Thomas Mwadeghu

Full name

Thomas Ludindi Mwadeghu

Born

1953

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

wundanyiconstituency@yahoo.com

Email

Wundanyi@parliament.go.ke

Telephone

0724-285347

All parliamentary appearances

Entries 71 to 80 of 604.

  • 17 Jan 2017 in National Assembly: Katika hao wote ambao wamependekezwa, naomba niwe wazi kuwa wawili wao ni watu ninawafahamu sana. Nitaanza na Wanjala. Yeye ni binti anayetoka Taita ijapokuwa ni mzaliwa wa Kwale. Babake ametoka Sungululu katika Wilaya yangu pale ambapo mimi mwenyewe nawakilisha kule Wundanyi, akahamia Kwale na bintiye akazaliwa lakini amerudi huko Taita. Ni binti ambaye namfahamu na ana uadilifu wa kutosha kwa hivyo hapo sina wasiwasi. Nina imani kuwa atatekeleza wajibu wake na atafanya kazi na imani sawa. Nikiangalia huyu mwingine ambaye watu wanaanza kushangaa ni nani ni dada yetu Consolata Nkatha Bucha Maina. Nimemfahamu akiwa mwanafunzi miaka themanini nikiwa wakati huo ... view
  • 17 Jan 2017 in National Assembly: Katika hao wote ambao wamependekezwa, naomba niwe wazi kuwa wawili wao ni watu ninawafahamu sana. Nitaanza na Wanjala. Yeye ni binti anayetoka Taita ijapokuwa ni mzaliwa wa Kwale. Babake ametoka Sungululu katika Wilaya yangu pale ambapo mimi mwenyewe nawakilisha kule Wundanyi, akahamia Kwale na bintiye akazaliwa lakini amerudi huko Taita. Ni binti ambaye namfahamu na ana uadilifu wa kutosha kwa hivyo hapo sina wasiwasi. Nina imani kuwa atatekeleza wajibu wake na atafanya kazi na imani sawa. Nikiangalia huyu mwingine ambaye watu wanaanza kushangaa ni nani ni dada yetu Consolata Nkatha Bucha Maina. Nimemfahamu akiwa mwanafunzi miaka themanini nikiwa wakati huo ... view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: Mhe. Spika, ninashukuru kwa muda huu ambao umenitunukia nijibu mawili matatu ambayo yameletwa na Kiongozi wa Walio Wengi Bungeni. Ninamheshimu na nitaendelea kumheshimu. Lakini, haimaanishi kuwa ana majukumu ya kutuambia msimamo wetu utakuwa upi kulingana na muongozo wa nchi. view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: Wakati umefika Mhe. Duale aambiwe wazi wazi kwamba hatakuwa akipeleka ubabe wake kila pahali. Pia, wakati umefika Duale aambiwe wazi wazi kuwa ana uhuru wake wa kueleza na kutoa maoni kuhusu msimamo wake, lakini msimamo wake hauwezi kuwa sawa na wetu. Msimamo wake ni wake na wetu ni wetu. Kitu ambacho tumesema ni kwamba hatuna haja ya uchaguzi wa ugomvi. La! Tunataka amani. Kama kuna watu wanahitaji amani ni sisi. Tunataka uchaguzi wa amani. Haimaanishi tunataka kuchangia uchafu ama machafu nchini tukiamua hatutashiriki katika zoezi lolote. Katika kila kongamano na kila upande wa siasa, kuna majadiliano. Watu huzungumziana, wakaelezana na ... view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: anasimama kusema: “Nimeambiwa yawe haya na haya.” Tunakubaliana na muongozo wake. Kwa hivyo, hana mamlaka yoyote ya kutuelekeza. La pili, ninaomba niweke bayana kwmaba ni kweli wala sitaki kukana kuwa nimetuma huo ujumbe. Nimeuzungusha lakini sikukaa nikautunga. Bila shaka, tumekaa tukajadiliana, nikatoa