12 Nov 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono.
view
8 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja iliyoletwa na Sen. Kasanga. Nampongeza Sen. Kasanga kwa kuleta Hoja hii, ambayo madhumuni yake ni kuwa na makundi ya kijamii ya kukuza miti, ambayo ina faida nyingi katika nchi yetu na ulimwengu nzima. Tunafahamu kwamba dunia bila miti sio dunia. Dunia ikikosa miti, itakuwa jangwa na hakutakuwa na maisha mazuri. Tuna jukumu la kuweka sheria ambayo itakuza miti katika kaunti zote 47. Tunapaswa kuweka asilimia fulani ya fedha za kaunti kwa sababu ya kukuza makundi ya jamii ambayo yanakuza miti. Madawa yote duniani yanatokana na miti. Madawa ...
view
8 Oct 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, mito mingi katika nchi yetu imekauka, na maisha kuharibika. Janga hilo limeletwa na ukosefu wa miti katika misitu ya asili na katika milima ambayo mito yetu hutoka. Kaunti ya Tana River imeathirika pakubwa, kwani mito mitano ilikauka hivi majuzi. Hii ni kwa sababu miti imekatwa kwa wingi katika sehemu ambazo mito hiyo inatoka. Mvua imekosekana kutokana na uhaba wa miti katika misitu. Jangwa imetokana na hali hiyo, ambayo ni hatari katika maisha ya binadamu.
view
8 Oct 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, miti huvunja upepo mkali, ambao ni hatari katika maisha ya mwanadamu kwani inaharibu mali. Penye miti mingi hata kuwe na upepo mkali unaoweza sababisha uharibifu wa mali, miti husaidia pakubwa. Na katika hali hiyo ambapo sisi, kama Seneti, tunafaa kuweka sheria kama hii iliyoletwa na Sen. Kasanga siku ya leo. Tuna haki ya kuunga mkono Hoja hii hili nchi ya Kenya iwe na miti. Kwa hakika, palipo na miti pana maisha mazuri. Dunia bila miti inakosa urembo na hewa safi. Kwa hivyo, tukipanda miti mahali penye janga, ukali wa jua utakosekana na pahali hapo patakuwa pasafi ...
view
8 Oct 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, nchi ya Kenya imegawanywa katika kaunti 47. Katika kaunti hizi, kuna zile ambazo ziko katika sehemu ya milima, ambapo hupata mvua; na kuna zile ambazo ni sehemu kame. Tukinyunyizia miti maji na tukuze makundi ambayo yanapanda The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
8 Oct 2019 in Senate:
miche ya kukuza misitu, tutatengeneza nchi ya Kenya, na tutapata mvua na hewa safi. Kwa hivyo, hatuna budi, kama Seneti, kuunga mkono Hoja hii. Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Asante kwa kunipa nafasi.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Naunga mkono Mswada huu wa wafanya biashara wadogo wanaofanya biashara zao katika sehemu za barabarani, vitongojini na katika vituo vya mabasi na matatu ambao wamedhulumiwa kwa muda mrefu sana. County Council ya zamani iliweka askari wa kuwafukuza The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
3 Oct 2019 in Senate:
wachuuzi hapa na pale. Pia, serikali za kaunti kwa wakati huu zimeweka askari wa kuwahangaisha wachuuzi hawa. Watu hawa wanapata dhulma nyingi sana wakifukuzwa huku na kule. Vile vile bidhaa zao hupotea na kuporwa. Ni wakati muafaka kabisa kuwa na sheria ambayo itasimamia wafanya biashara hawa ambao wanachuuza mali yao ndogo ndogo. Bw. Spika, unavyojua, kaunti zinaendelea kujengwa na tunaomba watenge viwanja vya soko maalum katika sehemu za kaunti ili wachuuzi waweze kuendelea na biashara zao.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Mzee wetu ambaye tunamheshimu sana, Senior Counsel, yuko barabarani.
view
3 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Vile mnavyojua Senior counsel ambaye tunamheshimu, baba yetu, mzee Orengo, ni mtu anayeheshimika sana. Sisi wengi tumefuata nyayo zake ndio tumekuja hapa. Sikusema kwa roho mbaya, nimesema kwa vile alikuwa anaongea na watu. Na vile tunajadili kuhusu biashara za watu wa barabarani, pia naye alikuwa katika sehemu ya kupitia na si kwa ubaya. Yeye pia ametupatia fursa hiyo. Ninafikiri naweza kuendelea. Bw. Spika, kaunti zinaendelea kujengwa na ni kweli wachuuzi wanafuata biashara katika sehemu za mabasi. Lakini vile kaunti zinaendelea kujengwa na pesa za ugatuzi zinafika katika sehemu za kaunti, ni wakati wa kuweka soko maalum na ...
view