Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 161 to 170 of 272.

  • 23 Jul 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kama unavyojua, uvuvi hufanyika katika sehemu ya Bahari ya Hindi, huko katika Pwani ya Kenya hii, na pia katika maziwa makuu kama vile Ziwa Viktoria na Ziwa Turkana. Vile vile, uvuvi pia unafanyika katika mito mikuu, kama Mto Tana huko kwangu nyumbani. Bw. Spika wa Muda, makao makuu ambayo yatajengwa katika mji wa Nairobi, huko South C, hakika yatanyima utenda kazi, hasa zile stakabadhi zinazohitajika na wavuvi katika sehemu ya Pwani. Hii ni kwa sababu Benki ya Dunia ilitoa pesa hizi na hasa ikaangazia Tana River, Mombasa, Kwale na pia Lamu. Sehemu hizo ziko na ardhi ... view
  • 23 Jul 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, sisi tunasema kwamba Kamati husika iangalie jambo hili. Sisi hatutakuja kulalamika wakati ofisi na makao makuu tayari yamejengwa. Saa hii, ambapo bado makao hayo hayajajengwa, na wananuia kujenga, ndio tunataka Kamati husika iaangalie na waseme, “La sivyo; wacha tujenge huko Pwani ya Kenya.” view
  • 23 Jul 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kuna haja gani twende katika ugatuzi wa Kenya hii, wakati mambo muhimu ambayo yanafaa sehemu tofauti, kama vile Pwani, yanafanyika hapa Nairobi? Sisi tuko katika majimbo yaliyoko katika ugatuzi, na ni lazima tuyaweke mambo mahali yanafaa. Pahali panapofaa makao makuu haya ni Pwani ya Kenya. Kwa hivyo, naiomba Kamati husika iangazie maneno haya mapema ili makao hayo makuu yasijengwe hapa South C, Nairobi. view
  • 23 Jul 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, mimi ninaishi huko South C, na nilipoangalia sehemu hiyo, niliona kuwa dunia imejaa kabisa na ujenzi unaendelea kila wakati huko. Hali kadhalika, kama ujenzi huo utafanyika katika uwanja ya Serikali, basi haina haja. Serikali inaweza kutenga uwanja huo kwa miradi mingine inayofaa Nairobi. Sisi tuko na ardhi ya kutosha ambapo makao hayo yanaweza kujengwa huko pwani. view
  • 23 Jul 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Taarifa iliyotolewa na Seneta wa Mombasa, Seneta Faki, ambaye ni rafiki yangu. Asante sana, Bw. Spika wa Muda. view
  • 18 Jul 2019 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii ya DORA. Ningependa pia kuweka sauti yangu katika kuheshimu Seneti kwa sababu tuko na nyumba mbili za kutengeneza sheria. Hasa Seneti hii inafanya watu ambao wametuchagua katika sehemu zetu kufikiwa na pesa. Kama kutakuwa na kizungumkuti cha watu ambao wanataka kupinga pesa zisifikie Wakenya, ni lazima sisi tusimame wima tuseme, hapana, haiwezekani. Ni lazima watu wetu wapate huduma za afya. Inafaa pesa zifike upande huo kwa sababu ikiwa pesa zitakuwa zinabaki hapa juu, tunajua hakuna maendeleo yatatendeka. Tuliapa kwa Biblia na Quran tukasema tutakinga ugatuzi kabisa usije ukaangushwa. ... view
  • 18 Jul 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Taarifa ya Sen. (Prof.) Kamar. Ninakotoka kuna mashamba makubwa ambapo mahindi yanakuzwa kwa wingi kupitia unyunyizaji maji. Kuna Hola, Bura na Galana-Kulalu irrigation schemes ambazo zinapatikana katika Kaunti ya Tana Rive. Nashangaa sana kusikia kuwa Serikali ina mpango wa kuagiza mahindi kutoka ng’ambo. Sehemu nilizotaja zinatosha kutoa chakula cha kutosha watu wa Tana River na Kenya nzima. Kwa nini tusikuze mahindi yetu hapa nchini badala ya kuagiza kutoka nje? Hilo ni swali ambalo tunafaa kujiuliza. Je, tuna upungufu gani? Tuna mito mikubwa ambayo ina maji kila wakati. Vile vile, tuna ardhi iliyo na rotuba. ... view
  • 18 Jul 2019 in Senate: katika sehemu za unyunyiziaji mashamba maji. Mashamba yetu hayanyunyiziwi maji jinsi inavyostahili. Ni kinaya kuwa Wizara ya Kilimo na Unyunyiziaji Maji haiwezi kusaidia watu wetu kupanda mahindi ili kupatikane chakula, kwa sababu nimeskia kuna mpango wa kuagiza chakula kutoka nchi nyingine. Tuna wataalamu, maji na ardhi bora ya kukuza mahindi. Nilishangaa kusikia kuwa maghala yetu yamejaa mahindi, lakini Serikali bado inapanga kuagiza mahindi kutoka nje. Hayo ni mahindi ambayo hatujui yanapandwa vipi. Pengine huwekwa dawa ambazo hazijulikani. Ikiwa tuna ardhi na maji ya kutosha, kwa nini tunawacha watu wetu kuteseka? Nafikiria tulienda na wewe kule Galana. Watu wa Galana ni ... view
  • 17 Jul 2019 in Senate: Asante, Bw. Spika, kunipa nafasi ili kumuunga mkono Seneta aliyewasilisha taarifa hii. Vile tunavyojua, kuna mambo yanayofanyika katika shule za upili. Kuna mambo yanayofanyika wanafunzi wanapojiunga na shule za upili na hiyo ni dhuluma. Kamati ya Elimu inafaa kufanya uchunguzi na kupendekeza jinsi ya kukomesha dhuluma katika shule za upili. view
  • 17 Jul 2019 in Senate: Wanafunzi wengi wanahofia kwenda shule kwa sababu kuna baadhi wanaoamrishwa kwenda kwa magoti. Baadhi humwagiwa maji baridi na wengine hupata kichapo cha mbwa. Hiyo si haki kwa sababu wazazi hupeleka watoto wao shuleni ili wasome bila shida. Ikiwa wanadhulumiwa, wengi hawawezi kusoma kwa sababu wanaogopa wenzao. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus