10 Feb 2016 in National Assembly:
Nikimalizia, kuna jambo ambalo ninaona linataka kuenezwa hapa ambalo si sahihi. Inaonekana kuwa labda tunataka kufurusha wenzetu upande huu wakimbie upande ule mwingine ama tunawaadhibu. Ninaomba ikubalike wazi kuwa wengi wetu ambao tuko hapa, mbali na wale wachache ambao walikuja Bungeni na tiketi za ubinafsi, tumeletwa na tiketi ya chama. Kabla ya kuingia Bungeni, wengi waliweka sahihi wakikubali masharti ya chama.
view
10 Feb 2016 in National Assembly:
Ninashukuru, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Umeamua na usawa. Ninaomba ieleweke kuwa kama umefuata sheria, zifuate mpaka mwisho. Sheria zetu za Bunge zinampatia Kiranja wa Bunge nafasi kama ameagizwa na chama chake kuomuondoa mtu mmoja kutoka kamati. Isije ikawa kuna watu ambao wanataka kupeana adhabu. Ninaunga mkono Hoja hii bila tatizo lo lote.
view
9 Feb 2016 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika. Naomba niunge mwenzangu mkono. Jambo la kwanza, ningependa kuwatakia Wabunge wote wakati mwema kwa kikao hiki na kuwatakia mema wakati huu wote tutakapokuwa tukizungumza ama kujadiliana Bungeni.
view
9 Feb 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, naomba niunge Hoja hii mkono kwani Kamati hii ya Bunge, ni kamati muhimu inayotoa mipangilio yote ya Bunge na kuhakikisha kuwa shughuli za Bunge zinaendelezwa vilivyo. Ukiangalia orodha hii, tumeangalia kwa utaratibu tuone kama kuna wengine ambao hawashughuliki sana na shughuli za Bunge na wengine wakaamua kuwa hawangependelea kuendelea katika hivi vikao kwa sababu kila siku ya Jumanne wakati shughuli za Bunge zimemalizika, lazima Kamati hii iende ikutane na ijadiliane. Unakuta wakati mwingine, wanakamati wengine ambao wako katika orodha hii ama walikua katika orodha ya awali, hawakuwa wakishughulika na mambo ya Kamati. Hapo ndipo ilipobainika wazi kuwa itakua ...
view
9 Feb 2016 in National Assembly:
Mhe. Spika, nikimalizia, la muhimu ni kuwa Wabunge waelewe kuwa bado kuna kamati zingine ambazo lazima zifanyiwe marekebisho kama itahitajika. Ni muhimu kuwa wakati huu, tuangazie umuhimu wa kamati za Bunge. Kuna Wabunge ambao sitawataja majina hapa, ambao wamepewa nafasi za kuhudumu katika kamati na hawajahudhuria mkutano hata mmoja.
view
9 Feb 2016 in National Assembly:
Nikipewa muda nitakuja na orodha niwaseme. Hata wale wanaosema na waseme - inajulikana wazi kuwa sheria zetu zinasema kama mwanakamati hajaudhuria vikao vitatu, aondolewe katika kamati hiyo. Wakati umefika Waheshimiwa, tuchukue majukumu yetu sawasawa na sahihi. Kila mtu ashughulike na shughuli za Bunge. Kama umeingia kwa kamati, ni muhimu na ni lazima ushughulike. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
9 Feb 2016 in National Assembly:
Kwa hayo mengi, Mhe.Spika, naunga mkono.
view
17 Dec 2015 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, ninampongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuona kwamba hawa ndugu zetu wawili, Charles Sunkuli na Dkt. Margaret Mwakima, wanafaa kuhudumu katika Serikali yake. Kamati yetu pia imewapiga msasa na tukaona kwamba wanafaa. Mimi ninaomba niunge mkono uamuzi na uteuzi huu ili hawa ndugu zetu wawili waingie kwenye Serikali. Bila shaka, wataboresha shuguli za Serikali na kujaza pengo pale ambapo kumeonekana kuna upungufu. Hawa wote wanatoko kwenye sehemu ambazo zinaangalia mazingara na mali ya asili. Bw. Sunkuli, akiwa anatoka sehemu za Narok; na Bi. Mwakima, akiwa anatoka sehemu yangu ya Taita, ...
view
17 Dec 2015 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami nitoe maoni yangu kuhusu uteuzi wa Daktari Muraguri. Dunia hii ni duara na rangi rangile. Naomba nikimuunga mkono huyo daktari, wakumbuke waliyonitendea wakati tulipewa fedha – Shilingi milioni mia moja katika hospitali ya Wesu Taita. Mhe. Spika, wamenizungusha huku na kule wakiniambia nilete orodha ya vifaa na mashine ambazo nahitaji. Niliwakabidhi lakini mpaka leo, Dr. Muraguri na wenzake wameshindwa kueleza vile walivyotumia fedha hizo na vifaa walivipeleka wapi. Hayo yalifanyika katika Bunge la Kumi. Ni ombi langu kwa sababu amepewa nafasi ya kuchukua wadhifa wa kuendesha Wizara ya Afya. Kwa yale ...
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Naibu wa Spika. Ninaomba nami nitoe mchango wangu kwa Mswada huu ambao uko Bungeni leo. Tukubaliane kwamba misitu ni moja ya raslimali za nchi hii, ambazo zinahitaji kulindwa na kuhifadhiwa. Mutakubaliana nami kwamba nchi ya Kenya imepiga hatua kubwa ya kuridhisha katika jitihada za kuhifadhi misitu. Ijapokuwa Mswada huu unaangazia changamoto ambazo zitakuwepo, ni muhimu tuangazie matatizo ambayo yapo katika uhifadhi wa misitu yetu nchini Kenya. Wakenya kwa ujumla ni watu ambao wanapenda miti na wanapenda kuhifadhi mazingira lakini mara nyingi wanavunjwa moyo na wale ambao wamepatiwa majukumu ya kuangalia na kutunza misitu yetu. Naomba kwa ufupi tu ...
view