19 Sep 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, ndugu yangu Sen. Faki amesema kuwa “aliingia collabo na mtu mwingine”. Je, hili ni neno ambalo tunalitumia hapa Bungeni? Kama sivyo, basi aliondoe, alifutilie mbali na kutumia neno linalo kubalika.
view
19 Sep 2023 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, natoa rambirambi zangu kwa wale wote waliopoteza maisha yao wakati wakifanya kazi ya kulinda nchi na kuangalia hali ya vile mipaka yetu inavyoendelea hapo juzi na jana na wakapatikana na hasara na kupoteza maisha yao katika ajali ya ndege. Pili, ninawapatia kongole wale maafisa wetu wa jeshi kwa kazi ngumu wanayoifanya. Ijapokuwa wanapitia mitihani mengi, wanaweza kuketi pale na kuona kwamba wameweza kutetea nchi yetu. Hususan pale sehemu za Kaunti ya Lamu. Kaunti ya Lamu ni mahali ambapo jamii zote za Kenya zinaishi. Panatakikawa kuangaliwa vizuri kwa sababu ni pahali ...
view
19 Sep 2023 in Senate:
Badala ya kutetea watu katika maeneo kama yale, sasa hivi Serikali inagongana wenyewe kwa wenyewe. Mawaziri wanaongea tofauti. Pia, yule Economic Advisor naye anaongea vile. Sasa unashindwa, je, watachukuwa wakati gani kuangalia zile sehemu zinaendelea namna gani kwa usalama. Wakiwa kitu kimoja, wataona ya kwamba maisha ya watu wa Lamu yameweza kutetewa vilivyo. Hivi sasa, tuko katika hali ya kupigana na hali ya uchumi. Kule kwingine watu wanakufa. Watu hawana chakula na inafaa wapelekewe chakula katika maeneo ambayo yako na shida zaidi kama vile Lamu. Ni sehemu ambayo iko n a shida nyingi na inatakiwa msaada upelekwe kule. Lakini, hivi ...
view
31 Aug 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Kitu cha kwanza ni, naunga mkono Mswada huu wa mabadiliko ya hali ya hewa, au kwa Kiswahili sanifu, mabadiliko ya tabianchi. Kwa mara ya kwanza nimejipata nikiona tabianchi au climate change kwa Kamusi lakini, hali ya hewa ni mojawapo. Bw. Spika, cha muhimu ni kuona ya kwamba tumezingatia swali hili katika nchi yetu. Hii tabia ya nchi inaweza kuangaliwa vizuri ikiwa sisi sote tutajumuika kama Wakenya na kuona tumepanda miti ambayo itaweza kulinda mazingira. Ninatoka sehemu za Kaunti ya Kilifi. Mara nyingi ukienda pande za ufuoni wa bahari, utapata sio kukata miti pekee yake katika ardhi lakini ...
view
31 Aug 2023 in Senate:
Tukiwa katika mazungumzo hayo wiki ijayo, ni muhimu kuonyesha ya kwamba Kenya iko katika kipao mbele. La muhimu katika hii mabadiliko ya tabia ya nchi ni kwamba sisi pia lazima tuone baada ya kupanda hii miti, tutailinda. Huwezi kupanda miti pekee yake bila kuilinda. Tuko na makabila mengi kama alivyotaja ndugu yangu. Kule ninakotoka, kuna kabila la Warta. Hilo ni kabila ambalo limeishi na linalinda misitu. Watu kama hawa ni lazima ikiwa kutatoka pesa zozote, wapewe nafasi hiyo. Bw. Spika, nikimalizia, dakika moja tu. Kunao umuhimu kuona ya kwamba watu wanaoishi katika hiyo miti ndio watapewa---
view
29 Aug 2023 in Senate:
Bw. Spika, kwanza ninaunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Kiongozi wa Walio Wengi. Katiba inatueleza kabisa kuwa mamlaka yote ya taifa hili yako katika mikono ya Wakenya. Kwa hivyo wao ndio wenye mamlaka. Sisi tuko hapa kama Bunge kutekeleza yote ambayo Wakenya wanahitaji yatekelezwe katika Bunge hili la Seneti. Mengi yamesemwa. Hata hivyo, Kipengele cha 94 cha Katiba kinasema wazi kwamba Wakenya watawakilishwa Bungeni na wale waliochagua. Tukiwa hapa, tunayo majukumu tofauti. Jukumu letu la kwanza ni kuona---
view
29 Aug 2023 in Senate:
Bw. Spika ningependa kusikizwa lakini kuna sauti nyingi zinazotoka upande huo mwingine.
view