Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 821 to 830 of 2266.

  • 5 Oct 2022 in Senate: Asante Bw. Naibu wa Spika. Kwanza ninawapa kongole wanafunzi wote wanaofanya kazi katika hili Bunge la Seneti. Wako katika hali ya kujifunza jinsi kazi inafanywa ili watakapomaliza masomo, wawe wafanyakazi wa kutekeleza majukumu yao. Ninakubaliana na ndugu yangu, Sen. Mungatana, kuwa ingekuwa vyema kuona wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali ya taifa la Kenya. Tusiwatoe tu kaunti moja peke yake. Ni jambo muhimu kuwa Bunge la Seneti linatoa fursa kwa wanafunzi, waje kujionea viongozi wao wakiwa kazini. Watakapotoka hapa, watakuwa na elimu ya kutosha ambayo itawasaidia maishani. Vilevile, ni vizuri hili Bunge la Seneti lionyeshe mfano bora. Ni muhimu na pia ni ... view
  • 5 Oct 2022 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, this is a Procedural Motion. I second. view
  • 5 Oct 2022 in Senate: If the House is agreeable to that, then I will proceed to put the question. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, asante sana. Kitu cha kwanza umesema ya kwamba lazima mtu abonyeze kidole ili uweze kuona katika kile kioo chako ulicho nacho hapo mbele. Utaweza kuona ni nani amefinya kibonyezo cha hoja ya nidhamu. Bw. Spika, katika Bunge hili, ni kawaida ya kwamba upande ya walio wachache na walio wengi, mtu yeyote anaweza kubonyeza kidole. Lakini, kwa mara ya kwanza, ninaona ya kwamba huyu ndugu yangu Sen. Olekina alikuwa amebonyeza kidole cha komputa lakini pengine wewe umeona ama pengine umefinya jicho lako moja hukuweza kuiona. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Nasema vile ilivyo. Hiki ni Kiswahili. Umefinya jicho lako moja hukuweza kuona ndio sababu ukakosa kumtaja. Lakini nadhani kwamba ikiwa hoja ya nidhamu iko upande hii au upande ule--- view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, siwezi kufanya hivyo. Siwezi kufanya namna hivyo wala kusema kitu kama hicho lakini najua binadamu sio kamili. Pengine umepitiliwa na hukuona kama alikuwa amefinya hicho kidole. Sina shida na yale aliyotamka ndugu yangu Sen. Khalwale. Asante Bw. Spika. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, naunga mkono. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Bw. Spika, Bunge la Seneti ni la hali ya juu kwa sababu ya taratibu zake za debate. Ninakusihi uangalie hii barua iliyoandikwa na Bi. Anne Njeri Nderitu ambaye ni Registrar of Political Parties. Hii barua iliandikwa tarehe 7 Septemba, 2022. Iliandikiwa Clerk wa Seneti. Barua hii inahusikana na ile barua ambayo yeye alikuwa amepeleka tarehe 6 Septemba, 2022 akitaka kujua vyama viko upande gani. Hii barua inasema kwamba UDM– view
  • 4 Oct 2022 in Senate: Barua hii iko na Clerk wetu ndani ya Bunge la Seneti. Nataka kumuuliza Clerk, ikiwa itawezekena--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus