2 Aug 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa hilo ulilolitamka. Nakubaliana na wewe kabisa ya kwamba sikutaja Meru pengine afikirie mimi nimesema huko tu. Huko kuna watu wangu na ndugu zangu wengi. Niko na familia ambayo damu yao iko upande huo. Kwa hivyo ninakubaliana kabisa na yale aliyosema. Sikusema hivyo.
view
2 Aug 2023 in Senate:
Bw. Spika, naomba nimjibu kwa sababu message ambayo amepeleka ni mbaya.
view
2 Aug 2023 in Senate:
Wakati mwingine watu kama akina Sen. Wambua wakichangia, tunasema pia hospitali kama ipo, iko huko Kitui. Lakini la kumalizia ni kwamba, taarifa hii ni nzuri na iko na mwelekeo mzuri. Tunaomba kabisa itakapopelekwa kwa Kamati itakayo shughulika nayo, ionelee ya kwamba katika kila eneo katika kaunti arobaini na saba, kuwe na hospitali kama hizi.
view
2 Aug 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika. Kwa Hoja ya Nidhamu, ukiangalia tabia za wale Maseneta wengine walio hapa ni vizuri kutimiza zile Kanuni za Kudumu. Sen. Orwoba ametoka upande ule akafika hapa katikati na kupita badala ya kwenda kwa mlango na kuinama, ili aje upande huu mwingine kulingana na taratibu zetu. Jambo lingine vile vile, Sen. Miraj amefanya kitendo kama hicho hapa mbele yetu. Sijui kama wanafaa kuomba msamaha kwa vitendo walivyofanya ama wakirejelee ili walifanye sawa sawa.
view
27 Jul 2023 in Senate:
Asante Bw. Spika. Kwanza, ninawapa kongole walimu walioleta Taarifa hii. Tunaelewa ya kwamba sisi zote ni watu waliohitimu kutoka kwa akili na mafunzo ya walimu. Taarifa hii ni muhimu sana ndani ya Bunge hili la Seneti. Ya kwamba tuweze kuangalia matatizo yanayowakumba walimu katika sehemu zao zote wanazofanya kazi katika inchi nzima ya Kenya. Taarifa hii imeletwa na watu wa Kilifi. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Kilifi, ninajua matatizo yanayowakumba waalimu katika maeneo waliyoyataja hapa. Ninaona Petition hii ni ya haki na ukweli. Kuna sehemu zingine ndani ya Kaunti ya Kilifi ambazo zimefika katika kiwango ambacho mapato yao hayalingani ...
view
27 Jul 2023 in Senate:
Bw. Spika, wale ambao hawajui Kiswahili---
view
27 Jul 2023 in Senate:
Bw. Spika, je, ni sawa kusema kwamba kwa sababu ya yale yaliyojiri nje ya Bunge wala si hapa kwa sababu kazi ya Bunge ni tofauti--- Tukiwa hapa, tunafanya kazi ya Bunge. Je, ni sawa mtu kuambiwa---
view