Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 314.

  • 4 May 2020 in National Assembly: Wananchi walisema wanataka Mbunge wa Bunge la Kaunti (MCA) awe na keki yake ndiyo wamuulize maswali kwa sababu wanaketi naye huko mashinani. Sisi tuko Nairobi na yule MCA aliyechaguliwa mashinani wanataka awe na keki yake huko, na haya ndiyo maoni yao. Wananchi walisema wanataka Waziri wa Serikali Kuu atoke ndani ya hii Nyumba yetu. Hayo sio maoni ya wakubwa, lakini ni ya wananchi. Kama ningekuwa na nafasi ya kuongea, ningewaelezea wenzangu maoni mengi ya wananchi. Ukija hapa kusema unapinga, jua unapinga wananchi sio sisi. Wenzangu, ningetaka kusema kwamba tumeona wananchi wako na macho. Unajua kama kitu ni kizuri na unataka ... view
  • 4 May 2020 in National Assembly: Nataka kuwaambia wenzangu ambao wanapinga kwamba hawapingi hii Nyumba ama wakubwa, wanapinga wananchi ambao wametoa maoni yao katika BBI. Kawa hivyo, tuheshimu maoni ya wananchi kwa sababu wameongea na tuko na rekodi zote. Kama asilimia thelathini ya wananchi walikuwa wanasema hawataki wanawake katika Bunge kama waakilishi wa wanawake wa kaunti, lazima tukubali . Wananchi walisema vitu vingi virekebishwe na tuweke vingine. view
  • 4 May 2020 in National Assembly: Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimechukua amri yako. Lakini ningekuomba uwaangalie walioketi mpaka saa tatu, ili kuwe na njia ya kuwapa nafasi kwa sababu wamengoja sana. view
  • 18 Feb 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Nampa Mheshimiwa hongera kwa kuleta Hoja hii ya nzige. Kulingana na jinsi wenzangu walivyoongea, nzige hawajaanza kuja leo. Nzige walikuja kitambo sana. Kuna wakati walikuja wakati wa ukoloni. Wakati walipoingia Kenya enzi za ukoloni, nzige wana madhara mengi ya kula miti, matawi na nyasi. Baada ya hapo, kuna ugonjwa wa ng’ombe. Kwa hivyo, tunalia kwani hili ni janga baya zaidi. Hili ni jambo ambalo limetushtua sisi ambao tuna wanyama kama ng’ombe. Tunajua baada ya nzige kuisha na dawa ama kuisha kwa njia yoyote, wataleta ugonjwa wa ng’ombe. Tumetembea upande ... view
  • 18 Feb 2020 in National Assembly: North Horr wakati waliingia upande wa Marsabit. Nzige hao ni wengi sana. Pia vile wenzangu wamesema, wanazaa kila baada ya masaa mawili. Wakati wanamwaga mayai, hata ukisimama wakati wanapita wanamwaga kinyesi chao na wewe mwenyewe unakuwa mweusi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 18 Feb 2020 in National Assembly: kama makaa. Huwa wanamwaga mbegu zao na wanawacha hapo chini. Saa hii tumeshtuka sana kwa sababu nzige hawa wana ugonjwa ambao tunaogopa hata sasa. Mara ya kwanza walipomwaga dawa hiyo, haikuwaua wale nzige. Badala ya kufa, wakaanza kushuka chini na kufagia kila kitu vile ambavyo trekta hufagia. Hutaona nyasi hata moja. Ni jambo ambalo litaleta shida katika Kenya nzima kwa sababu nzige wanahama na yale mayai yamemwaga pale ndiyo yanaamka. Naomba Serikali iamke na kuangalia ile dawa inamwagwa kwa sababu isipopimwa vizuri, tunaogopa kuwa italeta shida. Pahali ambapo dawa inamwagwa hapa chini panakauka. Nyasi inakauka. Tuna shida na ni lazima ... view
  • 10 Feb 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii nitoe pole zangu na za familia yangu na Kaunti ya Samburu kwa baba yetu Moi. Tunamkumbuka Baba Moi kwa mengi sana. Kile amefanyia Kaunti ya Samburu hatuwezi kusahau. Tunaamini yeye ndiye mtu wa kwanza kuanzisha shule ya upili ya wasichana katika Kaunti ya Samburu. Hatuwezi kusahau hata kidogo. Kila Mkenya anakumbuka kwamba Baba Moi hakuwa rais wa kuchezewa. Alikuwa rais wa kuheshimiwa zaidi. Ukiangalia kati yake na rais wa sasa, unaona kuna tofauti kubwa sana. view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia hii nafasi ili niunge mkono Ombi la Hon. Lentoimaga. Kuna maana ya Mhe. Lentoimaga kuandika Ombi hili. Nafikiri tuko na shida kubwa sana kuhusu haya mambo ya wizi wa mifugo. Sijui kwa nini inaitwa wizi wa mifugo ilhali ni kitu inaua wananchi katika pembe zote. Vita vilivyoko Baragoi ni mbaya zaidi. Ninaomba Kamati ya Usalama ichukue hatua na ihakikishe Waziri wa Usalama awe hapa ili wakutane. Shida kubwa iko kwenye hii ofisi. Watu wanauawa na inaporipotiwa, hakuna mtu anayejitokeza kuwa ni kweli watu wameuawa. Mali inaenda na watu wanaachwa bila chochote. Hakuna mtu anaangalia ... view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Miaka nenda miaka rudi, watu wamekuwa maskini na wengine kuuliwa. Hata sasa, tuko na watu karibu wanne ambao wako hospitalini Nakuru. Wamevunjika miguu na hakuna mtu anayewashughulikia. Wanapigana na kuuana tu ilhali Serikali iko kila mahali. Ng’ombe wanapita tu wakiangaliwa. Pia wao wanauliwa na hakuna hatua inayochukuliwa. Ninaunga mkono Kamati ya Usalama ichukulie maanani Ombi hili. Ni suala ambalo halina mchezo. Asante Bwana Spika kwa kunipatia hii nafasi. view
  • 16 Oct 2019 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu. Mambo ya wanyama wetu ni mengi. Niko katika Kamati ya Ukulima. Kila wakati huwa tunajiuliza ni kwa nini wafugaji wetu hawana njia yoyote ya kufaidika kutokana na wanyama wao. Sababu ya kutofaidika ni kwamba hawana soko lolote la kuuza wanyama. Hawana mahali pa kuchinjia wanyama. Katika Kenya nzima, hakuna mtu anayeweza kula chakula bila nyama. Unapokula nyama ndipo unahisi umekula chakula. Wanaofuga wanyama huwa wanaumia sana kwa sababu wakati wa ukame, wanyama wote wanakufa kwa sababu hakuna mahali pa kuwauza. Wakati mvua inaponyesha na wanyama wanapopata nguvu, wafugaji wanakosa mahali pa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus