8 Oct 2020 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker for giving me this opportunity to ask Question No. 278/2020 to the CS for Lands: (i) Could the CS provide details of the ownership of the parcel of land marked “Mbwanjumwali Dispensary” in Mbwanjumwali Village, Lamu East Constituency and confirm whether the parcel of land is registered in the name of Lali Bakari Lali (deceased) of ID No.03061116? (ii) Could the CS explain why the adjudication and subsequent issuance of title deeds left out Mr. Lali Bakari Lali leading to encroachment on the parcel? (iii) When will the Ministry cause cancellation of the title deed that ...
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Mswada wa Mamlaka ya Kitaifa wa Usimamizi wa Majanga.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Nimefurahia sana Mswada huu ambao utasaidia Kenya nzima. Unalenga mambo mengi kama moto, na mafuriko, hata kule kwetu kwenye bahari. Ningependa kiwango fulani cha mgao kutoka Serikali kuu kiwekwe hapo kama asilimia 10 au 20. Itasaidia Kenya pakubwa na tutasonga mbele kimaendeleo.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Kwa hakika, kuna majanga ambayo hutokea baada ya muda na bado hatujitayarishi wala kusoma. Kwa mfano, mafuriko. Tunajua miezi fulani huwa na mafuriko lakini huwa hatujitayarishi. Kuna sehemu za Lamu tunajua miezi fulani bahari inakua chafu sana na majanga hutokea hata tsunami. Maji hupanda hadi kwa nyumba za watu. Tunajua linajiregelea lakini huwa hatujitayarishi. Mswada huu utatoa suluhisho kwa majanga kama hayo.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Cha kusikitisha ni kwamba ikiwa kuna kampuni kubwa au mradi mkubwa katika sehemu, kwa mfano, Lamu Port South Sudan Ethiopia Transport corridor (LAPSSET), katika mambo ya bahari inafaa yajitolee kabla kuanza mradi, waweke kitengo cha kusimamia majanga ambacho kitakuwa kikisaidia majanga yakitokea. Lakini hakuna hata moja, ingawa ni rahisi kwao kufanya kitu kama hicho. Watu wanakufa wakati huo, wanapata shida ama wanakataa kwenda kwa bahari lakini kama kungekua na njia ya kuwasaidia, wangekuwa wanaendelea na maisha yao ya kawaida. Watu wanaenda baharini wanapotea na majanga ya kila aina yanatokea lakini kampuni kubwa kama hizo hazitusaidii. Mswada huu utasaidia sana.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Mafuriko na majanga mengine pia yako kwa Kaunti ya Lamu. Hata janga la ugaidi lipo. Watu wanahamishwa makwao haswa Wadi ya Basubwa lakini inajirejerea. Tunashukuru Mwenyezi Mungu iko vizuri wakati huu.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Ukienda upande wa Bara, katika Wadi ya Wito, huwa na mafuriko kila mwaka. Siku zote sisi huteta na KenGen. Lakini tunashukuru Mwenyezi Mungu siku hizi wanaingilia vizuri.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Ukame pia upo. Haya majanga yako mengi na yanajirejerea na huwa kama aibu. Ni kitu ambacho kinarejelea na tunajua hatuchukui hatua yoyote. Kwa hivyo, Mswada huu utasaidia pakubwa na tunaunga mkono sana, angalau watu wetu wapate kusaidika.
view
8 Oct 2020 in National Assembly:
Asante sana, Bi Naibu Spika wa Muda.
view