Ruweida Mohamed Obo

Parties & Coalitions

Born

1978

Telephone

0722222784

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 439.

  • 9 Nov 2021 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Spika. Naona ikifunguliwa au isifunguliwe, yote ni sawa. Kupata akidi katika Jumba hili ni taabu sasa. Kwa hivyo, ifunguliwe au isifunguliwe ni kuwapatia nafasi wengine ambao wanatafuta sababu. Kupata akidi imekuwa shida. Kwa hivyo, vyovyote vile, ni sawa. view
  • 9 Nov 2021 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Spika. view
  • 13 Oct 2021 in National Assembly: Asante, Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono Lamu, Tana River na Kwale angalau nao wawe na mwakilishi wao. Hayo mengine tunangojea. Mambo ya makao makuu kuwekwa mbali na Lamu, kwetu tunasema ni mbali sana maana usafiri utakuwa mgumu. Tunangojea hiyo ili tubadilishe. view
  • 7 Oct 2021 in National Assembly: Asante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi nami nichangie. Naunga mkono ombi la sala za kitaifa. Mhe. Spika, shida ya Kenya ni kwamba tunaenda misikitini na makanisani kwa wingi lakini roho zetu haziko safi. Kwa hivyo, tunahitaji Mwenyezi Mungu aongoze hizi nyoyo zetu ili yale tunayokwenda kusema na kufanya yawe ni hayo hayo, haswa wakati huu wa karibu na uchaguzi, shida inakuwa kubwa Kenya. Tunahitaji maombi maana kuna viongozi na wanasiasa kama sisi ambao wengine wataona wako mbele na kumbe wakija wakiona uchaguzi sivyo walivyotarajia, italeta shida. Kwa hivyo, tunahitaji maombi. Maombi ni muhimu. Nchini Kenya hatuna shida ya sheria wala ... view
  • 7 Oct 2021 in National Assembly: La pili, nataka kuunga mkono ombi la Mhe. Mwashetani. Kuna matatizo makubwa na hivi visiwa. Visiwa vimekuwa hapo kwa karne nyingi, kama vile Kisiwa cha Kiwayu. Kisha watu wa KWS wanakuja wanasema ni marine . Watu wamekaa hapo miaka yote. Haya mambo yanafaa kuangaliwa. Hiyo shida inatokea huko kwa Mhe. Mwashetani pia iko Lamu. Naomba hili Bunge, tafadhali, kama kutakuwa kuna muda, tufanye hizi shida ziondoke. Watu wakae huko miaka yote kisha ghafla, title zije zitolewe na hatujawapangia tunawapeleka wapi na tukiwapeleka huko tunakotaka kuwapeleka, watakaa vipi na wamezoea kuwa hapo siku zote? Ah,sante, Mhe. Spika. view
  • 10 Aug 2021 in National Assembly: (Lamu (CWR), JP): Ahsante, Mhe. Spika. Naunga mkono ombi la Mhe. Ali Wario. Hili tatizo linafaa lisuluhishwe maana likisuluhishwa, hata sisi watu wa Lamu tutafaidi. Ahsante. view
  • 3 Aug 2021 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi name nichangie. Nimejaribu kuweka alama ya nidhamu kwa muda mrefu lakini sikupata. Nafikiri katika mazungumzo haya nitamjibu Mheshimiwa. Mwanzo, ninawapongeza viongozi wa Bunge hili kwa kuweza kuleta huu Mswada. Pili, ninapongeza Tume ya Waqf iliyo chaguliwa na Rais wetu mpendwa ikiongozwa na Mwenyekiti wao, Mhe. Zuber Noor, Sheikh Juma Ngao na Gibsham Sang, Hussein Sharriff na wakili Mwanakitili. Hawa ni wasomi wenye sifa nzuri kwa jamii. Kwa hivyo, walifanya huu Mswada ukawa mzuri na tunauamini. view
  • 3 Aug 2021 in National Assembly: Uzuri wa Mswada huu sio kwamba hii sheria inatungwa sasa hivi. Ilikuwepo lakini kwa upande mmoja, tusema wa Pwani, lakini hii sheria sasa itakuwa ni ya Kenya mzima. Hapo inastahili tuelewe kwa wale ambao bado hawajaelewa. Sheria ipo lakini hii inaongeza maeneo. Pili, mambo ya pesa yameangaziwa vizuri. Itakuwa watu hawana wasiwasi kwamba pesa zimetumiwa vibaya. Mambo haya yameangaziwa vizuri katika hii sheria. Wakati wa kuomba nafasi katika tume, itakuwa mtu anatuma maombi na haitakuwa ni watu wale wale ambao watakuwa katika tume siku zote. Pia, imepatiwa nafasi na uwezo wa kujiendeleza. Kwa hivyo, ni sheria ambayo imeongezwa ili ifanye ... view
  • 3 Aug 2021 in National Assembly: Pili, si sawa kwa Mbunge mwenzetu kufanya kama lugha ya Kiswahili ni dhaifu ambayo haifai na mtu akizungumza Kiingereza ndio anakuwa msomi. Huko kwetu pwani kuna beachboys tele na wanazungumza fluent English na hawakuenda hata darasa la kwanza. Kwa hivyo, asijifanye na kizungu chake pengine amesoma na hana hekma. Waqf ni nzuri na naomba Wabunge wenzangu tushikane na kuipitisha isiwe kama kuna vuguvugu inaendelea. Kwenye mitandao tunaona wanasema Wakristo wanafanyiwa hivi na Waisalamu hawatafanyiwa hivyo. Hayo si mambo mazuri ya kuchochea hapa Kenya. Hapa Kenya tumekaa vizuri na kwa mambo ya dini tumeshikana. Kwa hivyo, tuendelee kushikana kabila na dini ... view
  • 3 Aug 2021 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus