16 Nov 2021 in National Assembly:
yaunganishwa? Naona hivi ni vita baridi dhidi ya wanawake. Kwa saa hii, tunaweza kusema ni wanawake kwa sababu sisi ndio tunakaliwa zaidi hapa Kenya.
view
16 Nov 2021 in National Assembly:
Tafadhali, Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba ulinzi.
view
16 Nov 2021 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunakumbuka vizuri kuwa si zamani ambapo Rais wetu mpendwa, Mhe. Uhuru Kenyatta, alichukua ahadi kwamba atapiga vita ukatili dhidi ya jinsia. Kwa sababu hiyo, tunafaa kuipa tume hii nguvu ili iweze kupigana vita hivyo. Tunafaa kutafuta mbinu ambazo zitaipatia tume hii nguvu ili ipigane vita hivi vita. Kwa mfano, kila kituo cha polisi chafaa kiwe na dawati la kijinsia. Ukitembea, utapata kuwa bado sehemu zingine hazina polisi mwanamke au hilo deski halina nguvu. Ukifika na kuuliza kwa nini mambo yako hivyo, utaona hawako au hakuna mtu wa kuwa hapo. Mbinu nyingine za kuongeza nguvu kwa ...
view
16 Nov 2021 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Itawezekana vipi wanawake wapate haki zao ikiwa wanaume ndio wengi katika police service ? Tukiangalia mfano moja tu, Lamu iko na polisi wanawake 10 tu. Je, wanawake wetu watapata haki zao wapi? Kama Mheshimiwa Sankok hajaelewa hilo, nafikiri itabidi asikize kwa makini ndio aelewe. Sina mengi zaidi lakini napinga Mswada huu. Asante.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi nichangie ombi lake Mhe. Baya.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Ni vyema kuangalia kwa kina mambo ya ardhi. Kuna desturi ya Wabunge wengine, sisemi wote, zaidi wa Miji Kenda, ikifika wakati wa uchaguzi, lao kubwa wanataka kuona ardhi gani inamilikiwa na Bajuni au Muarabu ili watume watu waingie hapo au wasaidie kuzuia court order . Hawana shida na watu wa bara wakimiliki ardhi. Lakini siasa zao siku zote ukiangalia ni hizo nilizotaja. Huu ni uhasidi. Miji Kenda wanakaa sehemu zingine. Lamu tuna Miji Kenda. Tunawaheshimu na wana ardhi. Ni haki yao wawe nazo kwa sababu ni Wakenya. Lakini badala ya wao kuonyesha maendeleo wamefanya kwa miaka mitano, mambo yao ni ...
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
zinatolewa sana. Siasa yao ni kutumia hiyo. Si sawa. Si sawa kabisa. Ichunguzwe. Wakileta maombi wachunguzwe. Ni mahasidi.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, hili ni Jumba la rekodi. Angalia Petition zao zote wanaoleta hapa. Ni kuhusu Waarabu wanaoishi C oast na wao pia ni Wakenya. Mhe. Naibu Spika, I will not withdraw.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, nakuheshimu sana. Lakini nikiwithdraw itamaanisha si hivyo wanaofanya akina Owen Baya.
view
10 Nov 2021 in National Assembly:
Sawa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view