25 Jan 2017 in National Assembly:
Mhe. Spika, kazi ambayo imebaki ni nyingi. Kama tulivyoona leo, wakati huu utakuwa mgumu sana kwa viranja kwa sababu mara kwa mara Wabunge watakuwa huko mashinani wakiomba kura. Lakini tumetumia wakati huu vizuri kwa sababu tumejaribu tuwezavyo--- Ninawapongeza Wabunge wenzangu vile wametumia huu muda.
view
25 Jan 2017 in National Assembly:
Hata hivyo, kwa muda mfupi ambao umebaki itakuwa ni wajibu wa kila Mbunge kuhakikisha ameangalia wastani wa muda wake. Ni muda upi utatumia kwa shughuli za Bunge na ni upi utatumia kuangalia maslahi na miradi yako ambayo imebaki?
view
25 Jan 2017 in National Assembly:
Kwa haya machache, ninaomba kuunga mkono Hoja hii. Asante, Mhe. Spika.
view
24 Jan 2017 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Ningependa kuchukua nafasi hii kuunga mkono Hoja hii. Ningependa pia kuwatakia Wabunge wenzangu kila la heri muhula huu kwa sababu watakuwa wanakunja jamvi wakijiandaa kwa uchaguzi ambao utafanyika hapo mwakani.
view
24 Jan 2017 in National Assembly:
Tunakubaliana kwamba Bunge limejaribu kufanya lile ambalo lingeweza kufanya. Nina imani kuwa katika zile kazi ambazo zimebaki, Wabunge watajitolea kikamilifu kuhakikisha kuwa wameifuata ratiba yao, ambayo tutaizungumzia leo jioni ili waweze kukamilisha. Kama ilivyosemwa na mwenzangu, uongozi wa Bunge umeonelea kuwa haina haja kubadilisha viongozi ambao wanahudumu katika Kamati hii inayoshughulikia masuala ya Bunge. Tumeiacha vile vile ili iweze kuwajibika na kumaliza muhula huu ili tuendelee na kazi ambazo tumepatiwa za Bunge. Ninaomba nichukue wakati huu kuwaomba Wabunge wenzangu kuwa tujibidishe tuwezavyo ili tujumuike na wenzetu wakati huu wa kujiandikisha ili wakati wa kupiga kura utakapofika mwezi wa Agosti, kila ...
view
24 Jan 2017 in National Assembly:
Mhe Spika, ninaweka tamati kwa kusema kuwa kulingana na takwimu tulizo nazo Bungeni, asilimia 80 ya Wabunge huwa kawaida hawarudi. Kwa hivyo wengine watakuwa wanakunja jamvi lao wakiwa wanaondoka na kuaga Bunge. Mimi ni mmoja wa Wabunge ambao watakuwa wanakunja jamvi lao kama Mbunge wa Wundanyi maana nitakuwa ninaomba kiti cha ugavana katika Kaunti ya Taita Taveta. Kwa hivyo, wenzangu ninawaaga polepole wakati huu ambao nimewatumikia. Kwa muhtasari, ninawatakia Wabunge kila la heri katika kazi yao. Kwa heshima na taadhima kumbwa, ninawaomba Wabunge waunge mkono majina haya ili tuendelee na kazi. The electronic version of the Official Hansard Report is ...
view
24 Jan 2017 in National Assembly:
Kwa haya mengi, ninaomba kuunga mkono majina haya ili yaratibiwe na Bunge na tuendelee na kazi. Asante, Mhe. Spika.
view
17 Jan 2017 in National Assembly:
Asante Mheshimiwa Spika kwa mjadala huu asubuhi hii na kwa kunipatia nafasi niuunge mkono. Tukiunga mkono mjadala huu, ni muhimu tukubaliane sote Wabunge kuwa tumeitwa kwa Kikao Maalum kuangalia Hoja ambazo ziko mbele yetu. Hoja ni kuangalia waliopendekezwa kuwa Mwenyekiti anayeangalia shirika linalohusika na ufisadi na hao ambao watakuwa wakiangalia mambo ya usajili na mipaka ili tuhakikishe kuwa upigaji kura utahalalishwa, na wenyewe ni watu ambao wamehalalishwa na Bunge. Hii ndio maana tumeitwa tuje Bungeni siku hii ya leo kwa Kikao Maalum. Tumeangalia yale masaa na muda ambao unaombwa Wabunge wauchukue kwa mjadala wa kwanza kuanzia 2.30 p.m. hadi 4.30 ...
view
17 Jan 2017 in National Assembly:
Nashukuru Mheshimiwa Spika kwa nafasi hii ambayo umenipatia nami nitoe mchango wangu kuhusu hawa ndugu na dada zetu ambao wamependekezwa ili wapewe kibali na Rais tukianzia na Bunge ili nao waingie kazini na kuwapa Wakenya matumaini ya kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki maana hivi sasa hatuna Tume nzuri. Tunataka kina Hassan waondoke na ni muhimu sisi kama Bunge tumalize zoezi hili ili tuwape Wakenya kwa ujumla nafasi ya kupiga kura ifikapo August. Nikiangalia orodha ile ambayo tumepatiwa hapa Bungeni kuanzia Mwenyekiti na wenzake, naona kuna usawa ambao umependekezwa kati ya wanawake na wanaume ili tufuate vile Katiba inavyosema. ...
view
17 Jan 2017 in National Assembly:
Nashukuru Mheshimiwa Spika kwa nafasi hii ambayo umenipatia nami nitoe mchango wangu kuhusu hawa ndugu na dada zetu ambao wamependekezwa ili wapewe kibali na Rais tukianzia na Bunge ili nao waingie kazini na kuwapa Wakenya matumaini ya kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki maana hivi sasa hatuna Tume nzuri. Tunataka kina Hassan waondoke na ni muhimu sisi kama Bunge tumalize zoezi hili ili tuwape Wakenya kwa ujumla nafasi ya kupiga kura ifikapo August. Nikiangalia orodha ile ambayo tumepatiwa hapa Bungeni kuanzia Mwenyekiti na wenzake, naona kuna usawa ambao umependekezwa kati ya wanawake na wanaume ili tufuate vile Katiba inavyosema. ...
view