15 Jun 2022 in Senate:
Tunaona kuna uzembe fulani unaoendelea katika Wizaya Kawi. Wale wanaohusika, wakati mwingine wanaongeza bei vile wanavyotaka. Hali hii inafanya maisha ya Wakenya kuwa magumu sana. Tunaelewa kabisa ya kwamba unapoguza mafuta, umeguza maisha ya mwananchi. Utakuwa umeguza bei ya hospitali wagonjwa wanapoenda kutibiwa na bei ya chakula kupanda juu. Vilevile, haiwezekani kufanya maendeleo pasipo matingatinga kuenda katika mashamba. Bunge huwa halivunjwi; linahairishwa. Tuko na Kamati ambayo inahusika ya mambo ya kawi. Hili swala linapasa kupelekwa katika hiyo Kamati yetu ya Kawi, kuangaliwa na kuhusika katika hii kazi. Ninampa kongole tena ndugu yangu kwa sababu yeye huwa anaongea mambo ya Wamaasai ...
view
7 Jun 2022 in Senate:
Asante, Bi. Naibu Spika. Naungana nawe kwa kupeana rambirambi zangu kwa familia, jamii na marafiki wa William Mwamkale Kamoti. Ni huzuni sana kusimama hapa na kuongea juu ya William Kamoti. Alikuwa Mbunge wangu katika Eneo Bunge la Rabai ambalo liko katika Kaunti ya Kilifi. Kamoti alikuwa mwandani wangu. Tulikuwa kama ndugu. Hili ni pigo kubwa sana kwa familia. Kwa niaba yangu, familia yangu ambayo ni moja, jamii yangu na watu wote wa Kilifi, sisi sote tunaomboleza kifo cha Kamoti. Bi. Naibu Spika, kama kila mtu alivyosema, Kamoti alikuwa mtu mungwana. Alikuwa wakili. Wakati mwingine tukipiga kelele na kufanya fujo, alikuwa ...
view
7 Jun 2022 in Senate:
Mheshimiwa Kamoti ameacha familia changa inayohitaji msaada. Familia yake inahitaji kila mmoja wetu kusaidia katika maombi na msaada wa aina yoyote. Alikuwa mmoja wetu katika chama cha ODM ambacho sasa kiko katika Muungano wa Azimio la Kenya. Alikuwa ni sure bet katika kura za tarehe tisa mwezi wa nane ambapo tutampigia ‘Baba’. Alikuwa mmoja wa wagombeaji katika Kaunti ya Kilifi ambapo angepigiwa kura kama Mbunge wa Rabai. Kwa hivi sasa watu wa Eneo Bunge la Rabai ni kama wameshikwa na butwaa na huzuni; hawajui sasa washike mti gani. Lakini tuko na imani ya kwamba yule ambaye ameteuliwa na chama cha ...
view
7 Jun 2022 in Senate:
Madam Deputy Speaker, I am not Sen. M. Kajwang’. My name is Sen. Madzayo.
view
7 Jun 2022 in Senate:
Thank you, Madam Deputy Speaker. I beg to lay the following Petition Report on the Table of the Senate today, 7th June, 2022. With your kind permission, if you will allow me, I will make a few comments. This Petition concerns appropriate leave rights for women who miscarry and suffer stillbirths. The Petition was reported to the Senate on Tuesday, 15th February, 2022, by the Speaker of the Senate. One of the salient issues raised in the Petition is that Section 29 of the Employment Act provides for maternity and paternity leave. It does not provide for a definition of ...
view
7 Jun 2022 in Senate:
Despite the setback mentioned above, the Committee noted a grave concern raised by the Petitioner and did a comparative analysis on how other jurisdictions dealt with the issues. The Committee noted that in Philippines, the law provides for 60 days of paid leave for miscarriages or emergency termination of pregnancy. India allows six weeks of payed leave. The United Kingdom (UK) provides for two weeks for bereavement of a child from pregnancy of after 24 weeks to a child of 18 years. In the United States of America (USA), the federal laws are silent on the matter. The Committee appreciated ...
view
18 May 2022 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda. Kitu cha kwanza, ninaungana na wewe kuwakaribisha maafisa wanaofanya kazi katika serikali za ugatuzi. Maafisa hao 31 wameingia katika Bunge la Seneti ili kujionea hali inavyoendelea. La muhimu ni kwamba hawa wafanyakazi katika maktaba wamekuja hapa kujionea na kupata faida ya kusoma na kujua jinsi ya kuendeleza maktaba huko wanakofanya kazi. Cha muhimu ni kuona watakaporudi wanakotoka, wataenda na elimu ambayo itawafaa katika kazi zao. Ninaona watu 31 lakini niko na imani pengine wale waliobaki, pia watapata nafasi ya kuja. Nimeangalia hii orodha nikaona wanatoka kaunti 31, lakini katika hii orodha, Kaunti ya Kilifi haipo. ...
view
18 May 2022 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nataka kuongeza kidogo nikisema ya kwamba wale waliotengeza barabara walikuja hapa Kenya wakapata kwamba kuna barabara zake tayari. Walitoboa mashimo, na kutengeneza barabara yao nzuri sana. Mimi nishawahi kuipitia. Lakini sasa, waliharibu barabara ya chini. Kuna umuhimu ya kwamba anayeharibu ndiye anayetengeza. Ninaona kuna mushkil hapo ya watu fulani kutaka kuingia katika mambo ya ufisadi; Hizo Kshs9 billion ni pesa za Wakenya walalahoi ambao wanajaribu sana kuishi katika hii inchi ambayo imekuwa ghali kwa watu kuishi. Tunataka kujua ni kwa nini wanauliza swala la kuongezwa pesa za Kshs9 billion ili kutengeza sehemu ambayo iliharibiwa na wale ...
view
18 May 2022 in Senate:
Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. I second.
view
18 May 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda. Ninasimama kwa hoja ya nidhamu. Ikiwa yule ambaye anazungumziwa hayuko ndani ya Bunge wala hajaitwa Bungeni na kuulizwa kisha akashindwa kujibu, mtu anaweza kusema alimwuliza na hakuweko? Je, ni haki? Waziri wa Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Vyama vya Ushirika, hayuko hapa. Katika mjadala unaoendelea hivi sasa, ndugu yangu anamtaja. Singependa kabisa kumuingilia kati rafiki yangu, mdogo wangu ambaye ninampenda sana na tunasikizana zaidi. Ni haki kuongea juu ya mtu ambaye hayuko ndani ya Bunge kwa njia ambayo haifai, ama kumwonyesha katika Taifa ya kwamba pengine si mtenda kazi maalum? Watu wengine kama sisi tunajua yeye ...
view