10 Mar 2016 in National Assembly:
Kama Mhe. Duale haelewi Kiswahili, basi niko radhi nimpatie masomo ya bure wala sitamlipisha chochote.
view
10 Mar 2016 in National Assembly:
Naomba radhi, Mhe. Spika. Waheshimiwa Wabunge, naomba tuelewane ili tujue nini tunatakiwa tufanye. Sio eti hamuelewi. Najua mnaelewa lakini, naomba tuelewane. Tukishaelewana, tutajua upande tutakaoenda. Kitu cha kwanza, kuna Hoja iliyoletwa hapa. Hoja ilipoletwa, tuliikataa. Hoja ililetwa ili kuona kama tutawakubali hawa wenzetu ambao wameteuliwa kushughulikia mambo ya makadirio ya fedha. Mliwakataa. Sasa ni lipi tutakalofanya? Nikiangalia vile hisia zenu zilivyo, inabainika waziwazi kuwa hata wakiletwa hivi sasa, mtawakataa tena.
view
10 Mar 2016 in National Assembly:
Naomba tuelewane. Mhe. Spika, tumekubaliana mara nyingi kuwa ni muhimu tuangalie hisia za wengi. Hisia zao zinaonyesha waziwazi kuwa hawangependelea hao waheshimiwa warudishwe. Wanatupatia muda tulete kamati nyingine. Kwa hisani yenu, nawaomba tuelewane. Bila shaka, itabidi Waheshimiwa waamue kama wanaunga Hoja hii mkono au la. Kama hawaungi mkono, basi tujue tutafanya nini. Naomba hili jambo nilirudishe mikononi mwako ili The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
10 Mar 2016 in National Assembly:
maamuzi yafanywe. Lakini la busara ni kukuomba tusitishe majadiliano. Tusimamishe majadiliano haya ili tupate muda wa kuwasiliana na kuzungumziana. Tusiendelee na mjadala huu leo. Naomba ukubali ombi langu kama kinara wa Bunge. Tusiendelee na mjadala huu. Mhe. Spika, narudisha kwako.
view
8 Mar 2016 in National Assembly:
Asante sana, Naibu Mwenyekiti wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ninashangaa ni kwa nini wenzangu wanafikiria kuwa sehemu hii iondolewe ili tuhakikishe kuwa mafuta na gesi zikipatikana basi watu wawili, mwanakandarasi na waziri wakishakubaliana yameisha, halafu ndio baadaye iletwe Bungeni. Kama kuna njia moja mbaya ya kuleta---
view
8 Mar 2016 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda, vile nilivyoelewa ni kuwa- --
view
8 Mar 2016 in National Assembly:
Wacha nifuate mwelekeo wako, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Yangu ni kusema kwamba nchi nyingi zimegombana na zimefanya watu wakawa maskini, haswa wakati mafuta ama gesi imepatikana kwa sababu mikataba inawekwa bila Bunge kuhusishwa. Wakati umefika tukubaliane kama Bunge kuwa mikataba yoyote ambayo itawekwa lazima iletwe Bungeni, hasa hii ya mafuta, kabla lolote kufanywa ili tujue ni nini iko ndani yake. Tunaweza kuwa tunajitia kitanzi. Mara nyingi tumejitia kitanzi. Mikataba imewekwa na baadaye ikiletwa hapa Bungeni, tunajikuta tumejifunga. Hatuna la kufanya na hatuwezi kujitoa kwenye mikataba hiyo. Wakati umefika ikiwa tunatunga sheria, tuhakikishe kuwa tumeangalia wale watu wako na hizo ...
view
8 Mar 2016 in National Assembly:
Ombi ambalo limeletwa na Mhe. Amina Abdalla na Mhe. Profesa Nyikal ni nzuri. Nawashukuru kwa njia ya kipekee kwa kuona pahali tatizo liko. Naomba Wabunge wenzangu tukubaliane kwa kauli moja. Hata tusibishane. Wakati umefika tuunde hii sheria kuwa mikataba italetwa hapa, hasa ya mafuta, kabla watu kupanga mikakati yao ya kunyanyasa Wakenya. Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda, naunga mikono. Asante.
view
8 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba kupongeza wenzangu kwa vile tumeangalia Mswada huu kikamilifu na kwa undani. Mwisho, tukakubaliana ya kuwa kile kipengele kilikuwa kinatupatia shida, tumekisawasisha na kukubaliana mwelekeo ni upi. Ni muhimu kama Wabunge tukubaliane na tuone kuwa nchi hii na wananchi wanalindwa kulingana na mali ambayo tumejaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa nayo. Mara nyingi, inatumiwa na wageni na wananchi wenyewe hawafaidiki. Ukiangalia nchi nyingi za Kiafriaka hivi sasa, zina shida kwa sababu ya zile sheria ambazo ziko nazo, haswa kuhusu rasilmali zao. Mara nyingi, wanashikwa mateka na watu ambao wamekuja nchi zao kutafuta mali hiyo. ...
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, nashukuru kwa nafasi hii umenipatia nitoe mchango wangu kulingana na Ripoti hii ambayo tumepatiwa ili kueleza mwelekeo wa makadirio ambayo yatakuja mwaka wa 2016. Mwelekeo huu umepeanwa na Kamati ya Ratiba ambayo imeongozwa na Naibu Spika, Mhe. Laboso. La kushangaza ni kuwa wenyeviti wa Kamati hizi hivi wangekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanachangia kikamilifu kutetea Ripoti hii ili nasi tuwaunge mkono. Wakati mwingine mambo kama haya yanafadhaisha kwani ingekuwa bora zaidi wao wawe kipau mbele. Naomba niwapongeze kwa kazi hii njema ambayo wameifanya. Wakati mwingine jambo linaweza kutokea na ukaliona labda si la faida, lakini labda ile ...
view