15 Nov 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nampa kongole Seneta wa Kaunti ya Kitui kwa kuweza kuleta Hoja hii. Imekuwa mtindo sasa katika sehemu fulani za nchi yetu ya Kenya ambako watu wanaleta mifugo, wanakuwa huru kuingia na kuweza kuyalisha hiyo mimea ya watu waliyotia bidi kuyapanda katika mashamba yao. Ni jambo la kusikitisha sana ikiwa mifugo hiyo inaharibu mali na mimea ya watu wa Kitui ambako kuna njaa. Watu wenyewe ni maskini lakini wamefanya bidi katika mashamba yao. Wamepanda halafu watu wengine wanakuja na ng’ombe, mbuzi na ngamia na kulisha katika mashamba yao ambayo siyo ardhi yao. Bw. Spika wa ...
view
15 Nov 2022 in Senate:
Kama Kiongozi wa Wachache Bungeni naomba unipe dakika mbili nimalize. Tafadhali.
view
15 Nov 2022 in Senate:
Ningeomba unipatie dakika mbili niweze kumaliza.
view
15 Nov 2022 in Senate:
Nataka kumaliza nikitumia dakika mbili tafadhali.
view
15 Nov 2022 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, utaona ya kwamba, sasa polisi wametaarifiwa na halafu walipoondoka, wale watu wamerudi tena. Hivi sasa tunavyoongea, wameingia na mifugo yao maeneo ya Kamale katika lile ziwa la Dera, wameweka ngamia hapo wanakunywa maji.
view
15 Nov 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
15 Nov 2022 in Senate:
Inabidi binadamu wanakunywa maji pamoja na wanyama. Ngamia na ng’ombe wanakunywa hapo. Halafu wanawaingiza ndani ya mashamba ya Wagiriama wanakula mimea yao. Hii italeta vita ambavyo Serikali itashindwa kukomesha. Hatutakubali hata kidogo kuona watu wetu wanafanya bidii kulima na kupanda mahindi na vyakula vingine, halafu watu wengine wanakuja na ngamia au ng’ombe kuliwalisha mimea ambayo hawakufanyia bidii. Inatatikana Serikali ichukue hatua. Tuko na Seneta mchapakazi, Mhe. (Prof.) Kindiki, ambaye amechaguliwa juzi kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Tunamwomba aanze kazi yake ili asilaumiwe. Kenya hii sasa tunaona watu wengine wanadharau wenzao. Sisi kama watu wa Kaunti ya Kilifi, hatutakubali hata ...
view
10 Nov 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninampa kongole Sen. Crystal Asige kwa hii Taarifa. Mambo ya ulemavu ni ya kusikitisha sana. Hakuna familia katika Kenya, jamii au marafiki ambao hawajaona familia ama kukumbwa na janga hili la kuwa na mtoto au
view
10 Nov 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
10 Nov 2022 in Senate:
watoto walemavu. Mimi nimmoja wao kwa kuwa tuko na mmoja ambaye pia hali yake ni hali ya ulemavu na ya kusikitisha. Pia ingekuwa vyema kufikiria kuongeza idadi ya walimu wanaoweza kufundisha watoto walemavu. Ingekuwa muhimu kuhakikisha usalama wao hatari inapotokea. Wakati mwingine watoto hawawezi kutembea. kunaweza kuwa na hatari kama ya moto, mafuriko au nyumba kuporomoka. Itabidi wawe na haraka ya uzaidizi kuona kwamba madhara kama hayo hayatawapata watoto walemavu katika nchi hii. Mwisho, ninatoa kongole kubwa sana kwa rafiki yangu mmoja kule Mombasa - Bw. Hasu - ambaye ndiye mwenye ile kampuni ya Mombasa Cement. Ni kampuni ya kutengeneza ...
view