16 Oct 2018 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, asante kunipa nafasi hii ili kuchangia Mswada ulioletwa hapa na dadangu, Seneta Mteule, Rev. Naomi Waqo. Ujangili na ugaidi umekuwa tishio kubwa katika nchi ya Kenya. Ugaidi umeshuhudiwa mahali pengi katika nchi hii na hasa wakati Chuo Kikuu cha Garissa kilipovamiwa. Wale waliohusika walikuwa vijana wa vyuo vikuu ambao walitekeleza maafa hayo. Hiyo inamaanisha kuwa sisi kama Wakenya tumepoteza uadilifu kama jamii ya kiafrika.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Ugaidi ni kitu ambacho sisi kama jamii tunafaa kuanza kupigana nacho. Ni vyema tupambane na ugaidi kabla haujafikia katika serikali za kaunti ama Serikali ya kitaifa. Sisi kama jamii ambao tunaishi vijijini na sehemu mbalimbali za Kenya tunafaa kuukandamiza. Tunafaa kutangaza na kuambia wanaohusika na ugaidi kuwa ugaidi haufai.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Hakika, masomo kuhusu ukandamizaji wa ugaidi yanafaa kutolewa kuanzia shule za chini kabisa mpaka vyuo vikuu ili watu wajue kuwa ugaidi ni kitu kibaya.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Seneta aliyezungumza kabla yangu, Sen. Madzayo, alisema kuwa ugaidi hasa unaletwa na ukosefu wa ajira na ni kweli. Vijana ambao hukosa ajira na kubaki nyumbani hukosa jambo la kufanya na kuingilia ulevi. Hatimaye wanaingia katika ugaidi kwa sababu wale wanaouendeleza huwaambia watawalipa vizuri. Kwa hivyo, ni jukumu la serikali za kaunti na Serikali ya kitaifa kupatia vijana wetu majukumu. Wale waliosoma wanafaa kupata vibarua ili wasijiingize katika ugaidi. Bi. Spika wa Muda, ugaidi unarudisha nyuma jamii iliyostaarabika na ambayo inataka kuendelea. Kuna mambo ambayo hufanyika kule Pwani ambayo ni ya kuvunja moyo sana. Wakati wa kushambulia magaidi, tumeona jamii fulani ...
view
16 Oct 2018 in Senate:
Ni vyema tuungane mikono kuanzia vijijini ambako jamii zinaishi na lisiwe jukumu la Serikali pekee. Serikali pekee haiwezi kufaulu katika vita dhidi ya ugaidi. Magaidi wanaishi miongoni mwa jamii vijijini na katika miji mikubwa ya nchi hii. Kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Oct 2018 in Senate:
hivyo, liwe jukumu la Wakenya wote kuangalia na kujua ni nani gaidi na jinsi tutakavyopigana na ugaidi.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Naunga mkono Mswada huu uliyoletwa na Sen. (Rev.) Waqo wa kurekebisha sheria ya kupigana na ugaidi, ujangili na ujambazi ambao umekuwa janga kubwa katika hii nchi yetu.
view
16 Oct 2018 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, asante kwa kunipatia nafasi.
view
11 Oct 2018 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nitume risala zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki waliopoteza maisha ya wapendwa wao katika ajali hii ya barabarani. Bw. Spika wa muda, ajali za barabarani zimekuwa kawaida katika maisha ya Wakenya. Sielewi kwa nini askari wa trafiki wapo barabarani. Kwa nini tusiwaondoe askari wote kutoka barabarani hapa Kenya? Tumewaajiri askari hawa barabarani ili kulinda na kuangalia iwapo magari haya yamebeba watu kiwango kinachostahili. Wakati askari hawa wako barabarani na magari yanabeba watu zaidi ya kiwango kinachotakikana, yanaenda kuanguka kila siku na kumaliza watu. Baada ya watu kufa barabarani ndio ...
view
11 Oct 2018 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwa uhakika wakulima wa mahindi katika nchi hii wanafaa kupewa heshima. Pia inafaa zile changa moto ambazo wanazipitia zichunguzwe. Magala yamejaa mahindi ya misimu iliyo pita. Nazungumza kwa uhakika kwa sababu natoka sehemu ambayo mahindi inakuzwa. Ukisafiri katika barabara za nchi hii, utakuta mahindi inamea kila sehemu hasa katika msimu wa mvua. Mahindi haya yanauzwa kando ya barabara, hayapati soko halisi. Wanaopanda haya mahindi wanataka kutumia wanachopata kugharamia mahitaji ya kinyumbani kama karo na kununua chakula. Mahindi ni chakula halisi ya Waafrika hasa Wakenya. Mahindi huliwa katika nyanja mbali mbali. Wengine ...
view