23 Jun 2021 in National Assembly:
Sina mengi. Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda.
view
22 Jun 2021 in National Assembly:
Asante Bi Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nami nichangie kwenye huu Mswada wa fedha. Nataka kuunga mkono Mswada huu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
22 Jun 2021 in National Assembly:
Malengo ya Mswada huu ni kuongeza mapato ya Serikali. Mapato ni muhimu kwa sababu kuna mambo mengi ya kufanywa. Kwa hivyo, mambo haya hayatafanyika isipokuwa waongeze mapato. Nimefurahishwa zaidi na pale kwa wanakandarasi wadogo ambao si Wakenya wafaa kulipa ushuru. Hii ni kwa maana imekuwa kawaida wanakuja wanafanya kazi Kenya, wanachukua pesa zetu na kwenda nayo bila kulipa ushuru. Kwa hivyo, pale nimefurahishwa. Nataka pia niseme kidogo upande wa mafuta. Mafuta yakiongezeka bei, inaongeza gharama zingine za matibabu kwa sababu Wakenya wengi wanabidi kutumia kuni au makaa ambapo moshi unaoingia kina mama unawaathiri mapafu wanakuwa na ugonjwa wa mapafu. Kwa ...
view
15 Jun 2021 in National Assembly:
Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi na mimi nichangie. Naunga mkono kaunti zipate pesa. Lakini kaunti zikipata pesa hizo, zilipe madeni yao kwanza. Kama wenzangu walivyotangulia kuzungumza, wanakandarasi wengi wanapata shida. Wengine walichukua mikopo na wengine pia wana familia. Kwa hivyo, ni muhimu mwanzo wawalipe kisha waendelee na mengine. Pia, nizungumze kuhusu pesa zinazostahili kupelekwa kwa pensheni. Kaunti zinafaa zipeleke pesa hizo mwanzo. Ni kwa sababu wao wanakata kwa wafanyakazi kisha hawazipeleki kule. Hiyo ni kama kombora ambalo linangojea kupasuka. Itafika wakati wale wafanyakazi wa kaunti hawatalipwa pensheni yao. Hiyo itakuwa ni vibaya sana kwa sababu mtu ...
view
15 Jun 2021 in National Assembly:
Itatusaidia sisi muliokuwa mkituona wachache. Saa hii inshallah, tutakuwa wengi Mungu akipenda. Kaunti wakipata pesa hizi wahakikishe wamezitumia vizuri kwa afya, kwa sababu afya ni kwa kila kitu. Pia, watumie nafasi hiyo kwenda kuhamasisha na kuwaeleza wananchi, haswa akina mama, mambo ya afya. Afya sio kujenga hospitali tu bali pia kujua huduma zinazopeanwa. Kuna changamoto sehemu za kwetu. Kuna watu hawafikii zile hospitali. Hospitali kama ya King Fahd iliyoko pale, kutoka Kiunga mpaka kule ni Kshs2000. Sasa tunawaomba hawa Magavana wahakikishe kila wodi imefikiwa. Kwetu haiendi hata kwa wodi. Kama wodi ya Kiunga, Ndau na Kiwayu iko kwa wodi moja ...
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ili nizungumzie haya Makadirio ya Bajeti. Mwanzo, napongeza Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
Katika hiki kitengo cha kwanza cha Executive Office of the President, wanafaa kupewa pesa zaidi na hata hicho kipeo chao kinafaa kuongezwa juu zaidi kwa sababu kinafanya kazi nyingi nzuri. Katika State Department of Interior and Citizen Services, kipeo chao kikipelekwa juu zaidi itakuwa vizuri kwa sababu bado tunatarajia kazi iwe nzuri zaidi. Hii ni kwa sababu kuna sehemu zingine kama kule kwetu, Kaunti ya Lamu, bado kuna watu hawajapata vitambulisho kwa miaka mitatu sasa. Wanazo stakabadhi zile za kungojea vitambulisho. Kama hiyo pesa ni kidogo, kazi haifanyiki vizuri. Kwa hivyo, hata wakiongezewa siyo vibaya. Bora kazi ifanyike. Sisi watu ...
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
Haina pesa mingi. Wizara hii inafaa kujijenga kama vile kuwa na maofisi. Blue economy ikiangaliwa vizuri tunaweza kuandika vijana wengi kazi. Lamu, kwa mfano, itaajiri watu wengi. Ninaona pesa kidogo imewekwa na kisha tunasema tunataka kukuza blue economy. Hiyo pesa kidogo pia hatuioni. Nilitarajia iwekwe pesa nyingi ili tuone viwanda vya samaki vikiekeza. Kwa kufanya hivyo, ndio kukuza blue economy sio tu kwa kutafiti kila siku na hatuoni mambo yakiendelea. Nilitarajia kuwa Kamati Kuu ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
9 Jun 2021 in National Assembly:
Kilimo ingeweka hapa ceiling kubwa na kuzungumzia mambo mengi ambayo yanataka kufanya upande. Tungeandika vijana wengi sana, na bado tuko na uwezo. Tuko na Kaunti tano za Pwani na pia kule upande wa Ziwa Victoria na Ziwa Naivasha. Tunaweza jipanga vizuri na blue economy na ikatuondolezea shida kubwa ya ukosefu wa kazi. Ningependa kuwapa wenzangu nafasi na kwa sababu ninaona masaa yameenda. Asante.
view
19 May 2021 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda, lakini mimi nilikuwa nimeweka ombi kwa Hoja iliyopita. Ahsante.
view