16 Dec 2015 in National Assembly:
litapatikana kama exhibit. Maofisa wa Serikali wanachukua hayo mengine na kuyatumia. Utakuta kwamba wao wenyewe ndio wanaendeleza hii biashara ya makaa kinyume na sheria. Ni ombi langu kwamba wakati huu tunahitaji kuhifadhi misitu. Tunataka kuhakikisha kuwa misitu imehifadhiwa. Kuna mpangilio mwafaka umewekwa kuhakikisha kuwa wale ambao wanashughulikia misitu wanafaidi kutoka hiyo misitu. Wale watu ambao wameamua kupanda na kuhifadhi miti binafsi, wataruhusiwa kupanda. Wakati wa kuivuna pia wapatiwe mpangilio vile wataivuna. La sivyo, tukiendelea hivi, utakuta hii nchi yetu imekuwa janga, ukame umeingia na hakuna chochote nchi hii itaweza kufaidi. Langu ni kuomba Wabunge wenzangu tuupitishe Mswada hii lakini tuangalie ...
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Asante Mhe. Spika. Ninaomba nitoe mchango wangu kwa ndugu zangu hawa ambao wamepewa nafasi na Rais ili watumikie nchi hii kama Makatibu Wakuu wa wizara mbali mbali.
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Kwanza, wakati walikuwa wanapigwa msasa, hawa ndugu zetu Wakenya wameonyosha kisomo ambacho kinafaa, sifa ambazo zinastahili na maadili wanayo ambayo yanahitajika kulingana na Katiba. Kwa hivyo, wamejitoa mhanga watumikie nchi hii. Ni muhimu hawa ndugu zetu watatu ambao wamechaguliwa kuwa Makatibu Wakuu wawajibike. Wasipowajibika watakuwa wanajinufaisha wao wenyewe. Na vile tunavyona nchi inavyoendelea, imekumbwa na mambo mengi ambayo yanahitaji ustadi muhimu sana wa kazi. Inabainika wazi wazi kuwa hawa ndugu zetu watatu wana uzoefu wa kutosha katika nyadhifa mbali mbali ambazo walikuwa wameshikilia kabla ya kuteuliwa kuchukua nafasi hii. Lakini hata hivyo lazima hawa Makatibu waangazie na waangalie wasije wakatumbukia ...
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mhe Spika.
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Kwanza, ningependa kuwapongeza wote walioteuliwa. Ninaomba nisisitize kuwa uteuzi huo bado haujaonyesha sura ya nchi. Tunaomba sura ya nchi itolewe na iononekane kwenye uteuzi kama huu. Mkuki ni mtamu kwa nguruwe na chungu kwa binadamu.
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, ninawaunga mkono wote walioteuliwa kwa sababu wana sifa na wanaweza kazi wanazopewa. Wao hawana shida bali mteuzi yule ambaye aliwateua ndiye ninataka aangazie uso wa Kenya. Lakini wale walioteuliwa, ninawapongeza na kuwatakia kila la heri.
view
16 Dec 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, ninaounga mkono.
view
24 Nov 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili niwafahamishe Wabunge wenzangu kuhusu ziara ya Baba Mtakatifu ambaye atakuwa humu nchini kuanzia kesho. Wabunge waheshimiwa, mpangilio ambao umewekwa---
view
24 Nov 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, kama kuna masahihisho yoyote ambayo yanahitajika, ni jambo la kawaida watu kusahihishana. Ninaomba niwafahamishe Wabunge kuwa Baba Mtakatifu atawasili kesho. Wabunge wamealikwa na Serikali waende Ikulu kesho wawe pamoja na Rais akimpokea na kumkaribisha Baba Mtakatifu katika Ikulu hapo kesho. Kila Mbunge amepatiwa cheti cha mwaliko. Iwapa kuna Mbunge ambaye hajakipata cheti hicho, ninamshauri aende kule sebuleni akakichukue. Pia, kuna pasi ya gari. Hapo awali tulifikiria tutapata basi ili tuende pamoja lakini imeamuliwa kuwa kila Mbunge yuko huru The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can ...
view
24 Nov 2015 in National Assembly:
kutumia usafiri wake binafsi mradi tu aweke kibandiko ambacho kinamruhusu kuingia huko Ikulu. Munaelewa kwamba mpangilio huo umezingatia masuala ya usalama. La pili, kuna ibada ya misa siku ya Alhamisi kuanzia saa kumi---
view