21 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono Taarifa iliyotolewa na Seneta wa Mombasa, ya kwamba mtu wa boda boda ameuawa kiholela. Nilitoa arifa hapo mbeleni tukiwa Kitui, ya kwamba hawa watu watatu waliuawa sehemu ya Tana River na watu ambao walijitambulisha kama polisi. Na katika Taarifa yangu, nilipewa wiki mbili ili niweze kupata jawabu kuhusu wale waliofanya uhalifu huo. Lakini hivi sasa, bado tunaendelea kupata habari ya kwamba watu wa boda boda wanauawa. Vile vile tunaendelea kupata habari kwamba polisi pia waliwapiga vijana wa JKUAT . Tukio hili haswa lilinaswa dhahiri shahiri kwenye picha, likionyes polisi wakiwapiga mateke vijana, ...
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Katika serikali zote za kaunti nchini Kenya, utakuta watu wamesimama katika majengo ya kulipia hela hizo. Wengi hawakupata hela zao kwa sababu gavana ambaye alitangulia kuwapatia kandarasi hizo hayuko katika utawala wakati huu. Bw. Spika, utaona kwamba watu wengi wakilalamika, wakisema pending bills, na jambo hili limekua kidonda ndugu katika kaunti zote za Kenya. Hata katika Kaunti yangu ya Tana River, kuna watu wengi wanaodai pesa kwa kandarasi ambazo walifanyia serikali iliyotangulia. Wakati huu, Gavana ni mwingine, na jambo hili sio katika kaunti ya Tana River peke yake, bali katika Kenya nzima. Watu ...
view
12 Nov 2019 in Senate:
(CoG) kukaa pamoja na Contoller of Budget ili kuangalia hizi pending bills, ili watu hawa wasiwe na shida zaidi. Tukifanya hivyo, wataweza kulipa madeni yao, na maisha yao yasisimame. Bw. Spika, Taarifa hii imetoka wakati mzuri, ila tayari tumechelewa, lakini ni vyema kabisa kwa Seneta wa Wajir kutoa taarifa hii kwa wakati huu. Tunaunga mkono kwamba magavana walipe pesa hizo. Hakuna mtu anadai gavana pesa, kwa sababu kandarasi imetolewa na serikali. Wao wameenda kuweka vidole pamoja na serikali hio. Huyo gavana atatakikana kulipa hiyo pesa hata kama hatakuwa mamlakani kwa sababu hio pesa sio yake bali ni pesa ya serikali.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Nitazungumzia jambo hili kwa ufupi. Kweli kabisa, nilipomsikia rafiki yangu, Sen. Madzayo, akizungumza, nilikumbuka siku ambayo nilidunda mara tatu katika Jimbo la Kilifi, ambako ni jirani na kwangu. Kidogo roho yangu ilipaa juu kidogo.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Nilidunda nikiwa ndani ya ndege hiyo. Sikuyumbayumba; huko juu ilikuwa---
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Kweli, kwa aliye ndani ya chombo, chombo ndicho hudunda. Nawe ukiwa ndani ya chombo hicho, basi unadunda maradufu.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Hii ni kwa sababu chombo kikiyumbayumba, pia aliye ndani ya chombo hicho pia huyumbayumba. Kwa hivyo, Sen. Wetangula, kile chombo nilichokuwa ndani, ambacho ni ndege, kilidunda mara mbili au tatu. Nilipomsikia rafiki yangu akielezea jinsi ndege hiyo haikumpeleka vizuri kwenye anga, nilikumbuka kuwa utakuwa unayumbayumba huko angani, na unadundadunga hapa kwa mchanga pia. Hiyo ni hatari kubwa sana. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, tunaiomba Kamati tekelezi ya Uchukuzi na Mawasiliano ifanye uchunguzi, kwa sababu ni juzi tu ambapo ndege hiyo ilitoka hapo uwanjani na ikaanguka hapo nje, na kuhatarisha maisha ya watu wengi. Kwa hivyo, ni vizuri Kamati hii iangalie ...
view
12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Nilipata fursa ya kutembea na Kamati hii, haswa wakati huu. Pia, nilipata fursa ya kutembelea Hospitali ya Hola, na kwa kweli, kazi inayofanywa na Kamati hii ni nzito. Hii ni kwa sababu wanatembelea zahanati zote, na kuwaongea na madaktari walioko humo. Wakitoka huko, wanaenda kuandika ripoti yao kuhusu yale waliona kule. Kwa hali hiyo, hauwezi kujua mambo haya mpaka uhusike na utembee nao. Mimi sio mwanakamati wa Kamati hii, lakini nimetembea nao. Nilikuwa nao katika kaunti za Malindi, Mombasa na Tana River. Hivyo basi, nilijua kwamba kazi wanayoifanya ni ngumu, na wanastahili kuongezwa muda ili waweze ...
view
12 Nov 2019 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view