1 Dec 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, Mhe. wa Kiharu anataka kupotosha Bunge. Ukija katika kaunti yetu ya Taita Taveta utapata watu wanapata fedha kwa kuhifadhi miti. Kwa hivyo, kutojua kwake na kutoelewa kwake kusije kukajumuishwa kuwa nchi yote ya Kenya haina ufahamu kama yeye. Ninaomba Mhe. wa Kiharu asipotoshe Bunge kwa kutojua yaliyoko nchini.
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nami nitoe mchango wangu kwa Hoja hii inayohusu Ripoti ya Kamati ya Mazingira. Ninaomba niseme kwamba ninaunga mkono Ripoti hii ya kuhalalisha Mkataba wa Paris. Ni jambo la kufadhaisha kusema kuwa mageuzi ya hali ya anga hayatuhusu watu wa Kenya. Maguezi yoyote ya hali ya anga yanatuhusu Wakenya kwa kuwa hata hivi sasa tukiangalia vile mambo yanaendelea na vile mvua inavyonyesha, tutaona kwamba hainyeshi kama hapo awali kwa sababu kuna mageuzi ya hali ya anga. Ni jambo la kufadhaisha kuona kuwa wakati mwingine hata sisi Wabunge husimama na kusema ...
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Inafadhaisha kwamba hata Serikali yetu wakati mwingine haihusiki kikamilifu. Kwa mfano, uwajibikaji uliokuwepo wa upanzi wa miti haupo tena. Umeachwa. Huko ninakotoka, Taita, utakuta misitu inakatwa kiholela. Watu wanaohusika wakiulizwa wanasema wanakata kidogo tu. Serikali, hata kupitia kwa maofisa wake wakuu, haitaki kushtumu ukataji miti katika sehemu nyingine. Kwa sasa, ninazungumzia juu ya Taita. Jambo la kuaibisha ni kwamba mkuu wa kitengo hicho cha misitu ni mtu wa kutoka nyumbani lakini analinda wale maofisa ambao wanahusika na ukataji miti. Ninaomba nichukue nafasi hii kulaani vitendo kama hivyo. Ipo miradi ambayo inafanywa ambayo inaenda kinyume na utunzaji wa hali ya anga. ...
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Ni jambo la kufadhaisha kuona kuwa sisi watungaji sheria wakati mwingine tunapotosha watu. Huwa tunawaambia eti turuhusu viwanda vijengwe na vifanye vinavyotaka. Ukweli ni kwamba viwanda hivyo vina madhara. Yale madhara ambayo yanaingia kutokana na moshi wa viwanda hivyo ni mengi. Watu wetu wataumia na tutatumia pesa nyingi kuwatibu hatimaye. Kwa hivyo, hamna haja kuwaacha watu waathirike ama wapatwe na shida eti kwa sababu haja yetu ni viwanda. Kuna mbinu nyingi za kuhakikisha kuwa vijana wamepata kazi ambazo ni nyingi. Viwanda vikiwa vinaiingia haimaanishi viingie kiholela. Sharti viingie kwa mpangilio. Pia ni sharti wenye viwanda hivyo waangalie mazingira. Pili, viwanda ...
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Speaker, would I be in order to ask the Mover to reply given the fact that we are repeating ourselves?
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Hon. Speaker, I second.
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii uliyonipatia ili nitoe mchango wangu na nipate kuwaeleza wenzangu ambayo yalijiri. Natumaini tuliunda kitengo cha mpito wa Serikali za Kaunti wakazunguke kila pahali, waulize wananchi na viongozi wao ni wapi wangependa makao makuu ya kila Kaunti yawepo. Sisi viongozi wote wa Taita Taveta tulikuwa 497 tulikutana Wundanyi. Tulikuwa na miji yetu minne, Wundanyi, Mwatate, Taveta na Voi. Sote, kwa kauli moja tukakubaliana makao yetu makuu yawe Mwatate. Lakini kwa sababu hakukuwa na vifaa wakati huo, wakaanzia Wundanyi iliyokuwa makao makuu ya serikali za mitaa wakati huo ndio washuke Mwatate.
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Baadaye kulingana na hali ilivyokuwa, pakawa watu wakaanza utaratibu wa kuihamisha Mwatate waipeleke pahali pengine lakini wananchi wakakataa. Ndio maana Seneti ilipokutana pakawa na makosa ya kusema bado makao makuu ya Taita Taveta yabaki Wundanyi. Hayo yalikuwa makosa. Mimi kama Mbunge wa Wundanyi nikaona hapa kuna makosa. Wananchi na viongozi walikubaliana makao makuu yawe Mwatate na hayo ndiyo marekebisho yanafanywa ili makao makuu yawe katika mji wa Mwatate. Ni muhimu tusisitize yawe katika jiji la Mwatate maana kuna sehemu zingine kama Mugero ambazo zinatakiwa kuwa jiji. Jiji la Mwatate ndilo tulikubaliana kuwa litakuwa makao makuu ya kaunti ya Taita Taveta. ...
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
ikaamua ilete Mswada huu irekebishe yale makosa yalifanyika. Tungependa makao makuu yapelekwe Mwatate kwa maana hapo kuna nafasi ya upanuzi na kuna ardhi ambaye imewekwa.
view
1 Dec 2016 in National Assembly:
Naomba niongeze kwamba Serikali kuu pia imeanza kujenga makao yake hapo hapo Mwatate. Kwa hivyo, tukiacha makao makuu yetu yaende pahali pengine, itakuwa tunafanya wananchi wapate shida ya huduma kwa sababu wakienda Serikali kuu, watakuwa Mwatate, wakienda kwa serikari ya ugatuzi, watapanda kule juu Wundanyi. Hapo ndio inaleta shida.
view