Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 341 to 350 of 2266.

  • 29 Aug 2023 in Senate: Bw. Spika, tunajua kuna mazungumzo yanayoendelea. Ni lazima yapitishwe katika hili Bunge. Ni muhimu hayo mazungumzo yafaulu ili amani ipatikane nchini. Kulingana na pande zote mbili; Upande wa Walio Wengi na wa Walio Wachache, tunajua wananchi wasio Wabunge walichaguliwa ili wasaidie ile timu ya Bunge. Timu ambayo tulichagua hapa inaongozwa na Wabunge wetu kutoka pande zote mbili. Hawa Wabunge wako na ujuzi na taaluma ya hali ya juu ya kuendesha mazungumzo haya. Vile vile, kuna technical experts ambao wanasaidia hilo kundi. Wao pia wako na taaluma ya juu. Jambo tunalohitaji katika nchi hii ni amani. Bila amani hakuna nchi inayoweza ... view
  • 29 Aug 2023 in Senate: Bw. Spika, nia yetu ni kwamba mazungumzo haya yaweze kufaulu. Tuna imani na timu ambazo tumeziweka hapa mbele. Bibilia inatuambia ya kwamba, pale watu wawili au watatu wako pamoja kuzungumza, ni lazima pawe na amani. Kwa hivyo, sisi tuko na imani na mazungumzo haya na vinara wote kutoka upande huu na ule tuliowachagua. Kuna Viongozi wa Walio Wengi wakiongozwa na mhe. Ichung’wa, na Viongozi wa Walio Wachache wakiongozwa na Mhe. Kalonzo Musyoka. Kwa hivyo, mazungumzo haya yataleta matunda na hatimaye Kenya itaendelea mbele na kupata faida kubwa. Bw. Spika, naunga mkono Mswada huu ili uweze kufaulu. Asante sana. view
  • 29 Aug 2023 in Senate: Mheshimiwa Spika, ule mjadala uko hapa ni wa muhimu sana na wa kitaifa. Lakini, ni sawa yale matamshi aliyoongea dadangu, Sen. Nyamu, ya kwamba hapa tunaongea juu ya Baba Raila Amolo Odinga? Ningetaka kujua kutoka kwake. Kama si sawa, anaweza kuondoa maneno hayo na akaomba msamaha? view
  • 29 Aug 2023 in Senate: Asante Bw. Spika. Nasikitika kwa view
  • 10 Aug 2023 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, I have been in this House long enough. This is the first time we are coming across such a challenge. It requires wisdom to keep the dignity of this House, and we should not expose it by washing not so good linen in public. I second what the Senate Majority Leader has stated. It will go a long way to sort out a number of issues. view
  • 9 Aug 2023 in Senate: Asante sana Bw. Naibu Spika. Jambo la kwanza, nataka kumpatia kongole dada yangu Sen. Okenyuri kwa Taarifa hii ambayo ameleta hapa. Utalii ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii. Asilimia 30 ya mapato ya uchumi wa nchi hii, ni pesa ambayo inaletwa na watalii. Kwanza, inaleta ajira. Vijana wengi wamepata ajira kupitia mambo ya utalii. Lakini ukiangalia hivi sasa katika sehemu nyingi huku Kenya, vijana wanakosa ajira kwa sababu utalii umekufa--- view
  • 9 Aug 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 9 Aug 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Wakati mwingine ni vigumu sisi sote kuelewa Kiswahili. Hata mimi pia bado ninajifunza Kiswahili. Sikusema “azilimia” bali nilisema “asilimia.” Kwa hivyo, nadhani amenielewa. Kitu ambacho nilikuwa nataka kusema ni kwamba, vijana walikuwa wakipata ajira hapo zamani. Lakini hivi sasa, ukiangalia hali ya uchumi na utalii katika nchii hii, haswa tukizingatia sehemu zote za pwani, utapata kwamba hoteli zimefungwa na vijana wamerudi nyumbani. Kile ambacho nasema ni kwamba, inatakikana kuwe na mikakati bora, kulingana na Taarifa iliyoletwa na Sen. Okenyuri, ili utalii uweze kurudi. Katika Kenya, tulikuwa na Utalii College na colleges zingine ndogo ambazo zimekuwa zikizingatia ... view
  • 9 Aug 2023 in Senate: Asante sana. Tunajua Lamu hupata watalii wengi. Kuna ile airport ambayo hata sisi tukiwa na mikutano Lamu, huwa tunapanda ndege na kushuka huko. Hiyo ni Manda Airport ambayo mpaka sasa ni kidogo sana. Tunasema kwamba Serikali ni lazima izingatie ya kwamba pale panaposhuka watalii pafanyiwe utaratibu. view
  • 9 Aug 2023 in Senate: ya Manda Airport pia sio nzuri ilhali hapo ndipo sisi hutua tukienda Lamu. Itakuwa vyema ikiwa Serikali itaongeza upana ili watu wakishuka pale waone kwamba iko sawa. Asante. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus