Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 604.

  • 31 Jan 2017 in National Assembly: Naomba Kamati ichukue jukumu hili ihakikishe kabla hatujapitisha Bajeti ya mwaka huu, ama makadirio ya pesa za mwaka huu, barabara zimerekebishwa na kila Mbunge apate nafasi ya kutengenezewa barabara. Ningependa Mhe. Naibu Spika, nikiwa gavana wa Taita Taveta na wewe ukiwa gavana wa Bomet, ule wakati unakuja Taita Taveta ama nikija Bomet, magari yetu yawe hayapati shida.. view
  • 31 Jan 2017 in National Assembly: Kwa haya mengi, naomba kuunga Ombi hili mkono. Ahsante. view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika. Ninaomba nichukue nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii na mwongozo ambao umewekwa bayana ili tupate kuelekezana vile tutakavyoweza kuwa na majadiliano hapa Bungeni. Wakati huu wa kupeana mwongozo wa majadiliano Bungeni, itakuwa vyema kama kila Mhe. atakayesimama kutoa maoni yake apewe muda tukianza na viongozi wa utawala Bungeni. Tutaangalia vile waheshimiwa watatoa maoni yao ili kila mmoja apatiwe nafasi ya kutoa maoni yake katika kila Mswada ambao utaletwa Bungeni. Mhe. Spika, ni jambo la kawaida kuwa mwongozo huu ukubalike na kila Mbunge ama Wabunge wengi ili tutoe utaratibu ambao utakubalika kwa kila mmoja wetu na kwa ... view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: Ahsante Mheshimiwa Spika kwa nafasi hii ambayo nimepewa ya kuunga mkono Ratiba ya Bunge na mpangilio ambao umewekwa waziwazi vile Bunge itakavyoendesha kazi zake. Naomba nichukue nafasi hii kuwatahadharisha Wabunge wenzangu. Mmekaa hapa karibu miaka minne na mpaka sasa hamjaelewa shughuli za Bunge. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: Mara nyingi nimeona Mheshimiwa Spika amesimama na naona Mbunge anatembea tembea ndani ya Bunge. Inamaanisha mpaka sasa hawajachukua nafasi ya kuelewa shughuli na mpangilio wa Bunge. Naomba wakati huu Mheshimiwa Spika hawa Wabunge ambao wamekaa hapa miaka minne na mpaka leo hawajaelewa--- Mmoja alikuwa anasimama mbele yangu wakati nilikuwa ninazungumza akikuzuia usinione. view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: Mhe. Spika, Mhe. Amina alikuwa anasema kuwa ninawatisha Wabunge. Naomba nirudie yale niliyoyasema hapo jana. Ninarudia Mhe. Amina, na si kwa ubaya vile ulivyokuwa umesisitiza kuwa tusitishie Wabunge. Theluthi themanini kulingana na stakabadhi na vile tunavyoelewa, wengine wenu hamtarudi hapa. view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: Kwa hivyo, tafadhali wakati umefika--- view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: Ni wakati wa lala salama. Wengine mnakunja majavi yenu kabisa, na wegine wanayakunja nusu na watarudi. Kwa hivyo, itategemea uko upande upi. Wengine wetu tumeamua kwa hiyari kwenda kuomba kiti cha ugavana. view
  • 25 Jan 2017 in National Assembly: Wale ambao mmeamua mnarudi hapa, wakati ndio huu ambao umebaki mchangie kikamilifu ule wajibu ambao mmepatiwa na umma kushughulika katika utungaji sheria na kuwajibika wakati wa ugawaji wa pesa. La sivyo, wengine wenu mtakuwa mnasema mmekaa hapa miaka minne lakina hakuna kitu chochote cha kuonyesha. Lakini wengi wamefanya kazi ya kuridhisha na ninawapongeza. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus