10 Nov 2021 in National Assembly:
Hon. Deputy Speaker, I am sorry, I will not withdraw. Sheria zichukuliwe lakini hii ni Petition na Petition zingine wanaleta nyingi nyingi hatasio nzuri. Kuna watu wanaoumia kule. Wakati wa election ndio wanafanya hivi vituko.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, sijataja jina la Mbunge yeyote hapa ndani. Nashangaa ni kwa nini napewa hizi hukumu.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, nimesema wazi wazi, siyo wote. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, niko tayari kuleta ushahidi.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Siwezi kwa sababu niliyosema ni ukweli.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Hon. Deputy Speaker, I withdraw.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi. Ningependa kuanza kwa kumpongeza Mhe. Didmus Barasa kwa Mswada huu mzuri wa pesa za uzeeni. Kwa hakika, inapofika siku ya mfanyikazi kustaafu, tumbo huwa linakataa kustaafu. Linataka kula kila siku. Pesa hizo zikichelewa kufika, yule mfanyikazi atakula nini? Tunajua kuwa watu wetu wakipata pesa, wanazitumia wakijua kuwa kuna pensheni yao ambayo itawasaidia kule mbele. Kwa hivyo pesa hizo zikichelewa, jambo hilo linamuumiza yule mfanyikazi na anachukua madeni. Hata hiyo pensheni ikifika, haitumii kwa njia nzuri. Wale ambao wanachukua pensheni yao wanatoka sehemu mbali mbali kwa mfano, Kiunga, Mkokoni na Tiwayu. Pengine ...
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
kwa wale wa kuwekeza mfuko wa pesa za uzeeni. Ni mbinu gani tutatumia kuhakikisha kuwa pesa hizo zinafika kule? Pia wao wanatatizika. Hawataki kukosa kulipa pesa za uzeeni lakini hawapewi pesa hizo. Sisi hapa katika Bunge tunafaa kuhakikisha kuwa tumeweka sheria ili pesa za uzeeni za kaunti zikatwe na kupelekwa kwa wawekezaji kabla hazijawafikia ndio waweze kulipa kwa muda unaostahilika. Tusiweke tu sheria. Naunga mkono sheria hii. Ni sheria nzuri na ninajua itasaidia. Lakini hii sheria ikiwepo, tutatafuta mikakati ya kuwasaidia wale wanaotoa zile pesa za uzeeni. Kusema ukweli, hata pensheni ya Serikali huchelewa sana lakini nawapongeza pia kwa ile ...
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hoja hii. Nangojea Mswada wa Waqf.
view