1 Dec 2022 in Senate:
Bw. Spika wa muda, umenipa muda kidogo lakini nataka kuongezea zaidi kwa kusema kwamba tumekua tukiona wakati wa likizo kama Krismasi, polisi wanafurahia sana kushika watu waliochelewa ama kushika watu ovyo ovyo kwenye vilabu. Huu ni wakati wa Wakenya kufurahia juhudi zao za mwaka mzima na itakuwa jambo la kusikitisha ikiwa polisi wataregelea ule mfumo wao wa kushika watu Ijumaa na kuwaachilia Jumatatu au kushika watu kiholela na kuwaambia watoe pesa. Ni jambo la kusikitisha.
view
1 Dec 2022 in Senate:
Umesikia ukiwa hapa kuwa kuna jambo la kununua watu. Wanasiasa wengi wanakumbwa na shida na inafika wakati wanaambiwa waende upande fulani. Tumeanza kuona hiyo ni hatari kwa sababu kuna nia au njama ya kuvunja upinzani katika taifa letu. Tunawaambia ndugu zetu walio katika mamlaka, waendelee lakini tunawaangalia.
view
1 Dec 2022 in Senate:
Mambo ya kuruka upande huu na kuanza kununua wanasiasa ni jambo la aibu. Utapata kiongozi aliyechaguliwa na wananchi akifika bungeni, anageuza msimamo wake na kuwa rangi nyingine; anaenda upande ambao hakuchaguliwa kwa ajili ya kusisitiza maslahi yake. Ninawaambia ndugu zangu ambao wako na tabia kama hizi waziwache. Hakuna kitu kizuri maishani kama kuwa na msimamo.
view
1 Dec 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
1 Dec 2022 in Senate:
Hata kama wameshinda au kuchukua uongozi, hawakuchukua uongozi kwa sababu hawakuwa na msimamo. Walikuwa na msimamo. Baada ya kukaa kwa mamlaka, sisi kama wanasiasa, tujifunze kuwa na msimamo. Tusiende upande huu ama ule.
view
1 Dec 2022 in Senate:
Ukiwa umechaguliwa na chama fulani, itakuwa jambo la kusikitisha wewe kuondoka na kuenda chama kingine baada ya kupita au kuangalia sera za chama kingine na kusema ndicho chama chako.
view
23 Nov 2022 in Senate:
Ahsante, Bw. Spika. Kwanza, ninataka kupatia dada yetu, Sen. Crystal Asige, kongole kwa taarifa hii ya walemavu. Walemavu wako katika aina mbalimbali. Utapata kuwa kuna walemavu wa macho ambao hawawezi kuona, kama dada yetu, Sen Crystal Asige, kuna walemavu hawawezi kutembea, wale ambao hawawezi kusikia na kadhalika. Ni muhimu sana kuona ya kwamba tumeweka mikakati ya kutosha katika hospitali zetu ili walemavu waweze kuwa na njia ya kupitia. Nimekuwa katika hospitali yetu ya Kilifi na sijaona mikakati mzuri ndani ya hospitali ya kuwezesha walemavu kupita katika zile njia bila kupata taabu. Ukienda upande wa ngazi, walemavu wanakuwa na shida wakiwa ...
view
22 Nov 2022 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise on a point of order. I have a Notice of Motion on Adjournment, to discuss a definite matter of urgent national importance. Mr. Speaker, Sir, I have an urgent matter, that I would like to place before the House and therefore, I would request for adjournment to discuss this definite matter of urgent national importance.
view
22 Nov 2022 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I would like us to discuss the Genetically Modified Organisms (GMOs), such---
view