Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 351 to 360 of 2266.

  • 9 Aug 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Kwanza, ninaipa kongole Kamati yetu ambayo inajihusisha katika mambo ya mkasa wa bomu wa mwaka 1998 katika Ubalozi wa Amerika. Wakenya wengi waliathirika na majeraha na wengine kufa. Juzi nikitizama runinga, niliona mtu ambaye wakati huo alikuwa miezi saba tu tumboni mwa mama yake. Mama yake aliathirika katika huo mkasa wa bomu. Watu wengi walipata majeraha. Lakini wafanyakazi wa lile jumba la Amerika, kwa sababu ya sheria zao na mienendo yao ya kibinadamu, ilibainika wazi ya kwamba wale walioathirika na wale waliopata majeraha makubwa, walilifidiwa. Walifaidika ijapokuwa walipoteza watu wao na wengine kupata majeraha. Ile bomu ... view
  • 9 Aug 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 9 Aug 2023 in Senate: Jambo la kusisitiza zaidi ni kwamba hawa Wakenya wetu ni binadamu pia. Hebu fikiria mtoto kuathirika akiwa tumboni mwa mama yake na anasema hadi wa leo anahisi kisunzi na macho yake hayaoni vizuri. Ni kwa sababu ya athari iliyotokea wakati ule. view
  • 9 Aug 2023 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika. Sijui kama hiyo Hoja ya nidhamu--- view
  • 9 Aug 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika, nilidhani umempa Sen. (Dr.) Khalwale nafasi kwa sababu alikuwa tayari na hoja ya nidhamu. view
  • 9 Aug 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika, Kamati hii iwe na ushirikiano mwema na utendakazi mzuri. Serikali ya Amerika nayo iangalie hili swala kwa jicho la imani ili Wakenya wapate haki yao. Asante. view
  • 3 Aug 2023 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. Nampa kongole dadangu Sen. Kibwana kwa kauli aliyoleta Seneti. Tunaelewa ya kwamba, Wakenya wenzetu walio na akili punguani wanaenda hizo hospitali za akili punguani ili kupata matibabu. Lakini, tukiangalia zile sehemu zao za matibabu na vifaa vinayotumika kuwaweka katika yale maeneo, hali ya usafi na hali ya chakula, Serikali inafaa itafakari zaidi na kuhakikisha kuna madaktari wa kutosha ambao wana ile taaluma inayotumika kufanya hayo matibabu. Nilitembelea hospitali ya Port Reitz, eneo la Pwani. Matokeo tuliona kule yalikuwa hayafai hata kidogo. Hali ya usafi imepungua. Hali wanavyokaa wakati wanapokea matibabu, haiwezi changia watibiwe na kupona. Mtu, hata ... view
  • 2 Aug 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 2 Aug 2023 in Senate: Watu kama hawa wanapatikana katika nchi nzima, katika kila kaunti. Wanastahili kuwekwa katika hali nzuri. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus