3 Mar 2016 in National Assembly:
hazijakamilishwa zimekamilishwa na vipande vya ardhi ambavyo vina utata vimeratibiwa. Zaidi ya hivyo, tunafaa kuhakikisha kuwa majukumu ya Jopo hili yametimizwa kabla muda wao haujaisha. Nashukuru Kamati ya Ardhi kwa kuondoa yale mapendekezo ambayo walikuwa nayo ya kubadilisha fedha ambazo zilikuwa zimepatiwa kitengo hiki kwa sababu imebainika wazi kuwa mara nyingi, kitengo hiki kinanyimwa fedha ndio maana kinashindwa kutekeleza wajibu wake. Vile Mhe. Amina amesema alivyokuwa akichangia, naomba nimuunge mkono kwa dhati alivyosema kuwa katika nchi hii ya Kenya, madini yameanza kuleta faida na kuchangia katika kuzalisha fedha ambazo zinahitajika nchini. Lakini ni vizuri tuangalie fedha ambazo Wizara zinazohusika na ...
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, naomba wakati utaratibu utakuwa umeanza wa kuhakikisha kuwa makadirio ya fedha za mwaka 2016/2017, tuambiwe fedha hizo ziko wapi na tuambiwe zimefanya nini na kwa nini hazijatumiwa.
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Jambo lingine ambalo ningependa kuangazia ambalo limezungumziwa na wenzangu ni kuhusu fedha za wazee. Wazee wamelalamika. Tunasema tunaongeza hizi fedha lakini nikiangalia hapa, hazijaongezwa. Zimebanwa. Tunasema kuwa zitakuja kuongezwa mwaka mwingine. Ni nini kimetokea na hawa wazee wetu bado nao wamejitoa mhanga kuhakikisha kuwa taifa linakuwa? Wamejibidiisha vile wawezavyo kushikilia taifa lakini tukifika wakati wa kuhakikisha wamepata kitu angalau kabla maisha yao hayajafika kikomo, tunawanyima fedha.
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Ni ombi langu kuwa wakati makadirio yatakuwa yamefikishwa hapa, fedha ambazo zinahitajika ziwekwa ndani sawa sawa. Fedha za walimu zimewekwa kama fedheha. Kila mtu amepiga kelele kuhusu walimu. Wakati umefika katika nchi hii tuangalie haya makadirio kuwa yamewekwa sawa sawa na walimu wamepewa haki yao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Nimekubaliana na wewe. Umesema kuwa katika orodha yetu ya leo, Orodha No.13, tunatakiwa tuangalie sheria hii ambayo inatupatia viwango na vipimo ambavyo hatuwezi kupitisha.
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, ombi la Mhe. Junet ni la muhimu. Ni vyema tumalize mjadala huu kwa sababu muda wake ni leo. Kama mnaomba niweke tamati ili wenzangu wapate nafasi, ni radhi niweke tamati.
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Kwa haya mengi, naunga mkono.
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa muda huu ambao umenitunukia niweze kutoa mchango wangu kuhusu Mswada huu wa Ardhi ya Wenyeji . Kama tunavyojua wenyeji ni watu ambao wamekuwa mahali tangu miaka iliyopita na ardhi ambayo wanaikalia kulingana na vitengo vya sheria ni yao. Shida iliyopo ni kuwa mpaka sasa tangu tupate Uhuru, ardhi hiyo imechukuliwa kiholela. Mtu yeyote ako huru kwenda kuikalia vile anayvotaka. Mapendekezo ya sheria hii inasema kuwa sheria hii ikipitishwa, ile ardhi ya wenyeji, wale watu wameenda wakakaa pahali hapo, wakijikusanya wawe kama kitengo kimoja, wanaweza kupatiwa hiyo ardhi iwe yao. Wakati umefika watu waheshimiane ...
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Ama la sivyo ardhi kama hizi zinaweza kutumika vibaya hasa wakati huu wa kisiasa. Watu watoke sehemu zingine waje wapewe vipande vya ardhi na wale wamekaa sehemu hizo kwa miaka nenda miaka rudi wakanyimwa ardhi. Nikisema hivi haimaanishi watu hawatakubaliwa waende kukaa kwa ardhi. La! Tunasema watu waangaliwe vile watakavyo kaa katika ardhi zao. Watu waangaliwe vile wale wamekaa katika ardhi watafaidishwa na hivyo vipande vya ardhi. Tumeona dhuluma zimetendewa watu katika vipande vya ardhi ambavyo vilikuwa vyao. Tukiangalia kama sehemu ya Kaloleni Voi, ni jambo la aibu kuona vile mambo yako. Sheria hii ingekuwa imepitishwa hapo awali watu wa ...
view
3 Mar 2016 in National Assembly:
Hivi ilivyo, wale ambao wanaongoza kaunti wanaweza kuamka asubuhi wakasema: “Hapo tumeamua sehemu hiyo ya ardhi inachukuliwa na inafanyiwa hivi na vile” na wenyewe hawana habari wala fahamu. Hawajaulizwa ama kuombwa. Mara nyingi unakuta sheria hii tukiangalia vipengele kadha wa kadha, na tumevichunguza, moja ya matatizo ya sheria hii nikuhusu dhuluma ambazo zimetendwa hapo awali. Kwa kizungu zinaitwa historical landinjustices. Tunaomba Mswada huu upitishwe na marekebisho, maanake kuna marekebisho ambayo tunahitaji kuyaleta, ili wale watu ambao wamedhulumiwa kwa ardhi zao wapate haki. Ile dhuluma nazungumzia ni dhuluma kama ile imefanyiwa watu wa Taita Taveta; ardhi yao ikachukuliwa ikafanywa mbuga za ...
view