17 Jul 2019 in Senate:
Kumekuwa na ongezeko la visa vya dhuluma. Mimi pia nilidhulumiwa wakati nilipokuwa shule ya upili. Cha kushangaza ni kwamba bado kuna dhuluma shuleni. Watoto wetu hawafai kudhulumiwa na wengine. Dhuluma shuleni inafaa kukomeshwa kwa sababu inaweza kufanya wanafunzi wa shule za msingi kukataa kwenda shule wakichukulia kuwa shule si pahali pazuri. Kwa hivyo, visa vya wanafunzi kudhulumiwa shuleni vinafaa kukomeshwa.
view
17 Jul 2019 in Senate:
Ahsante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ninamheshimu sana Seneta mteule anayetoka katika Kaunti ya Kwale, Sen. (Dr.) Zani. Yeye ni msomi na mjuzi wa Lugha ya Kiswahili. Kwa kweli, mtu ambaye anaongoza kikao katika Bunge ni Mwenyekiti ama Bwana Spika. “Mzungumzishi” ni yule ambaye anafanya watu ambao ni bubu waweze kuongea.
view
17 Jul 2019 in Senate:
Kwa hivyo, Bw. Spika wa Bunge hili la Seneti, usiruhusu mtu akuite “mzungumzishi” kwa sababu wewe ni Bwana Spika. Asante sana, Bw. Spika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
17 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, tunamheshimu sana Sen. (Dr.) Zani kutoka jimbo la Pwani, sehemu ile ya Kwale. Alitangulia kusema kwamba hatatumia neno “Bw. Spika” wala “mzungumzishi”. Hata hivyo, amemaliza kwa kutumia neon “mzungumzishi”. Tungependa aondoe arifa ambayo ametoa ili isikae katika rekodi zetu na kuheshimu Bunge la Seneti. Asante, Bw. Spika.
view
10 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kuna haja ya kuhifadhi mazingara yetu hasa misitu ya asili na misitu iliyopandwa. Nilipata fursa ya kutembea na Waziri, Tobiko katika misitu iliyopo Tana Delta, Kaunti ya Tana River. Katika kuhifadhi misitu katika kaunti yangu, kuna miti ya Mathenge ambayo inamea kila mahali na inaharibu mazingara. Sehemu ya Tana Delta ambapo tunalisha ng’ombe zetu, Mathenge imemea na kuharibu mazingira yetu. Bi Spika wa Muda, si ukweli kwamba miti yote inatengeneza mazingira. Ukiona athari ya miti ya Mathenge utatambua kwamba miti zingine zinaharibu mazingira. Mathenge inawezamea katika sehemu za ukame na inamea ...
view
4 Jul 2019 in Senate:
Asante Sana, Bw. Naibu Spika. Jana ulinionya na leo mimi ni mwadilifu kabisa.
view
4 Jul 2019 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuchangia Mswada huu na kuunga mkono Kamati ya Uwiano ambayo ilikaa pamoja katika Bunge zote mbili, na kuandika ripoti nzuri kabisa ambayo tunaweza kusema, kwa wakati huu, tuiunge mkono ili Mswada huu uweze kuwa sheria. Bw. Naibu Spika, Bunge zote mbili zimekaa chini ya uenyekiti wa Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge la Taifa, Mhe. Adan Duale, na kutupatia Mswada huu. Hasa walisisitize kwamba sehemu ya mazingira iangaliwe vizuri katika kutengeneza shirika la Unyunyizaji Maji, yaani Irrigation Board. Pia walinakili vizuri katika kugharamikia pande zote, yaani cost sharing katika kimombo.
view
4 Jul 2019 in Senate:
Ripoti hii ilirejeshwa katika Bunge zote mbili na ikajadiliwa na watu ambao wamesema sasa ni nzuri. Tuliposomewa Ripoti hiyo hapa mbele, tuliiona ikiwa nzuri kabisa. Nikiwa Mwanachama wa Kamati ya Ukulima, Ufugaji na Uvuvi, ambayo Mwenyekti wangu ni jirani hapa nyuma yangu, tuliweza kuikalia vizuri. Nilishiriki katika mazungumzo ya kuleta uwiano na tutaiunga mkono.
view