Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 651 to 660 of 2266.

  • 1 Dec 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Kwa hivyo, wakae wakijua, huko nyumbani ya kwamba, wanawakilishwa hapa ndani ya Bunge la Seneti na Seneta mshupavu zaidi. Namtakia ndugu yangu kila la heri katika juhudi zake za kuleta maendeleo huko nyumbani. Cha pili ni kuwakumbusha wabunge wa County Assembly ya Baringo kwamba wakati wa kampeni umekwisha. Mara nyingi tunaona ni kama tunaenda katika hali ya kampeni lakini mambo ya kampeni sasa yamekwisha. Kazi iliopo sasa ni hao kujitokeza wazi na kusaidia watu wa Baringo ambao waliwapeleka katika hilo bunge. Mimi ninataka kusisitiza tu kitu kimoja. Tuwache kusema upande huu ulishinda na upande huu ulishindwa. Tunajua walioshinda. Kama kulikuwa ... view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Kwa muhula huu ambao wapo ndani ya hilo bunge, itakuwa vyema kuona ya kwamba wameweza kutenda kazi, kulinda pesa na kutekeleza wajibu wao katika lile bunge la kaunti. Lazima waone ya kwamba zile pesa hazijatumika kwa njia mbaya na miradi ambayo imewekwa ama imepangwa kufanywa imefanywa ili watu wa Baringo wafaidike na hizo miradi. La mwisho, hatuko katika mashindano ya akili. Kama ni kushindana kwa akili, upande huu pia uko na profesa wa sheria. Tuko na watu ambao wamesoma zaidi na watu washupavu. Ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, ni daktari na upande huu uko na profesa wa sheria. Ndugu zangu ... view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Bw. Naibu Spika, sijui kama umeskia nilichoskia. Ni haki kwa ndugu yangu Sen. Cherarkey kusema ya kuwa, MCA ndio mtu wa kwanza wa kumuuliza kabla hujaenda kuoa bibi yako ambaye utaishi naye miaka yote mpaka ufe? view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Hoja ya nidhamu, Bw. Spika wa muda. Bahati mbaya, ndugu yangu amemaliza kuongea. Katika uwanja wa siasa, kila mtu ana majukumu ya kuchagua pale anataka. Sen. (Dkt.) Khalwale akipewa nafasi ya kuongea hapa, huo si uwanja wa kuanza kutongozona, kuitana na kusema kuja upande huu. Mimi nafikiria niko vyema na niko sawa kabisa nikiwa upande huu wa upinzani; upande wa Baba Raila Amollo Odinga. Asante. view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Mimi kama kiongozi ninaomba nipewe muda kidogo hata nikizidisha dakika tano, sita, saba ama nane. Asante kwa nafasi. Ndugu yangu, Sen. Cherarkey, anafuraha sana. Sijui kama ametoka huko kwenye vinywaji ama ni namna gani? Tangu kura zipigwe na maseneta wachaguliwe wakaingia ndani ya bunge na kuketi hapa, tumekuwa na ratiba ya kazi nyingi. Tumekuwa na shughuli nyingi na view
  • 1 Dec 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Maseneta wote katika hii Bunge wamekuwa wakishirikiana kuona kuwa wameenda njia moja mwanzo wa safari hii. Maseneta wametaka kuona kuwa tumefanyia Wakenya juhudi wanazozihitaji katika utendakazi wetu kama Maseneta. Sisi bado hatujafanya kile ambacho Seneti iliyopita ilifanya na ninatumaini kuwa wakati wetu ukifika, tutafanya hivyo. Ninatumaini ya kwamba tutapeleka Bunge la Seneti mashinani. Tumekuwa hapa Nairobi na ingekuwa vizuri tutakaporudi, tupate nafasi ya kuenda mashinani ili Bunge letu la Seneti lijulikane kule mashinani kwa kazi ambayo tunafanya. Hivi sasa, ninaona muda umeenda. Tumekuwa hapa pamoja karibu miezi mitatu au nne na sasa ni wakati wa kuenda mapumzikoni. Ninaunga mkono Hoja ... view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Tunapoenda likizoni, tunaomba serikali izingatie janga la njaa ili lisipatakaa kila mahali katika nchi yetu ya Kenya. Watu ambao wanaishi katika ardhi ambazo hazipati mazao ama mimea wameathiriwa sana na janga hili la njaa. view
  • 1 Dec 2022 in Senate: Njaa imekithiri zaidi mahali kama Kaunti ya Kilifi, Garissa unakotoka, Wajir na Turkana na serikali inatakikana iweke mkazo zaidi. Hayo ni maeneo ambayo yamekumbwa sana na baa la njaa. Haitakuwa vyema iwapo tutakwenda kwa Krismasi wengine wakiwa wanafuraha na wengine wakifa kwa njaa. Haitakuwa vyema Serikali ikiangalia watu wake wakifa. Ni jukumu la Serikali kuona kuwa hakuna Mkenya atapoteza maisha yake kwa sababu ya njaa katika ya nchi yetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus