20 Apr 2016 in National Assembly:
Mheshimwa Naibu Spika wa Muda, naomba kutoa mchango wangu kama mwanakamati wa Kamati ya Ardhi. Tumekaa katika vikao na kuchangia itoshavyo. Ni matumaini yangu kuwa Mswada huu utawafaidi watu wa nchi hii ijapokuwa tumekuwa na changamoto nyingi. Nashukuru kwa yale ambayo yamepita kuwa watu wameweza kuridhiana na kukubaliana kuwa yale mapendekezo yote ambayo yaliletwa, hasa na ndugu zetu wachungaji na Wabunge wa Pwani, yamewekwa ndani na tukakubaliana. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu.
view
14 Apr 2016 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kusimama kwa hoja ya nidhamu. Je, Mheshimiwa anayezungumza hivi sasa ana haki ya kuzungumza yale anayosema kuwa tunachukua hundi ya Hazina ya Ustawishaji Maeneo Bunge na kuipeleka nyumbani? Nani anapeleka hundi ya Hazina ya Ustawishaji Maeneo Bunge nyumbani? Labda ni maongezi yake ya mwanzo. Naomba afafanue.
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Asante, Mheshimiwa Spika. Nimesikia ombi la Mwenyekiti wa Kamati kuhusu fedha ambazo zinaombwa kimkopo. Ni muhimu kuwa ijapokuwa Bandari inaomba hizi fedha, kuwe na uangalifu mzuri. Mara nyingi, mashirika yanaomba hela ama fedha na mara nyingi yanakabidhiwa fedha hizo lakini ule utumizi wake unatia hofu. Naomba Bunge likubali kuwaongezea ule muda ambao wameomba. Kuongeza huo muda kutakuwa ni jambo la busara. Itawabidi nao wazingatie mambo mawili au matatu. Taasisi hii imetimiza yale ambayo yalitakiwa yafanywe katika mwango wa kwanza maana kuna kipindi cha kwanza. Waliomba fedha na tungependa kujua kama peza hizo zimetumiwa kama vile walivyosema. La pili, wakiongezewa muda ...
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba nami nitoe mchango wangu kidogo kuhusu sheria hii. Hizi sheria vile zilivyo, hakuna mtu yoyote anayeweza kuziunga mkono. Mimi kama mwanakamati, naziunga mkono kwa sababu nazijua na nazielewa. Kuna mabadiliko kadhaa ambayo tumekubaliana kama wanakamati kuyaleta hapa, ili turekebishe pale ambapo tunaona kuna upungufu. Kama si hivyo, zingekuwa na utata na hazingeridhi
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nimesikia ombi la mwenzangu ambaye ni wakili na namheshimu sana. Nashukuru kwa kuwa haujakataa hilo ombi, ila umelichukulia maanani. Vile alivyosema kuwa anaona kweli nafaa kuwa gavana, namshukuru na naomba kuwa Mungu azidi kulirehemu na kulibariki ombi lake. Tutakutana wakati mwingine. Ni muhimu tuangalie kuwa hizi sheria ambazo tumezipitisha hapa na ambazo tutazipitisha tukipata nafasi, Inshallah Mungu akipenda, ziwe sheria ambazo zitaendesha nchi yetu isije ikapata matatizo kwa sababu ya ardhi. Langu la muhimu ni kuangalia vipi tutakavyofanya na ile rasilimali tulionayo. Vile ilivyo, itabidi wale watu ambao wamefanyiwa maovu tangu hapo awali watafute ...
view
15 Mar 2016 in National Assembly:
Nashukuru Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii umenipatia nami nitoe mchango wangu.
view
15 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika Naibu wa Muda, Migingo ni sehemu ya Kenya.
view
15 Mar 2016 in National Assembly:
Natumaini muda wangu unaangaliwa usije ukaisha kwa sababu ya shughuli za kuangalia nani amezungumza na nani hajazungumza. Kisiwa cha Migingo ni sehemu ya Kenya. Mimi ni Mkenya na nawakilisha sehemu ya Wundanyi ya Taita Taveta ambayo ni sehemu ya Kenya. Sehemu yoyote ya Kenya ikiguswa na mtu yeyote, nina haki ya kuzungumza kuhusu jambo hilo na kutoa mchango wangu. La pili, tumesikia na tumeelezwa kuwa mara nyingi Hoja zimeletwa hapa Bungeni kuhusu Kisiwa cha Migingo lakini hakuna lolote linalofanywa. Watu wanaumia, wanauawa, wananyang’anywa mali yao na Serikali yetu inaangalia. Kulingana na maoni ambayo yametolewa hapa leo, tumeelezwa kuwa kulikuwa na ...
view
15 Mar 2016 in National Assembly:
ya kina Joho hayaturidhishi yakifanywa humu nchini kwa Wakenya. Kwa hivyo naweka mkazo na nasisitiza kuwa wakati umefika Serikali ichukue hatua kuwalinda watu wa Migingo. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
10 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, nakushukuru kwa muda ambao umenipatia niwasiliane na wenzangu katika Ukumbi huu.
view