Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 861 to 870 of 2266.

  • 18 May 2022 in Senate: Bwana Spika wa Muda, mwacha asili ni mtumwa. Sote kama Waafrika tukona asili zetu tofautitofauti. Ukiniambia niwache pombe ya mnazi itakuwa si sawa. Ijapokuwa mimi si Mmaasai lakini naishi naye kila siku nikiingia na nikitoka pia. Yeye ni ndungu yangu na rafiki yangu. Nimeenda ambapo amezaliwa, Kijiji kile na mahali familia yake yote ip, naijuwa. Katika miendendo na asili za wa-Maasai fimbo ni mmojawapo ya nguo ambazo wanazovaa. Huwezi kua Maasai na ukawa mikono yako ni mitupu kama hii yangu. Uamuzi uliotoa kwamba kinaweza kuwa kifaa hatari, si rahisi sana Wamaasai kuwa na hasira za kuanza vita. Labda awe amechokozwa ... view
  • 26 Apr 2022 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninaungana na wewe kutoa rambirambi. Ningependa pia kutoa rambirambi kwa niaba ya familia yangu na hususan watu wangu wa Kaunti ya Kilifi ambao walinipa nafasi hii kuwaakilisha katika Bunge la Seneti. Rambirambi ziwaendee watu wa Kaunti ya Nyeri, eneo Bunge la Othaya na familia ya mwendazake, marehemu Mwai Kibaki. Kitu cha maana cha kumkumbukia marehemu ni ushupavu wake katika mijadala Bungeni. Katika historia ya wanasiasa waliokuwa Bungeni, yeye alikuwa mmoja wao wa kipau mbele. Alikuwa Bungeni kwa zaidi ya miaka 50. Bi. Naibu Spika, wewe na mimi tunaelewa ya kwamba kuketi ... view
  • 26 Apr 2022 in Senate: nilipochaguliwa kama Mwenyekiti wa Shirika la Ukulima nchini Kenya, Mhe. Mwai Kibaki ndiye alichaguliwa kuwa Rais. Huo ndio wakati ambapo tulikutana wakati wa Maonyesho ya Kilimo, ambayo yanafanyika kila mahali nchini Kenya. Tulizunguka na yeye nikiwa Mwenyekiti wa Shirika la Ukulima naye akiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya na Patron wa kilele cha wakulima wa Kenya. Kila tulipokuwa na maonyesho hayo, kama patron, ilibidi aje kufungua maonyesho kirasmi. Nilikuwa karibu sana na yeye kiasi cha kupanda gari la Commander-in- view
  • 26 Apr 2022 in Senate: pamoja na yeye. Hilo ndilo gari ambalo tulikuwa tukitumia kuzunguka wakati wa kufungua maonyesho ya ukulima. Huo ndio wakati ambapo nilikuwa karibu naye na nikajua alikuwa mtu wa aina gani. Alipenda nchi yake na alihisi kwamba lazima wakulima wasaidiwe. Ninakumbuka ni wakati wake ambapo bei ya mbolea ilishuka chini. Wakulima waliweza kumudu bei ya mbolea; walilima na nchi ikawa na mazao tele. Wakati wa Rais Kibaki, hapakuwa na baa la njaa jinsi ambavyo watu wanaaga kwa njaa siku hizi. Rais Kibaki alifungua uchumi na kuwapa wakulima mbolea kwa bei nafuu ili wakuze chakula cha kutosha nchi nzima. Bi. Naibu Spika, ... view
  • 26 Apr 2022 in Senate: Rais. Siwezi kusema ni nani sasa, lakini tunajua yule Rais wangu ndiye atakaye kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Kwa hivyo, ikiwa ni yeye ndiye atakaye kuwa Rais, tuna imani kwamba yeye ataweza pia kuiga mfano wa Rais Kibaki, kwa sababu walikuwa pamoja katika Serikali ya “Nusu Mkate.” Ikiwa yeye ataenda kuongoza hii nchi yetu, basi jambo la kwanza la yeye kufanya kama Rais wa Jamhuri ya Kenya ni kupigana na ufisadi kama vile Rais Mwai Kibaki alipigana na ufisadi. Asante Bi Spika. view
  • 7 Apr 2022 in Senate: Madam Temporary Speaker, I beg to lay the following Paper on the Table of the Senate today, Thursday, 7th April 2022. view
  • 7 Apr 2022 in Senate: Report on the Standing Committee on Labour and Social Welfare on the Sports Amendment Bill (Senate Bill No.40 of 2021). I thank you. view
  • 7 Apr 2022 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kwanza, nampa kongole Sen. Shiyonga kwa kuleta Taarifa hii kuhusu upungufu wa chakula katika nchi yetu. view
  • 7 Apr 2022 in Senate: Ni kweli kwamba chakula ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Kama inavyojulikana, Kenya ni nchi ya ukulima. Ni jambo la aibu kwamba Wakenya wanahangaika kwa sababu ya ukame ambao umesababisha ukosefu wa chakula. view
  • 7 Apr 2022 in Senate: Yote hayo yanasababishwa na ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wale walio na jukumu la kuhakikisha kuwa kuna chakula cha kutosha nchini. Wale wanaopewa majukumu hawayatimizi ili kuhakikisha kuna chakula cha kutosha nchini. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus