29 Jun 2021 in National Assembly:
zinazohitajika lakini pia akawa hafanyi kazi vizuri. Kwa hivyo, utaona saa hii kama sasa wakati huu, tumepewa pesa nyingi kama Kaunti ya Lamu na World Bank lakini utaona kwa kaunti zimebakia pesa zaidi ya shillingi millioni mia tatu ambazo hazijatumika na watu wana njaa. Kama wangepea women representative, pesa kama hizo zingekuwa zimetumika vizuri sana katika vikundi. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ule mradi unaitwa Climate Smart, imagine mwezi unaokuja ndio mwisho. Hizo pesa zitabidi zirejeshwe na Serikali ya Kenya inalipa loan . Tukipata wafanyikazi ambao wana qualification s na hizo qualities zote ambazo zimewekwa hapa kama
view
29 Jun 2021 in National Assembly:
, waweke watu wa kutoka jamii mbalimbali, kila wadi ipate nafasi yake, wale walemavu pia wapate nafasi yao, youth na akina mama, naona itaweza kusaidia sana. Ahsante.
view
23 Jun 2021 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. I wish to ask Question No. 198/2021 to the Cabinet Secretary for Sports, Culture and Heritage. (i) Could the Cabinet Secretary explain the plans in place to rehabilitate and restore ancient and historical monuments of national importance to their original form and stature? (ii) What measures is the Government putting in place to ensure that buildings that are on the verge of collapse due to adverse weather, age and natural deterioration in Lamu Old Town, Lamu County and other coastal monuments with status of national or world heritage are restored to their original form and properly ...
view
23 Jun 2021 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. On behalf of Hon. Adagala, I wish to ask Question No. 209/2021 to the Cabinet Secretary for Transport, Infrastructure, Housing, Urban Development and Public Works. Could the Cabinet Secretary specify any plans the Government has to repair and operationalize the Kisumu-Butere Railway Line in order to promote economic growth in the area and state the timelines for the same? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
23 Jun 2021 in National Assembly:
(Lamu (CWR), JP): Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ili nichangia katika Mswada huu muhimu wa damu.
view
23 Jun 2021 in National Assembly:
Mwanzo, ningependa kupongeza Wizara kwa kufanya majukumu yake. Baada ya wale wanaosaidia kujitoa, walichukua jukumu hilo, wakasimama na wakaanza kurekebisha na kufanya mambo wenyewe. Tumekuwa tukitegemea wafadhili kwa muda mrefu. Ghafla, wafadhili walijitoa. Walijizatiti kusimamia hali ile ngumu ambayo ilikuwa. Damu ni muhimu sana. Naomba wenzangu wapitishe Mswada huu kwa umoja. Wenzangu waliotangulia walisema kwamba hivi vituo vya damu vinafaa kuwa katika kila eneo bunge. Lakini, ziko kwa mikoa sasa. Tukisema ziwe kwa kaunti, hatusemi tuwapatie. Ndio, ziwe za Serikali Kuu lakini ziwe katika kila kaunti kwa sababu kuna kaunti zingine zilizoko mbali na inakuwa ngumu kupata huduma hizi. Damu ...
view
23 Jun 2021 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, Wakenya wengi wako na hofu ya kuenda kutoa damu kwa kuogopa kuwa hali zao zitajulikana na wengine; wengi wanataka kutoa lakini wanaogopa hilo. Ikiwa itawekwa siri, kama vile Mswada huu unazungumzia, na watu waweze kuelemishwa, watu wengi watatoa damu. Wakenya wengi ni wakarimu na tuko tayari kusaidia wenzetu. Lakini Wakenya wahakikishiwe kuwa wanapopimwa na kupatikana na maradhi fulani, hiyo itakuwa siri yake tu na isitoke kwingine. Ikitoka kwa mmoja, inaharibia hata wengine kuenda kutoa damu.
view
23 Jun 2021 in National Assembly:
Narejelea tena kwamba damu ni muhimu na tunafaa kuwa na damu nyingi. Wengine wametoa hesabu ambazo hazina hakika lakini mimi ni mmoja wa wanakamati na Mswada huu ni mzuri. Walikuja wakatueleza na tumeusoma. Kwa hivyo, kuna umuhimu wa sisi kupitisha Mswada huu kwa maana ulipaswa kupitishwa mapema hata kabla ya sasa; ni Mswada muhimu. Langu ni kushukuru sana. Tulikuwa tunaona kuwa kazi hii ilikuwa imeachiwa Shirika la Red Cross lakini sasa nimeona kuwa Wizara ya Afya imechukulia yenyewe kufanya mambo muhimu na huduma muhimu kama hizi.
view
23 Jun 2021 in National Assembly:
Pia, wizara hizi hazifai kutegemea wafadhili sana. Kama kuna huduma yeyote ya afya, Wizara ya Afya inafaa ichukue majukumu hayo. Hili liwe ni funzo maanake tumepata funzo wafadhili walipojitoa kwa ghafla. Tusitegemee sana huduma muhimu zitimizwe na wafadhili.
view