23 Feb 2016 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Ninaona Mwenyekiti ana wasiwasi. Nilikuwa nikitafuta tafsiri ya Kiswahili ya Ripoti hii lakini ninashukuru, imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Nitachukua nafasi hii kuwatafsiria wale ambao labda lugha ya kimombo inawaletea shida. Tumeisoma na kuielewa Ripoti hii. Ninaomba nichukue nafasi hii kuwapongeza Wanachama wa Kamati husika. Hii inaonyesha wazi kwamba ukichukua fimbo na kuwachapa watu fulani, wanaamka. Tulipomwambia Mwenyekiti hapa kwamba wanazembea katika kazi yao, walifanya bidii na kuhakikisha kwamba ripoti hizi zimeletwa Bungeni na hivi sasa zinashughulikiwa.
view
23 Feb 2016 in National Assembly:
Ninaomba ripoti kama hizi zinapofika Bungeni na kujadiliwa, Kamati Tekelezi – ambayo inahitajika kutekeleza maamuzi ya Bunge – iyatekeleze maamuzi hayo. Sioni maamuzi ya Bunge yakitekelezwa. Ninasema hivi kwa sababu niko na ushahidi kuhusu ripoti nyingi ambazo zimepitishwa na Bunge hili lakini mpaka sasa hakuna pendekezo lolote ambalo limetekelezwa. Kamati ambayo inahusika na masuala ya sukari imetueleza na kufafanua jinsi hali ilivyo duni katika sekta ya sukari humu nchini. Tunasubiri tuone iwapo Kamati Tekelezi itafuata maagizo ya Bunge, ambayo yameandaliwa na kila mtu ameyasoma na kuyatilia maanani ili tuyafuatilie.
view
23 Feb 2016 in National Assembly:
La muhimu ni kwamba sukari inatumika kwa njia ya kawaida na takriban watu wote humu nchini. Tukiwa na upungufu wa sukari, utasikia kelele kutoka pembe zote za nchini hii. Tukiwa na mapendekezo yanayoweza kuiboresha sekta ya sukari nchini, ni bora kuyatoa. Inastaajabisha kwamba hata fedha zikitengewa shughuli ya kuboresha viwanda vya sukari, punde tu zinapowasili kwenye kampuni husika, pesa hizo hupotea. Kampuni ambayo ilikuwa maarufu wakati nilipokuwa chuoni na wakati nilipoanza kufanya kazi ni kampuni ya Sukari ya Mumias. Kampuni hiyo ilikuwa imebobea enzi hizo; kila mtu alikuwa akiisifu. Hivi leo kila mtu anastaajabu ni kitu gani kimetokea katika kampuni ...
view
23 Feb 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, utakumbuka kwamba humu nchini kulikuwa na viwanda vya makonge, bixa, korosho na nyama, miongoni mwa viwanda vingine, ambavyo hivi sasa haviko. Kwani nchi yetu ina nini? Aidha tunaanzisha viwanda tukiwa na nia ya kuvipora baadaye ama utendakazi wetu ni hafifu. Wakati umefika wa kujiuliza: “Jamani, tunaenda wapi Wakenya, na ni kitu gani tunachohitaji kufanya ili tuiboreshe hali hii?”
view
23 Feb 2016 in National Assembly:
Katika sehemu ya magharibi ya nchi, wananchi wengi wanategemea sukari katika maisha yao ya kila siku. Wakulima hupanda miwa ambayo wanaitegemea kuwaelimisha watoto wao na kupata ajira zinazowawezesha kulea familia zao. Ni kitu gani kimetokea hivi sasa? Hivi sasa, watu wamefadhaika na kukata tamaa. Hawana mbele wala nyuma kwa sababu ya mambo ambayo tumeyaona kwenye Ripoti hii. Ripoti hii imeeleza kwamba kuna ufisadi wa hali ya juu katika sekta ya sukari humu nchini. Kuna masuala ambayo hayajatekelezwa vizuri. Mara nyingi Serikali huleta kampuni kutoka nje kusimamia utendakazi katika viwanda vyetu vya sukari lakini punde wasimamizi wa kampuni hizo wanapowasili humu ...
view
23 Feb 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, kwa sababu tumeisoma Ripoti hii na kuielewa, ninaiomba Kamati Tekelezi ya Bunge iyafuatilie mapendekezo yote kwa uangalifu angalau tuweza kugeuza sura ya sekta ya sukari na kuihifadhi.
view
23 Feb 2016 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninaunga mkono Ripoti hii.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaomba nimuulize mwenzagu wa upande ule mwingine, Mheshimiwa Chepkong’a, kama kweli ana uwezo na mamlaka ya kuachia mtu mwingine nafasi yake ya uanachama kwenye kamati ya Bunge. Uwezo huo ameutoa wapi? Hana uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu huo uwezo uko Bungeni. Kwa hivyo, asijitwike mamlaka ambayo hana. Amejibandikia mamlaka ambayo si yake. Watu hao wanaitwa, kwa lugha ya mtaani, wezi. Hawezi wala hana huo uwezo na hatakuwa na huo uwezo kwa sababu uwezo huo ni wa Bunge hili.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nikiunga mkono Hoja hii ya kawaida, ninaomba nichukue nafasi hii kufafanua mawili au matatu. Hoja hizi zinaletwa wakati Kamati mbili za Bunge zimeshikana ili kutoa mchango wao kwa jambo lo lote ambalo limeletwa Bungeni. Ripoti hiyo ikiletwa Bungeni, ni muhimu kila Mbunge apatiwe nafasi ya kutoa mchango wake kwa Hoja hiyo.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Hii ndio maana Kiongozi wa walio wengi Bungeni anapendekeza kuwa yule ambaye ameleta Hoja apatiwe dakika sitini na Wabunge wengine wapatiwe dakika kumi kutoa michango yao kwa Hoja hii. Ninaomba pia ieleweke kuwa litakuwa jambo ambalo limekwisha changiwa katika Kamati za Bunge na Wabunge wakatoa maoni na mapendekezo yao na lile ambalo litaletwa hapa Bungeni ni jambo ambalo lishakubalika. Hapo ndipo Wabunge watapata nafasi ama ruhusa ya kulichangia na kuweka msimamo kuhusu jambo hilo.
view