muelekeo na nikaupeleka. Umesikia Mhe. Midiwo akisema yeye hajapata huo ujumbe. Kwa hivyo, maadamu ameamua anaenda Mombasa, anaenda. Hakuna yeyote ameambiwa asiende Mombasa. view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: Sheria za Bunge zinasema niko na uhuru wa kuzungumza lugha ya Kiswahila ama ya Kizungu. Nimeamua nizungumze kwa lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha yangu na ninaielewa. Wala ninyi wa upande ule msifikiri kuwa Kizungu sikiwezi. Kizungu ninakiweza lakini nimeamua nitumie Kiswahili. Sasa, kitu kinachowawasha ni nini? Mnawashwa na nini? Pilipili usiyoila yakuwashiani? Wachana nayo! Wachana nayo, whether umeelewa--- Kama uko hapa Bungeni, unatakiwa uwe unajua Kiswahili. Wewe ni Mkenya na huelewi Kiswahili. Ni Mkenya wa aina gani ambaye haelewi Kiswahili? Jamani, ninaomba nijieleze na nijifahamishe. view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: Tumesema, kwa maoni yetu, kongamano hili, si eti tumelipuuza. Ninaomba tuelewane; hatukulipuuza. Tunasema kwamba wakati huu ambapo kuna mambo mengi ambayo yanatokea, hatuoni kama hilo kongamano, vile limekuja, litakuwa na maslahi tulivyokuwa tunatarajia. Kama mheshimiwa mwenzangu alivyoeleza, kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanatukera, na yanakumba nchi hivi sasa. Mambo ya ufisadi yametukera. Yako ndani. Tunauliza kwa nini tusiwe tunazungumzia mambo hayo kwanza ndio twende kwa kongamano hilo? Nchi inataka kuzama. Sio CORD inataka kuzamisha nchi. Ni upande huu mwingine wa Jubilee unataka kuzamisha nchi. Na nini? Na wizi. Sasa mnataka mfanye wizi, na mnataka mtuhusishe ndani. Tumekataa na tutaendelea ... view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: Ninazungumza Kiswahili, lugha ambayo unatakiwa uelewe hata kama wewe ni mbabe wa kivita. Hata kama wewe ni mbabe wa kivita, ninaomba mnielewe na ninaomba mnisikize kwa sababu huu ni wakati wangu. Mara nyingi mmenichukulia kwa kero kuwa Mwadeghu ni mpole na mnaweza kumsukuma Mwadeghu mpaka hapa. Hamjui Mwadeghu yule mnazungumza naye. Leo utajua kuwa mimi ninaweza kuwa mbabe. Ninaomba niseme haya. Wacha niwapashe na niwapashe sawasawa maana mna uzoefu mbaya. Mna uzoefu wa kuona kuwa mnaweza kutusukuma--- view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: Mhe. Spika, ninakubali muongozo wako na ninaomba nimaliza kwa kuwaomba wenzetu tuelewane. Msichukue ujumbe wetu vibaya. Ninaomba muelewe ujumbe wetu vizuri kuwa kongamano hili ambalo ni la Bunge hatukulidharau wala hatujalidharau. Kongamano hili la Bunge ni la muhimu wala hatukusema halina umuhimu. Kitu tunasema ni kuwa wakati huu ambao kuna mambo mengi ambayo yanakumba nchi hii, kwa maoni yetu, tumeona si vizuri, upande wetu, kushiriki kikamilifu kwa wakati huu. Lakini, haimanishi mtu akitaka kwenda atafungiwa. Ndio maana Mhe. Midiwo amesema yeye ataelekea. Lakini, ninaomba tuheshimiane. Kama upande wetu umeonelea ndio hivyo, basi, uwachwe ufikirie uone kwa nini umeonelea hivyo. Kwa ... view
  • 1 Dec 2016 in National Assembly: On a point of order, Hon. Deputy Speaker. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus