisha na kuwaambia Wakenya yaliyojili kulingana na ule uchunguzi waliofanya, basi litakuwa jambo nzuri kuongeza. Hili ni jambo la kusikitisha. Watu wa Kilifi wanasikitika na wana majonzi mengi kwa sababu ni kwenye ardhi yao ambapo kila uchao watu wanafukua miili. Hata ikiwa hatuhusiani kidamu, hawa ni Wakenya kama ... view
  • 26 Sep 2023 in National Assembly: Asante Bw. Spika. Najiunga na wewe kwa kuwashukuru ndugu zetu waheshimiwa wakiongozwa na gavana Jeremiah kwa ukarimu na makaribisho yao hapa Turkana. Nimejionea mwenyewe wakati nilipofika kwa mara ya kwanza. Kaunti zote ambazo tumeweza kwenda kwa shughuli ya Seneti Mashinani, kama kungekuwa na kupeeana zawadi ya ushindi basi, tungepea Kaunti ya Turkana. Makaribisho ya watu wa Turkana ni hali ya juu sana. Tumeyapendelea na kuyakubali. Pia tumeweza kucheza ngoma za kinyumbani za hapa Turkana na tumefurahia sana. Asante sana Bw. gavana, Waheshimiwa wenzetu na ndugu zetu wengine wote walioshiriki katika makaribisho hayo. Vile vile, ninatoa shukrani kwa ukarimu wenu na ... view
  • 21 Sep 2023 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 21 Sep 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ninataka kuuliza swali moja. Je, ni haki yeye kiongozi wake wa waliowengi wachache--- kama mmoja wa wanaotakiwa kuongea kuhusiana na “mchele”, unaofanya wengine kuzimia. Ni haki? view
  • 21 Sep 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Tabia ya kuwekewa ‘mchele’ katika vilabu vya kimataifa au vya kawaida, iko. Watu wamepoteza maisha yao na wengine kuugua na hatimaye kufariki. Tunajua kuwa watu wanapoenda katika vilabu vya burudani, huwa hawana uangalifu maalumu wakati wamelewa. Ni kweli kabisa. Ninamuunga mkono kwa dhati dada yangu, Sen. Okenyuri, kwamba ni muhimu kuwe na uangalifu zaidi. Vile vile, tusisitize na tulete sheria ambazo zitawezesha kuwachunguza wauzaji wa madawa katika vituo vya afya. Siku hizi kuna mchezo ambapo mtu anaingia tu katika duka la kuuza dawa na prescription kutoka kwa Dr. Boni Khalwale, halafu unauziwa dawa. ... view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Asante Bw. Spika. Ninajiunga na wewe kuwakaribisha waheshimiwa kutoka Bunge la Uganda. Tumekuwa nao katika mkutano hivi leo na tumeweza kugeuziana mahusiano ya hizi nchi mbili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Ni jambo nzuri kwamba wamekuja hapa kuona vile tunavyofanya kazi na pia kujijulisha mambo fulani fulani ambayo wanaona tofauti kati ya sisi na wao katika Bunge lao. Tumeona mambo mengi yamefanana. Hata hivyo, kusema ukweli ni kwamba hawa wabunge wa Bunge la Uganda wametushindia kitu kimoja. Kiranja wao akiandika barua ya kwamba katika kamati hii nimetoa huyu na kuweka yule, Spika huwa hana njia yoyote ya kufanya isipokuwa kusema kuwa hiyo imekubaliwa. view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Asante Bw. Spika. Mimi nina imani ya kwamba ndugu zetu kutoka Uganda wamekuja hapa na wamefurahi kuona vile tunavyoendelea kufanya kazi. Wako hapa kwa siku mbili au tatu na wataendelea kujifunza na kuona. Ndugu zangu Maseneta, ninaomba tuweze kuhusiana nao ili tuwe na uhusiano mwema baina ya nchi yetu hii na nchi ya Uganda. Uhusiano pia uendelee kama vile Sen. Mundigi husema ya kwamba yeye katika hizo harakati, amefaulu sana. Asante. view
  • 19 Sep 2023 in Senate: Thank you, Mr. Speaker. Sir. I second. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus