Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 604.

  • 29 Mar 2017 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nitoe sauti yangu kwa haya machache ambayo yamejiri hapa katika ukumbi huu. Nakubaliana na wenzangu kuwa ni muhimu Wabunge wasome na waelewe hizi sheria ambazo tunataka kuzipitisha kwa sababu nyingi zao, wasipozisoma, zitawaadhiri hao waliopo hapa na wengine wanaokuja. Mara nyingi, huwa tunakutwa na hizi sheria tukiwa tumetoka Bungeni na sisi wenyewe hatujazisoma. Hata hivyo, si jambo la kuchukulia kiholela kuwa tunaleta sheria Bungeni za kuangalia uchaguzi utakuwa wa aina gani halafu Wabunge wenyewe wawe hawajazisoma, hawajazielewa wala hawazitambui. Wanaenda kuleta zogo huko mtaani baada ya kutoka hapa. Vile ... view
  • 14 Feb 2017 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Spika. Naomba nichukue nafasi hii kwa niaba yangu na watu wangu wa Wundanyi ambao ninawawakilisha kutoa rambirambi zetu kwa familia ya mwenda zake Mheshimiwa Seneta Juma Boy ambaye aliaga dunia hapo mwisho wa wiki na alizikwa jana. Naomba tukubaliane na wenzangu kuwa Seneta Juma Boy hakuwa Mheshimiwa hivi hivi. Yeye alikuwa amejisitiri sana katika shughuli zake na utendaji kazi wake. view
  • 14 Feb 2017 in National Assembly: Alikuwa ni mmoja wa maseneta nchini ambaye alikuwa anategemewa na kuaminiwa sana kwa utendaji kazi wake. Tukubaliane kuwa wakati huu kuna msiba kwa familia yake, familia nyinginezo na Kenya kwa jumla kwa kumpoteza Seneta wetu. Mheshimiwa Spika naomba nitoe rambirambi kwa nchi yote nzima kwa kumpoteza Seneta Boy. view
  • 14 Feb 2017 in National Assembly: Wenzangu Wabunge, naomba tujiunge pamoja wakati huu mzito wa majonzi ili kuona vile tutaweza kusitiri familia yake Seneta Boy wakati huu wa msiba. Mheshimiwa Spika, Juma Boy alikuwa amejitoa mhanga kutumikia nchi hii na ni wazi kuwa alitekeleza wajibu wake bila ubaguzi. view
  • 14 Feb 2017 in National Assembly: Naomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Ahsante Mheshimiwa Spika. view
  • 31 Jan 2017 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Naomba nimpongeze Mhe. Sara kwa kuleta malalamishi haya ya bararbara Bungeni. Ijapokua, Mhe. Sara naomba nikufahamishe kuwa suala hili la barabara linaadhiri kila Mbunge aliyeko hapa. Tukianzia na mimi, katika sehemu ya Bunge ninayowakilisha ya Wundanyi, tuko na kilomita moja ya lami. Tangu ilimwe na wafungwa wa Kiitaliano katika Vita vya Pili vya Ulimwengu, hatujawahi kupata lami mpaka siku ya leo. view
  • 31 Jan 2017 in National Assembly: Ni jambo la aibu hata Wabunge wenzangu wakitembelea eneo langu la Bunge, kutoka Bura kwenda Mgange, Mgange Mwanda, Mgange Weruga, Weruga Wundanyi hadi Mbale na Msau na huko Mgambonyi. Barabara imekuwa kama makaburi. Gari haliwezi kupita. Mtu akija na gari lake ndogo, linakwama hapo. Hundi sawanisha ambayo tunapatiwa - kwa Mhe. Mburi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 31 Jan 2017 in National Assembly: ambaye haelewi hundi sawanisha ni nini, nimueleze kuwa ni Equalisation Fund. Hundi sawanisha imebidi ndiyo tutaitumia kurekebisha barabara zetu. view
  • 31 Jan 2017 in National Assembly: Ni jambo la kuudhi. Tunaomba Kamati ya Bunge ambayo inahusika na ujenzi na urekebishaji wa barabara iangalie hizi barabara kwa kila sehemu ya uwakilishi Bungeni hapa. Kila mmoja wetu analilia upande wake angalau watu wake wapate nafasi ya kuanza kuwasiliana, kutembeleana na kufanya shughuli zao kama kubeba mboga, matunda, mizigo na maziwa. Lakini kama hamna barabara, tunatarajiaje nchi hii ipate kuendelea? view
  • 31 Jan 2017 in National Assembly: Suala nyeti ni kuwa hizi hela ambazo tulikubaliana zitumike kutengeneza barabara kilomita elfu kumi ziko wapi? Ni nini kimetokea? Ni lipi limeenda vibaya? Ule wakati ambao tulikuwa tumepitisha sheria hapa kuwa kuna barabara zitakuwa katika mikononi mwa Serikali kuu na zingine kwa Kaunti, ni nini kimetokea? Tunaambiwa kuwa magavana wengine wameweka sahihi barabara zitengenezwe na wengine wamekataa. Je, wale ambao wameweka sahihi barabara zitengenezwe, zimetengenezwa? Na wale ambao wamekataa, kama wangu wa Taita Taveta, barabara zetu hazijatengenezwa, ni nini kitakachotokea? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus