17 Sep 2019 in Senate:
Tana River, kwa sababu, tumeanzia katika kaunti ambazo zimeendelea sana. Ningependelea mje Tana River pia muone vile kunakaa. Kama hamtashindwa kukaa katika hoteli zetu, tutawapeleka Mombasa. Lakini mimi nina imani kwamba mnaweza kuja kukaa na sisi huko Tana River na tuendelee. Sisi ni marafiki wa watu wa Kitui na nimeongea na Seneta kuhusu mambo kidogo kidogo yaliyo pale na tutayatatua na kila kitu kitakuwa sawa. Ninajua sehemu ya Tana River iko na watu wengi wa Kitui kuliko watu wa Tana River. Asante, Bw. Naiba Spika. Naunga mkono Mswada huu.
view
17 Sep 2019 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, point taken.
view
1 Aug 2019 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja iliyoletwa na Sen. Pareno. Kabla sijafanya hivyo, ningependa kutuma rambirambi zangu kwa jamaa na marafiki wa waliotuacha. Miongoni mwao ni marehemu mhe. Ken Okoth na aliyekuwa Gavana wa Bomet, mhe. Joyce Laboso. Tuko pamoja nao wakati huu mgumu.
view
1 Aug 2019 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, teknolojia ni kitu muhimu hasa katika sehemu ninakotoka. Huko kuna hospital chache sana na ni vigumu kuzipata. Watu wengi hupata shida kupanga foleni hospitalini ili wapate matibabu.
view
1 Aug 2019 in Senate:
Tukitumia teknologia ya kuunganisha mgonjwa na daktari, itapunguza foleni ambazo wagonjwa wengi hulazimika kupanga ili kupata matibabu. Kupitia matumizi ya teknolojia, wagonjwa wataweza kuzungumza na daktari popote alipo. Pia, kuna malipo mengi ambayo mtu hulazimika kufanya kabla hata hajapata matibabu. Katika hospitali kubwa, mgonjwa anapoenda kumwona daktari, yeye hulazimika kutoa pesa nyingi. Kufikia wakati unapopata matibabu, mtu huwa ametoa pesa nyingi licha ya kuwa kupata pesa ni shida. Kupitia teknolojia, wagonjwa wataweza kuwasiliana na madaktari katika sehemu zingine. Kuna wakati mgonjwa huenda kumwona daktari kisha akaruhusiwa kwenda nyumbani. Wakati mwingine, mtu hutakikana kurudi hospitalini ili kuchukua majibu ya uchunguzi uliofanywa. ...
view
1 Aug 2019 in Senate:
na uangalie. Hata hivyo, wakati mwingine Google itakufanya ukate tamaa, kwa sababu ukijua shida yako, utadhani dunia yako imeisha. Lakini ukiongea na daktari wako moja kwa moja, wakati mwingi madaktari wanakutia moyo. Mgonjwa anatakikana kupata heri njema kwa daktari moja kwa moja. Bi. Spika wa Muda, katika hali hiyo, ninaunga mkono Hoja hii ya teknolojia, ambayo sasa hivi imenawiri katika dunia nzima. Asante, Bi Spika wa Muda.
view
25 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi. Kwa kweli dunia imeharibika. Bidhaa na hasa vyakula vimeharibiwa kabisa. Bidhaa za nyama zikiwekwa kemikali ili zisioze ama zikae kwa muda murefu, tunakiuka hali halisi ya chakula. Katika hali hiyo, nyama inawekwa madawa ili ikae siku mbili au tatu bila kuharibika. Ile kemikali ambayo inawekwa hiyo nyama kwa muda mrefu inaweza haribu afya ya mwanadamu.
view
25 Jul 2019 in Senate:
Ninaunga mkono taarifa hii ili kemikali na vitu vingine visiwekwe kwa nyama na hata vyakula vingine kama ndizi, machungwa na kadhalika. Chakula kiwekwe katika hali yake halisi ambayo imekuzwa katika mashamba ili tukuze jamii bora zenye afya.
view
25 Jul 2019 in Senate:
Ninaunga mkono, Bw. Spika.
view
23 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Kama unavyoniona, nimesimama wima kama mlingoti, bila kuyumbayumba, ili kuunga mkono Taarifa iliyotolewa na Seneta wa Kaunti ya Mombasa, ya kwamba makao makuu ya uvuvi yajengwe huko Pwani.
view